Thursday, December 30, 2010

"MJADALA ULIOVUNJA REKODI KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO MWAKA 2010"

Ndugu wasomaji wa blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO, katika kupitia mada mbalimbali nilizowahi kuweka humu ili kupata ile ambayo ilivuta hisia za wasomaji wengi na kuleta changamoto, nimevutiwa na mada hii ambayo ilileta vuta ni kuvute miongoni mwa wadau wa blog hii.
Kwa hiyo basi nimeichagua mada hii kuwa ndio mada iliyovunja rekodi kwa mwaka 2010.
Natoa shukrani kwa wadau wote mlioshiriki katika kuichangia mada hii.
Naomba muungane nami katika kujikumbusha kile kilichotokea katika mjadala huu.
Hospitali ya Ludewa/ Mambo ndio haya!!


Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua, kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu.
Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma

Inasikitisha: Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini. (picha na Albart Jackson).
Na: Yasinta Ngonyani kl. 1:14 AM

NA HAYA YALIKUWA NI MAONI YA WADAU...........

Koero Mkundi said...
Bora umeona na wewe Yasinta maan ningeona mie ninganangwa kweli na wahafidhina....
haya sijui na wewe utaitwa Femisist, kama mie...
Nakusikitikia kwa kuingia katika vita hii, jiandae kushambuliwa dada.....
April 8, 2010 7:20 AM

Yasinta Ngonyani said...
Koero mdogo wangu!Wala siogopi kabisa waiti watavyo na wanishambulie watavyo kwani atayefanya hivyo basi hajui utu na bado hajajua wanawake wana mateso gani na sio haki kupata mateso kama hayo. Tuna haki na tunatakiwa kupata.
April 8, 2010 7:40 AM

Anonymous said...
siku zotw huwa nanyata katika uwanja wako lakini leo nitacomment,huku ni ludewa kwetu na hii ilibiniwa kutokana na wananchi wanaoishi mjini ludewa kuwa na wageni mpaka 3 kwa mara moja (rejea extended family theory ya kiafrika) wakisubiri kujifungua hivyo ukabuniwa mradi huu wa kuwa na jengo lao.angalau sasa wanapumua...pia jengo hili lilitaifishwa toka kwa mjasiliamali mzalendo enzi za mwalimu......wageni wa hapa wengi ni wakisi,wamatumba,wamanda wapangwa ni wachache kwani huhudumiwa na lugarawa mission hospital

April 8, 2010 8:21 AM

Mija Shija Sayi said...
Mimi huwa nasema serikali inatakiwa ipinduliwe maana haifanyi kazi zake ipasavyo, sasa mwakilishi wa jimbo hili sijui ni nani ambaye anashindwa hata kupeleka ripoti serikalini kwa hospitali Ludewa hazina huduma nzuri.
Yasinta ukipata na picha za wodi za wanaume na watoto pia tuletee tuone nao wako katika hali gani.
April 8, 2010 9:19 AM

Baraka Chibiriti said...
Kwakweli maisha yetu yanasikitisha sana tena sanaaaa....basi tuu Mungu anatusaidia sana kutulinda kuendelea kwenda mbele na maisha haya ya tabu. Poleni sana akina mama jamani.
April 8, 2010 10:02 AM

John Mwaipopo said...
namnukuu mija shija sayi "Yasinta ukipata na picha za wodi za wanaume na watoto pia tuletee tuone nao wako katika hali gani."
nadhani za wanaume zitakuwa nzuri tu.
April 8, 2010 10:10 AM

Anonymous said...
kiukweli hii ni waiting home ya akina mama wanaosubiri siku zao zotomie,sio ward,kiuhalisia ward yao na inatosheleza mahitaji.na hii nyumba iko nje ya mazingira ya hosp yenyewe.si kweli kuwa kuna huduma mbovu za wazazi .............wa mkondachi
April 8, 2010 10:54 AM

