Wednesday, December 15, 2010

2010-KUELEKEA MWAKA MPYA 2011

Tafadhali nisaidieni kupata ufumbuzi wa swali la hicho kitu kinachoitwa mwaka mpya maana nimekuwa najiuliza miaka kibao sijapata hasa kujua hicho kinachoitwa mwaka mpya nini.

Mimi nimekuwa na mtazamo ninauambatanisha ili nanyi mnisaidie kupata ufumbuzi ambao naamini utawasaidia watanzania wengi

Naitwa Salehe Msanda niko Njombe Tanzania


SWALI HICHO KITU KINACHAOITWA MWAKA MPYA NI NINI AU NI KITU GANI?

1.SIKU YA KWANZA YA MWEZI JANUARI-1/1

2.NI TUKIO LA SIKU YA KWANZA YA MWAKA.

3.NI MABADILIKO YA KUTOKA KATIKA HALI MOJA KWENDA NYINGINE NA HASA KUMALIZA SIKU 365
NA KUZIANZA ZINGINE 365.

Kila mwaka inapofika mwezi wa 12 na hasa tarehe za kuanzia 15/12 huwa kunakuwa na pilikapilika nyingi za kwanza kuelekea katika sikukuu ya kuzaliwa mkombozi wetu yesu kristo na kumaliza mwaka na kuelekea kuanza kinachoitwa mwaka mpya.

Je tumewahi kujiuliza kwa makini na kupata angalau ufumbuzi/jibu/majibu, wa kitendaliwili cha
hiki kitu kinachoitwa mwaka mpya au tunakwenda tu kimazoea na hivyo kupelekea kuishia katika kufanya mambo kimazoea na kimapokeo?

Tukirudi katika swali na huenda ikiwa moja ya majibu ya hiki kitu tunachokiita mwaka mpya tukianza na jibu la kusema mwaka mpya ni siku ya kwanza ya mwezi januari yaani tarehe 1/1.

Hapa kunajitokeza utata hasa ukizingatia kwa mfano kuna mwaka mpya wa kiislam na kikristo
ambayo yote inaanza katika miezi tafauti kuzingatia na mwaka husika.

Lakini pia kuna suala la kama ni siku ya kwanza ya mwezi januari ni nini hasa kinachapelkea kufanya
siku hiyo kuwa ni ya kwanza na kuwa na umuhimu wa kipekee.

Tukija katika masuala ya hesabu na hasa msingi mkuu wa hesabu yaani kujtmlisha
+,kutoa-,kuzindisha X,na kugawanya .Tuatjikuta tunapata mambo yafuatayo katika siku hiyo ya
kwanza ya mwaka yaani 1/1/2011

Pia ukichukua namba hizo bila ya kuzitenganisha unapata 11 na 20 na namba 11 tena.

Maana yake kwa tafsiri yangu kwa kucheza na namba kwa kuamini kuwa mwaka mpya ni siku ya
kwanza ya mwaka tunapata mambo yafuatayo

Kunakuongezeka katika masuala mbalimbali mfano masuala ya kipato ,neema na kukua

Tukio la pili ni kufuta au kuondoa kile ulichonacho na kubaki ukiwa hauna kitu na hivyo kuanza upya

Tukio la tatu unabaki na kilekile ulichokuwa nacho kiwe kizuri au kibaya itategemea na mtazamo wa
mtu halikadhalika kwa tukio la nne linatubakisha katika hali ile ile.

Ukienda katika kuzitenganisha namba hizo za 1/1/2011 za mwaka tunaotarajia kufika na kwa
kuziweka bila ya kuzitenganisha unapata mabo yafuatayo yanayofanana 11=2,20 pia sawa na 2 na 11 ya mwisho sawa na 2.

Maana yake tunatakiwa kuongeza kwa upande wa mazuri hii ni tafsiri yangu
Pia ukirudi katika msingi wa hesabu na kuamua kutoa 1-1=0,2-0=2 na 1-1=0
Maana yake tunaweza kuongeza au kupunguza na kubaki palepale tulipokuwa
Ukizijumlisha namba zote 1+1+2+0+1+1=6,maana yake tuna nafasi ya kuongeza mara sita ya kile tulichonacho

Tukija katika jibu la pili kuwa ni tukio la siku ya kwanza la mwaka mtarajiwa 2011.
Mkanganyiko unakuja hiyo siku ya kwanza mbona haina tofauti na siku zingine? Maana kutakuwa na asubuhi,mchana,jioni na hatimaye usiku kama siku zote tulizozizoea na kama kwa huku Njombe tunatarajia kutakuwa na baridi kama kawaida yake na mvua.

