Friday, January 21, 2011

JAMANI MWENZENU YAMENIKUTA LEO TENA NIMETAMANI KWELI HIKI CHAKULA KITAMU CHA NYUMBANI!!!!

Mlo huu sijala muda mrefuuuu!!
Jamani mwenzenu niko katika msimu mbaya sana, UNGA wa ugali umeniishia. Na nimepita kila duka, nimepata unga lakini ni wa njano PALENTA kwa aliyezoea ugali kama mimi haunogi kabisa. Kwa hiyo nilipoiona picha hii mate wacha yanidondoke. Hali hii inanifanya niimbe wimbo huu NARUDI NYUMBANI EEEH, NARUDI PERAMIHO, NARUDI SONGEA NAKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU..... Au labda tuusikie mwimbaji mwenyewe akiimba Marehemu Dr. Remmy Ongala


NA JAMANI IJUMAA NA MWISHO WA JUMA MWEMA. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE!!!

20 comments:

  1. acha tamaa wewe.

    usinisemee kama napenda kula""""................

    ReplyDelete
  2. Sisi ugali umetuchosha huku dada,fanya utualike tuje huko angalau tusafishe utumbo.

    ReplyDelete
  3. Acha unoko Dada Yasinta weee!

    Na kweli hamna chamshakinywa bora kama kwenye picha hiyo.


    Ukiona asubuhi huna hamu ya chakula, mwamshe mtu yeyote yule karibu nawe mle wote tena sahani moja na utaona ugali UTAKWENDA TU!

    ReplyDelete
  4. Duh umenitamanisha kweli kesho lazima nipike chakula hiki, hakuna cha diet wala nini lol!!!

    ReplyDelete
  5. Mtu kwao na chakula alichokulia kukisahau si rahisi wala si tamaa hii Kamala.

    Usiye na jina unachoka na ugali kweli? hakika ni ajabu!!

    Kaka,GMP!Ungekuwepo ugali mwenyewe hapo sawa ningekula na mtu yeyote na sahani moja kabisaaa.

    Dada M. afadhali wewe umetamani na utakitengeneza mimi siwezi kwani sina ungaaaaaaa:-(

    ReplyDelete
  6. Ameutaka kweli huo ugali, Mdogo Wangu Yasinta, Jamaani! Mpaka kuchagua wimbo [wakurudia huko Ungonini] kama anayvoimba marehemu Remmy Ongala?


    Yasinta, nasikitika kwa hali yako ulimi nje bure, kwani mimi nawe damu moja ikiwa babu zangu Phiri kutoka Afrika Kusini kwelekea Zambia, Malawi na Tanzania walikuja kama haohao Wangoni wanakotokea babu zako!


    Nipe fursa basi tena niongelee zaidi juu ya chakula hicho kwenye picha, labda unaweza uka riwadha ("TAKE COMFORT"???)


    Kusema ukweli ndivyo nilivyokula nami asubuhi ya Ijumaa leo.



    Kasoro ya chakula changu ilikuwa badala ya samaki mkubwa nilikula dagaa.


    ONION (Kiswahili chake nimesahau niulize Kikaburu wanasema "Uie" ikiwa Wazulu wanachukulia kwaWaingerea na kusema "uanyanisi") nakula mbichi na kwa kawaida ni nzuri sana kwa afya kukabiliana na vitu kama vikohozi na mifupa dhaifu. Kama umeolewa usisahau kuongeza ONION kwenye SALAD ya mumeo kwani yasaidia kuzuia magonjwa ya PROSTATE.

    ONION ni nzuri sana!!! Leo hii mdogo-mtu aliyemezwa na tumbo langu alisindikizwa na kaka-mtu GARLIC...wa kuchemshwa lakini.


    Maharage nayapenda lakini leo sikuongeza kwa hofu chakula kitanishinda kwa wingi; na kwakua jina langu ni Manyanya nilidondosha ndani ya sahani hata nyanya chache ndogondogo kwani sikua na muda wa kutengeneza kachumbali.