Koero Mkundi said...
Ngoja ninukuu annony wa hapa.
"kiukweli hii ni waiting home ya akina mama wanaosubiri siku zao zotomie,sio ward,kiuhalisia ward yao na inatosheleza mahitaji.na hii nyumba iko nje ya mazingira ya hosp yenyewe.si kweli kuwa kuna huduma mbovu za wazazi .............wa mkondachi"
Mwisho wa kunukuu.
Kama hiyo kweli ni waiting home, ina maana kuwa hakuna vituo vya afya katika vijiji hivyo tajwa mpaka watu wakimbilie katika kituo hicho cha Afya cha Ludewa ambapo inabidi walundikwe kwenye hizo nyumba za kusubiri kujifungua.
kwa hiyo hata huyo mbunge wao hayajui madhila ya watu wake maana kama angeyajua basi wanawake hao tunaowaona hapo wangeshaondolewa tatizo hilo.
Ikumbukwe kamba walioshinda kwa ushindi wa kishindo walituahidi maisha bora kwa kila mtanzania na ujenzi wa zahanati kwa kila kata. sasa miaka mitano ndio hiyo inaishia........Je watakuja na msamiati gani?
Mimi nadhani kuna haja ya wananchi kuambiwa ukweli kuwa CCM imechoka na sasa ikae pembeni ili watu wenye utambuzi na uwezo wa kuongoza washike hatamu......hakuna haja ya kuimba CCM nambari wani kila baada ya miaka mitano wakati hata hawapo kwenye 100 bora.
Kwanza takwimu zinaonyesha kuwa kuna idadi kubwa ya vijana hapa nchini ukilinganisha na wazee.....nadhani tunatosha kabisa kuondoa huu unafiki, watu mpaka meno yanang'oka kwa uzee lakini wamo tu kwenye siasa.....

nasema wameshindwa waondoke.....
nakubali kuwa wazee wanao mchango wao kwa taifa lakini kama hawazalishi idea za kulikwamua taifa hili kuondokana na tabia ya kuombaomba, lakini wameshindwa, basi wapumzike na tunawaahidi kuwalea na kuwatunza mpaka mungu atakapowachukua mbele ya haki ambapo huko watajua kile walichopanda tangu kuwepo kwao hapa duniani.
Narudia ena waondoke hawatufai.....
April 8, 2010 1:05 PM

Anonymous said...
Nikubali kutoka kwa koero kuwa huduma za uzazi katika vijiji si njema ndio maana akina mama hawa huja katika hospitali ya wilaya kwa huduma mapema zaidi na hutakiwa kusubiri katika nyumba hii.wanashauriwa kuja mapema ili kuepuka any complication ambayo inaweza kujitokeza ilikupata huduma mara uchungu unapoanza.viji vyenye angalau ya huduma ni manda,luilo,madunda,mlangali,makonde na lupingu kidooogo,but still vituom hivi si vya kutegemea sana kwani huduma thabiti pekee ni hapa ludewa na lugarawa mission hosp pekee.Koero pia hii ni wilaya katyi ya chache zinazowakilishwa na wabunge maprofesa,hapa yupo mh.Prof Raphael Mwalyosi.hao wasomi wataalamu wa afy ahawaja motishwa kwani huku ni moja ya wilaya ni tata kimazingira.......wa mkondachi
April 8, 2010 2:40 PM

Ramson said...
Name Raphael Mwalyosi
Surname Mwalyosi
First Names Raphael Benedict
Alternate Name
Title Prof
Country of Birth Tanzania

Positions
From To Organisation Position
2005 Ludewa Constituency
MP for Ludewa
Date of Birth 3 Dec 1946
Political Affiliation CCM

eMail
Telephone
Address
Notes EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Agriculture, Norway PhD 1988 1990 PHD
University of Dar es Salaam MSc. 1975 1979 MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam BSc. 1971 1974 GRADUATE
Tabora Boys' Secondary School A-Level Education 1969 1970 HIGH SCHOOL
Tabora Boys' Secondary School O-Level Education 1965 1968 SECONDARY
Madunda Middle School Primary Education 1961 1964 PRIMARY
Lufumbu Primary School Primary Education 1957 1960 PRIMARY
--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
University of Dar es Salaam/IRA Professor 1999 2005
University of Dar es Salaam/IRA Associate Professor 1993 1999
University of Dar es Salaam/IRA Senior Reseacher 1988 1993
University of Dar es Salaam/IRA Reseacher 1984 1988
Rufiji Basin Development Authority Ecologist 1979 1984
Tanzania National Parks Reseacher 1974 1979
--------------------------------------------------------------------------------
[ Retrieved on 13/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
April 8, 2010 3:04 PM

Anonymous said...
Namshukuru ramso kwa kupachika cv ya mheshimiwa wetu,na kama ujuavyo wataalamu wa mazingira ni wakereketwa wa nature zaidi kuliko vitu vingine kwani alishawahi endesha IRA pale UDSM IRA ni Institute of Resourcr assesment.Lakini kipimo cha picha hii tu kitatutosha kujudge au tukusanye takwimu zaidi lakini hata hali ya shle si njema sana na barabara hata uchumi pia au siju tumpate injiania aongeze na kasi ya uchimbaji wa makaa yetu ya mawe na chuma cha pua kule liganga,nina hamu nishuudie maana tangu nazaliwa niu habari ya upembuzi yakinifu mara mtalamu mshauri maka leo...daa twachoka......wa mkondachi
April 8, 2010 3:42 PM

