Friday, December 17, 2010

KUMBUKUMBU KWA MAMA YETU ALANA NGONYANI!!!!

Hapo ni mama Alana ni huyo aliyekaa na mimi
nikimsuka mwaka 1997 kijijini Mahumbato Mbinga!!!
Nimeamka leo nikia na majonzi mengi kwani hii tarehe huwa inanikumbusha sana mama. Kwani ndio ilikuwa tarehe ambayo alituacha ni 17/8/2004, kwa hiyo leo ni miaka 6 na miezi 4. Nina mengi ya kuongea nawe mama, kuna wakati huwa nadhani upo nasi na nachukua simu na nataka kuongea nawe, nataka kuisikia sauti yako, kicheko chako pia kukumba ushauri/mawazo. Na mwisho nabaki nikitoa machozi. Mwe!!!.

Halafu natamani kweli kukusimulia jinsi wajukuu wako wanavyoendelea pia makuzi yao. Wao pia wanakukumbuka sana. Unakumbuka mara ya mwisho uliwapa zawadi Camilla ukamnunulia gauni na Erik shati na kaputula, bado wanavitunza mpaka leo. Na wanaviabudu mno.
Najua unanisikia huko uliko, sisi wote tunakukumbuka sana mama Ustarehe kwa Amani. SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA ZAIDI. AMINA.
Mama ngoja nikuwekee huu wimbo wako ambao ulikuwa ukiimba tangu mimi nilipokuwa mgongoni.


AU MIMI NAMI NIKUKUMBUKE KWA WIMBO HUU HAPA CHINI NA KAKA ALBINO FULANI!!!!


22 comments:

  1. Pole Dada Yasinta.Ndio safari yetu wanadamu wote.Mungu na akupe nguvu ya kuuhimili upweke.

    ReplyDelete
  2. Tuko pamoja nawe ewe mpendwa dada yetu...

    ReplyDelete
  3. Yasinta. Majonzi na huzuni yako vinasikika vyema. Pole!

    Badala ya huzuni na majonzi pengine ni vizuri kama ungeigeuza siku hii kuwa siku ya kufurahi na kusherehekea maisha ya mama. Yeye alikuja kutoka alikotoka, akatimiza lililokuwa limemleta na akaenda alikoenda (au pengine tuseme akarudi alikotoka). Kwa nini basi hili lisiwe jambo la kufurahia hasa ukizingatia kwamba hii ndiyo njia yetu sote wenye mwili?

    ReplyDelete
  4. Yasinta sikufahamu lakini kwa kusoma blog yako tu nadhani tumefahamiana. Sisi sote ni ndugu. Pole sana kwa hili lakini kumbuka kwamba yupo nawe kiroho amekuacha kimwili. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kuweza kuvumilia.

    ReplyDelete
  5. Edna! asante sana kwa kunipa nguvu ya kuweza kuumili upweke huu.
    Simon! Ahsante sana.
    Kaka Mrope! pamoja sana.
    Adela! shukrani

    Kaka matondo hakika umenena. Nakushukuru sana kwa hayo uliyosema kwani kuna kitu nimejifunza.

    Usiye na jina nawe kwanza karibu sana Maisha na Mafanikio na ahsante sana kwa ulilo sama. Ningefurahi kama ningejua jina lako.

    ReplyDelete
  6. Oh Yasinta pole sana mpenzi,maisha ndivyo yalivyo sio wewe peke yako tuko wengi tuliopoteza wazazi,mimi huwa namshukuru sana mungu kwa yote,na bado huona kama niwenye bahati kubwa kuwa na wazazi katika maisha,huwafikilia wale watoto wanaoachwa na wazazi wao wakiwa wadogo.

    ReplyDelete
  7. Pole sana, Dada Yasinta. Mungu aendelee kukujalia nguvu. Naona niseme tu kuwa hii tarehe imenipa mshtuko, maana nilizaliwa tarehe 17 Agosti.

    ReplyDelete
  8. PASSION4FASHION.TZ! Ahsante nakubali ni wengi wamepoteza wazazi na wapendwa wao. Na inabidi tusiwasahau.