    CABBAGE ilikuwa imechemshwa bali kwa kuwa (1994) Muhimbili Hospital waliniambia BLOOD GROUP yangu ni "A+", sikuogopa kula hata majani ya SPINACH mbichi. (Nasikia watu wengine wenye damu tofauti SPINACH kama hiyo inawadhuru, chunga sana na usije ukasema umelogwa kwa kusoma ushauri wangu kutoka kwenye blogi ya Yasinta Ngonyani na yeye akafungwa na kukosa huo ugali milele ya milele ikiwa huku anaupenda kufa! Kifupi mie sidaktari!).

    Kifupi (tena ya miwisho), Dada Yasinta, uchaguzi bora wa chamsha-kinywa ndio msingi wa watu wote na tutawapoteza rafiki zetu wapendwa wenye blogi yako kwa sababu moja tu: WANAKULA NINI KILA SIKU KAMA CHAMSHA-KINYWA? ANDAZI NA CHAI YA SUKARI? UMEKWENDA NA MAJI!!

    ReplyDelete
  7. Mhh ugali, wengine wanaita nguna...hapa Dar, chakula cha nguvu kwa watu wenye nguvu au sio

    ReplyDelete
  8. karibu kwetu mamito hicho ndiyo chakula changu kikuu

    ReplyDelete
  9. Hiyo sahani mimi imenikumbusha J.K.T enzi zile!

    ReplyDelete
  10. Umenikumbusha mbali, chakula hicho ni kizuri mno. Hongera kwa kukipenda kwan ni chakula kizuri.

    ReplyDelete
  11. mambo ya msosi wa nguvu!! Huku tunao huo unga lakini si unajua tena masuala ya kusafirisha msosi yalivyo na masheria kibao?? Ngoja nitacheki na kukujulisha. Pole na udenda!!

    ReplyDelete
  12. ha ha ha ha ha ha ha!!!!
    SHIBE SHIBEEEE
    HAINA BEIIII
    SHIBE SHIBEEE,
    HAINA BEIIII,
    NAENDA KULA NYUMBANI....
    HAINA BEIIIII
    KWANI NYUMBANI NI NYUMBANIIIII
    HAINA BEI,
    HATA KAMA KICHAKANI,
    HAINA BEIIII

    nimelazimika kuyakumbuka maneo yaliyomo katika kiitikio cha wimbo wa NYUMBANI NI NYUMBANI kilichoimbwa na Juma Kassim a.k.a Juma Nature na lile kundi lake la zamani la WANAUME.

    ni kibao kikali kweli.

    yaani SHIBE nyumbani haina BEIIIIII
    ha ha ha ulolili lenu, lighandu ukosili. nkoyoli kwawaka.
    huyoooooo Yasinta poleeeeeeeeeeeeeeeeeee ha ha ha ha ha haki ya mungu nihekili hadi matumbo ghanivinili mwengaaaa ha ha ha ha ha ha ha ha ha

    ReplyDelete
  13. Ahsanteni wote kwa mchango wenu- Ila si utani hapa ni kweli nimeishiwa unga na ni kweli natamani kweli kweli ugali si mchezo....

    ReplyDelete
  14. Yasinta mimi nimeshakwambia lete anuani tukutumie lakini wapi.. Haya shauri yako.

    ReplyDelete
  15. pole dada yasinta, napenda nikutumie, lakini sijui nitakutumiaje.

    ReplyDelete
  16. UMENITAMANISHA NA NINANJAA SAIZI UNGEKUWA INAWEZEKANA NINGEUTOA KWENYE INTERNET.SSSSSSSSSSSASASSSSSSSSSSS KWAKWELI NI MTAMU. NIPE NJIA YA KUKUTUMIA UNGA WA MUHOGO.

    ReplyDelete
  17. Sjui nikaupike leo umenitamanisha sana

    ReplyDelete