Mbele said...
Hii makala imenigusa kiasi cha kuiweka kwenye blogu yangu, pamoja na utangulizi ambamo nimegawa vidonge kwa wahusika. Bofya hapa.
April 8, 2010 4:23 PM

PASSION4FASHION.TZ said...
Maisha bora kwa kila mtanzania.....?kweli? au watanzania ni wadanganyika kama watoto wadogo,wanaoambiwa usilie nikirudi nitakuletea pipi,mtoto ananyamaza na anakuwa na hope kuwa mama akirudi ataniletea pipi.
Jamani carne hii watu bado wanaishi maisha kama haya kweli? kinachosikitisha zaidi wanawake ndio wapiga kura wazuri wa kuichagua CHUKUA CHAKO MAPEMA(CCM) wanawake tuamkeni CCM haina shukurani wala fadhila, hawa wanawake wanahitaji msaada wa kuelimishwa,nahisi bado kuna watu wanamawazo finyu kuwa bila CCM haitakuwa Tanzania,kwa hali kama hii basi hayo maisha bora kwa kila mtazania zitabaki kuwa ndoto za alinacha!
April 8, 2010 4:52 PM

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...
kwani nyie si mko mijini?? mbona mimi nimebanana vijijini natoa hudma kwa wana vijiji. sasa nuoe kama wasomi na wabunge mko mijini mnalilia lia tu. anayeona huruma akawe diwani
lakini kwa wanawake ni kawaida kwani ndio wapiga kura wakuu
April 8, 2010 4:53 PM

Anonymous said...
Yasinta asante sana kwa kutujulisha yote haya mungu akuzidishie akupe afya njema wewe na familia yako. Ubarikiwe sana.Unapatwa na uchungu unalia unashindwa kujua ufanye nini? Mimi natokea Ludewa. Huu ni ujumbe ambao mkuu wa nchi ulitakiwa umfikie halafu ajitetee. Nafahamu si Ludewa peke yake lakini ni wilaya na vijiji vingi vina mapungufu haya. Huu ni upuuzi wa serikali yetu halafu tunawachagua viongozi wale wale wenye kujaza matumbo yao na kuwasahau wananchi. My take fukuza kazi watu wote husika kuanzia wizarani mpaka tukafike Ludewa kwenyewe huu ni upuuzi. Wanaludewa tufanyeje kukabiliana na hili? Kama tunaweza kufanya kitu basi wajameni tuwasiliane.Kukaa mbali na nyumbani hakuna maana tutashindwa kuleta msaada
April 8, 2010 5:21 PM

Yasinta Ngonyani said...Anony wa April 8, 2010 5:21 PM! Asante unajua ni kweli nimelia sana kutokana na jambo hili. Nimeshuhudia jambo hili kwa macho yangu wakati naishi Kijiji cha Kingoli kulikuwa na zahanati, lakini hakuna sehemu ya akina mama wajawazito kujifungulia na akina mama wengi walikuwa wana kufa. Hoospitali ya karibu ilikuwa ni Peramiho na kufika huko usafiri wake ulikuwa ni kutembea na mgonjwa/mamamjamzito amebebwa katika machela. Kufika Peramiho inachukua siku mbil. Je huu kweli uungwana?
April 8, 2010 5:44 PM

Anonymous said...
Hii picha imenisikitisha sana. Kwa hakika najua hiyo sio wodi ya hao akina mama wajawazito kama alivyosema mchangiaji mmmoja. Nafahamu utaratibu uliopo kule maeneo ya kwetu, ni kwamba akina mama wajawazito huwa wanapangiwa tarehe za kusogea jirani na hospitali ili kujitazamania kusudi siku ya kujifungua isiwe shida kufika hospital na kupata huduma inayostahili. Nafahamu hivyo kwa vile binafsi natoka jirani na hospitali kubwa na ya uhakika ya misheni Peramiho (kuna mpango wa kuifanya hospitali ya rufaa). Na katika utaratibu wa hiyo hospitali ni kwamba hata kama unatoka km kadhaa toka hospital ni lazima uende kujitazamia hapo hospital na tarehe za kwenda hapo wanakupangia wao wenyewe. Pale kwetu usafiri wa kufika Peramiho ni masaa 24 lakini hiyo hospital ni wakali sana, lazima uende kabla. Ukiuliza wanakupata vipi mpaka wakuamuru kwenda hapo mapema ni kwamba kama mjamzito anahudhuria clinic basi hapo ndio wanapokupata na kukuingiza katika utaratibu huo. Sasa hoja ninayotaka kusema hapa ni kwamba huu ni mpango mzuri sana hasa kwa maeneo ambayo huduma za hospital zipo mbali. Lakini sasa inabidi kuyafanya hayo mazingira yawe mazuri, yavutie na akina mama wakiwa hapo wawe na amani na sio kuwaweka katika mazingira kama hayo ya kwenye picha.
Inasikitisha sana kwa kweli hizo picha.
April 8, 2010 9:40 PM