    Prof. Mbele! Oh! kwanza asante kwa kunipa pole lakini ndo maisha na pole na wewe kwa kupata mshtuko kama huo basi nitakuwa nikimkumbuka mama nitakuwa nakukumbuka na wewe kwa siku hii.Ahsante sana. Pia najivuna sana kuwa na akina kaka, dada, wadogo, jamaa na marafiki kama ninyi ambao mna moyo wa pekee wa kumpa mtu nguvu, imani na utulivu. NAWAPENDENI WOTE.UPENDO DAIMA.

    ReplyDelete
  9. Mzee MMN!! Niliandika ujumbe kama huo lakini nikafikiri na nikaufuta kwa kumuogopa dada Yasinta... uliyoyasema ni kweli, Dada Yasinta wapaswa kumshereheka mama yako daima na isiwe jambo la huzuni. Kwetu sisi marafiki zako yeye ni shujaa wetu kwa kutuletea rafiki mkarimu na mwenye busara kama wewe!! Hivyo basi twamsherehekea. Nawaza kwa maandishi tu!!

    ReplyDelete
  10. pole Yasinta kwa kuwa mbali kimwili na mama lakini ktk sala tupo naye..Tuzidi kumwombe apumzike kwa amani.amina

    ReplyDelete
  11. Kaka Mrope kwanini uniogope mimi? wala huna sababu ya kuniogopa mimi ungejua huo ujumbe nimeupenda sana. Na nilipokuwa nikisoma mpaka chozi likanidondoka kwa furaha ya kuona ni jinsi gani nipo karibu nanyi ndugu zangu na jinsi mnavyonipenda.
    Edo! ulikuwa wapi kwanza Ehh! umekuwa kama mwana mpotevu kakangu. Ahsante kwa kujitokeza hapa na kunipa pole. Usipotee sana bwana!!!

    ReplyDelete
  12. tumuombee kwa mungu apumzike salama

    ReplyDelete
  13. Pole da'Yasinta, tuzidi kumuombea mama yetu aliko azidi kupata mapumziko mema wakati tukiyatekeleza na kuyatimiza aliyopenda kutuasa

    ReplyDelete
  14. Ahsante sana kaka Mathew Upendo Daima !

    ReplyDelete
  15. Da Yacinta,
    Hicho ndicho kilimwengu
    Japo kinayo machungu.
    Bora jikaze mwanangu,
    Maisha kizunguzungu.

    Leo ni kwako najua,
    Kesho wengine elewa.
    Tumshukuru Bahawa,
    Kwa kila tulipatalo.


    Pole dada Yacinta,
    Ukubwa una matata.

    ReplyDelete
  16. Ka´NN Mhango!
    NANUKUU "Hicho ndicho kilimwengu
    Japo kinayo machungu.
    Bora jikaze mwanangu,
    Maisha kizunguzungu."mwisho wa kunukuu. Kweli maisha kizunguzungu Najikaza sana lakini kuna wakati unajikuta unashindwa.Ahsante sana kwa kunipa moyo na kunifariji. Kweli kuwa na marafiki kama ninyi ni jambo la kujivuna .UPENDO DAIMA.

    ReplyDelete
  17. Pole dada Yasinta,ni mara yangu ya kwanza kuchangia ktk blog yako lakini ni msomaji mzuri sana na nimejifunza mengi kupitia kwako yaani nakuona kama dada yangu mzaliwa nawe,kwa hili umeniliza saana tuu nimesoma comment,nimesikiliza nyimbo,yaani machozi yamenitoka utadhani nimeletewa habari ya msiba,nafikiria ni jinsi gani unam-miss lakini muachie mungu,mama ameacha KOPI ambayo ni wewe hivyo fanya yale yote aliyokufunza busara na hekima zake na watoto wako pamoja na sisi tutanufaika kupitia kwako kama ulivyonufaishwa na mama.mungu akupe nguvu na moyo wa kumuombea dua..

    ReplyDelete
  18. MRS! Ahsante sana nashukuru kwa kulia nami na karibu sana Maisha na Mafanikio. Ila ningefurahi kujua jina lako kamili.Karibu tena.

    ReplyDelete
  19. kumbe na wewe ulicheza michezo ya utoto, manake zamani tukishindana kusuka majani, ndio ilikuwa michezo ya kizamani, siku hzi hata kusuka mabutu unakuta msichana hajui, akifumua nywele gafla hadi ajatafute mtu wa kumfunga

    ReplyDelete