Yasinta Ngonyani said...
ninenukuu toka kwa Hapa kwetu yaani Pro.Mbele kwa vile nimeyapenda haya maelezo yake! "Inasikitisha kuwa katika nchi yetu, yenye mali nyingi, hali ya watu katika vijiji vingi na mijini ni mbaya kiasi hiki.
Wenye madaraka wanafuja utajiri wa Tanzania. Kwa mfano, hivi karibuni tu, CCM imeagiza magari 200 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi. Fedha hizi zingeweza kutumiwa kuboreshea huduma za afya kwenye hospitali kama hii ya Ludewa, au kuwapa mitaji hao akina mama, wakabadilisha maisha yao.
Wako ambao wanachuma mishahara na marupurupu kwa mamilioni ya shilingi. Wako ambao wanatumia mamilioni kwenye sherehe na starehe. Wengine wamechota na labda bado wanachota, mamilioni ya shilingi na kuyahamishia nje, kwenye akaunti binafsi. Badala ya kutumia hela kuboresha huduma za afya sehemu kama hii ya Ludewa, Tanzania imetumia mabilioni ya shilingi, tangu miaka ya mwanzo ya Uhuru, kwa kuwapeleka wachache nje, kwa matibabu au hata tu kuchekiwa afya, mambo ambayo yangeweza kufanywa katika hospitali za nchini, kama vile Muhimbili. Ninafahamu jinsi gharama ya matibabu ilivyo mbaya katika nchi kama Marekani. Fedha zilizotumika miaka yote hii zingekuwa zimeboresha huduma katika hospitali sehemu mbali mbali za nchi." Mwisho wa kunukuu. Ni kweli inaumiza na kusikitisha shana na ningependa hii serikali ipinduliwe kabisa! Upendo Daima.
April 9, 2010 12:44 AM

Mija Shija Sayi said...
Yasinta, swali muhimu linakuja sasa wa kuipindua ni nani katika jamii yetu hii iliyofunzwa nidhamu ya WOGA?
April 9, 2010 1:18 AM

Yasinta Ngonyani said...
Da Mija ni sisi vijana wa leo au? ni lazima kuna mmoja asiye mwoga.
April 9, 2010 3:19 PM

Albert Paul said...
"Tanzania na Watanzania tuna amani" hii ndio hirizi iliyofungwa kwenye vichwa vyetu imiminayo nidhamu ya "WOGA" kwenye akili zetu. Mawazo haya "POTOFU" tumeyakumbatia kiasi kwamba yanatufanya tunashindwa kutetea haki zetu ipasavyo na kukosa umoja miongoni mwetu.
April 9, 2010 7:53 PM

penina Simon said...
Ha ha ha maybe yatasaidia jamani,manake mimi kwa uzoefu wangu sidhani kama mimba ni ugonjwa, ila hufuata unavyojiendekeza,
Mfano inaweza kukufanya uteme mate kila wkt na ukiendekeza utajikuta unatembea hadi na kikopo. Au kukuletea uchovu na ukiiendekeza basi utaamuka sa4,5..
etc.
April 10, 2010 3:23 PM

samuel blandes said...
Inasikitisha,Kliniki au hospitali kama hizo ziko nyingi nchini.Serikali isikimbilie kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi au idadi ya wilaya ni matumizi mabaya.Gharama za kujenga kliniki 20 na kuziendesha vizuri ni nafuu kuliko gharama za kuongeza jimbo mmoja la uchaguzi.Kupanga ni kuchagua.
Rwegasira
Singapore
April 11, 2010 8:29 AM

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
Enzi za Prof Mwalyosi pale IRA mambo yalibadilika yakaifaya IRA ikatoka kuwa Institute of Resource Assessment ikawa Institute of Resource Assassination kwani Environmental Impact assessments za ajabu ajabu zilikuwa na bado zinafanywa na watu wa taasisi hiyo. Utaona miradi mikubwa ambayo utategemea kuwa haitopitishwa lakini waapi!!!
Hayo yanayotokea Ludewa yako kila pahala na ukistaajabu ya hospitali za wilaya utakuta kuwa hata hospitali za mikoa kama Mara utayakuta :-(
April 12, 2010 8:19 AM

nkwera said...
Yasinta
Hii picha umepewa au umepiga mwenyewe?
Mimi ninaishi mita chache kutoka kwenye nyumba hizo.
1. Hiyo siyo wodi ya akina mama, wodi ya akina mama wajawazito Ludewa ina vitanda zaidi ya 6o
2. Nyumba hiyo ipo ukingoni mwa eneo la hospitali na hutumiwa na wote wenye wagonjwa hapo hospitali lakini hawana pa kufikia. Bionafsi naona ni jambo jema hata nyumba si nzuri
3. Akina mama wanaosubiri kujifungua au wenye magonjwa hatarishi walishajengewa na vosacom foundation jengo zuri tu, ungeweza kuomba picha zake au kupiga mwenyewe:-) Habari zake zinapatikana hapa http://www.jambonetwork.com/blog/?p=59059
Hali ni mbaya vijijini lakini picha ulizotumia si sahihi na sielewi ulikuwa na nia gani kutumia picha hizo. Bottom line, those are not wards and probably you know it!
pdn
April 13, 2010 8:27 PM

Yasinta Ngonyani said...
Kaka nkwera ahsante kwa taarifa na hiyo link nitapita kuangalia.
April 13, 2010 10:51 PM

Simon. said...
poleni sana ndugu zetu watanzania wa huko ludewa na maeneo ya jirani na hapo ambao mnategemea matibabu kutoka katika hiyo hospitali. lakini sio ninyi tu huko hata sehemu mbali mbali za hii nchi wote wanateseka sana hasa linapokuja suala la hospitali na huduma za kina mama wajawazito nchini..hii ni kutokana na usimamizi wa serikali yetu kuwa ni wa kubabaisha!NADHANI NI WAKATI MUAFAKA SASA KWA SERIKALI KUWA SERIOUS KATIKA KUTATUA MATATIZO SUGU YANAYOWASUMBUA WALIPA KODI WA NCHI HII!!! tumeshachoka na sanaa zao!
April 15, 2010 5:36 PM

Anonymous said...
dada yasinta nipo mbioni kutangaza nia ya kushirikiana na wananchi kuondoa kero hizi sasa hakuna haja mpaka kusubiri "KUOMBWA NA WAZEE"wenye nia ya dhati trujitokeze si ubunge tu hata udiwani uongozi wa vijiji na mitaa unahitaji watu makini na wenye upeo wa kuondoa kero na si kuiongeza kero kama hizi.IWE NI WODI ISIWE NI WODI IREKEBISHWE HUDUMA ZA HAPA HAZIKIDHI VIWANGO VYA AFYA.Tuzindukesasa na tusababishe hali njema
April 20, 2010 10:56 AM


6 comments:

  1. MOANI YALIKUWA MAZURI, LAKINI YALIKOMEA NJIA PANDA YALILAUMU. JE TUFANYE NINI SASA?

    SWALI TU HILI WAHESHIMIWA MSIKONDE

    ReplyDelete
  2. Na ndipo wote waliponyamaa kimya baada ya kukosa jibu. Akarudia tena "Je tufanye nini sasa?" Hapakuwa na wa kuweza kujibu swali hilo. Ndipo nikajua kuwa umaskini wetu si wa khali bali na fikra pia. HAAA! Naota tu!!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana sana kwa blog nzuri> Natumai mwaka mpya mambo yatakuwa hivi na zaidi.

    ReplyDelete
  4. kama ingekuwa pombe, tungesema kutoa na kusoma maoni ndicho kiwango cha ulevi (alcohol content in percentage) kilichomo ndani ya kinywaji kinaitwa 'kublogu' (blogging). kublogu kumekuwa kama ulevi fulani ambao kama vilevi vingine vina addiction. Kesho unatamani kublogu tena, na kesho..., na kesho..., na kesho...

    naam na mwaka kesho pia panapo majaaliwa.

    ReplyDelete
  5. kwani bado hali hii ipo, au wahusika wameiona wakarekebisha mambo?

    ReplyDelete