Mkanganyiko mwingine unakuja iwapo ni tukio la siku ya kwanza utatafaotishaje iwapo imetokea ukapoteza fahamu kuanzia mfano tarehe 29 na kuzinduku siku hiyo maana utashuhudia mambo
nilypotaja hapo juu. Kama utazinduka asubuhi utaona hiyo hali ya asubuhi ambayo umeizoea
na halikadhalika kama ni mchana,jioni na usiku na zaidi utashuhudia watu jamaa na ndugu zako
wamekuzunguka. Na iwapo hautaambiwa kuwa leo ni mwaka mpya hautakuja kupata kitu au ishara itakayokuaminisha kuwa siku hiyo ni mwaka mpya.

Pia kwa upande mwingine tukienda kwa undani matukio tunayatarajia yawe na vitu au tabia
ambazo zinatoa nafasi ya kuona uhalisia wa tuki husika mfano tukio la kuzaliwa,kuna uhalisia hapo wa kupatika kiumbe mwingine ambaye atapita katika hatua za kuelekea kuwa mtu mzima.
Matukio ya u siku na mchana,kuwa na jua na mwezi kuna uhalisi wa kile kinachotokea lakini kwa hicho tunachakiita mwaka mpya sijaona uhalisia unaoweza kutuaminisha kuwa kweli mwaka mpya ni tukio kama matukio mengine.

Tukija katika jibu la tatu la mwaka mpya ni mabadiliko nadhani hapa ndipo tunapoweza kuona uhalisi wa mambo mbalimbali na kutuaminisha kuwa mwaka mpya ni zaidi ya hicho tunachofikria sisi cha siku ya kwanza ya mwezi januari.

Mfano ni ukweli uliowazi kuwa kama tunakubaliana kuwa mwaka mpya ni mabadiliko kama ni
mtoto aliyezaliwa tarehe 1/1/2011 atakuwa amefikia hatua ya kutembea hilo ni badiliko ambalo
wanafamilia wanaritarajia na ni lazima litokea labda kwa kesi chache. Kama ulikuwa unaitwa mr
na mrs Fulani mtakuwa mnaanza kuitwa baba na mama Fulani,lakini pia kama ulikuwa unaitwa
HANDSOME BOY NA BEUTIFULY GIRL utaanza kuitwa handsome man na beautiful woman. Na wale
waliokuwa wanajiita girlfried na boyfried wataanza kujiita manfriend na womanfriends.

Mfano hai sasa hivi dunia yote inapiga kelele kuhusu mabadiliko ya tabianchi kitu ambacho
kinatotokea kama mabadiliko kutoka na baadhi ya matendo ya binaadamu katika kutafuta
kukabiliana na mabadiliko ya mienendo ya dunia ya mabadiliko yanaypotokea katika ulimwengu huu tunaoishi mengine kwa kujua na mengine bila ya kujua.

Mwaka mpya ni mbadiliko inazihirishwa hata katika masuala mbalimbali ambayo wewe na mimi
tunayafahamu,mfano kama kwa wakulima na naamini tuliowengi tumetoka katika familia za
wakulima,shamba limelimwa kwa muda mrefu zao la aina moja huwa tunase,ma limechoka maana yake kumekuwa na mabadiliko yaliyopelekea shamba hilo kuchoka.

Kwa msingi huu kama wote tunakubaliana na jibu la tatu la hicho kinachoitwa mwaka mpya ni
mabadiliko sasa nini kifanyike kuanzia katika ngazi ya familia ambayo ndiyo msingi mkuu wa ujenzi wa masuala yote yanayomuhusu binaadamu na vile vilivyopo juu ya dunia ambayo mwanaadam amebalikowa kuingozo kuiweka chini ya imaya yake na tukirudi katika msingi wa jibu la kwanza katika majibu ya hesabu za msingi wa kuanzia masuala ya msingi

1. Tubadilike kwa kujikagua katika kila Nyanja ya maisha na kutenda kwa kuaongezaa kwa
upande wa kujenga ili kuwa na dunia Tanzania salama ya kuishi kuanzia katika ngazi ya
familia.

2. Tunatakiwa kuwajibika kwa maisha yetu na viumbe tunavyvitawala si kwa chini ya asilimia
60% na asilimia zilizobaki zitajaziwa na wengine. Ukiwajibika kwa zaidi ya asilimia 60% ni
vizuri zaidi.


3. Tuwe watu wa vitendo zaidi badala ya kuzungumza sana ,kulaumu,kulaani na kulalamika kwa
katika hali halisi kulaumu,kulaani na kuongea sana hakujawahi kubadili kile unachakitaka.


4. Tunatakiwa kubadilika kutoka katika hali inayoumiza wengi na kuhakikisha tunakuwa chachu
ya kuona kila mmoja anawajibika kuifanya Tanzania kuwa yenye neema, Furaha, upendo na
ridhiko.


5. Katika ngazi ya familia na walio katika uhusiano ni wakati wakuhakikisha uhusiano
unashamili na kuifanya taasisi ya kale katika dunia hii inayoitwa taasisi ya NDOA kuwa taasisi
yenye msingi imara wa kujenga kizazi kilichopo na kinachokuja.


6. Tukiamini kuwa mwaka mpya ni mabadiliko na tunatakiwa kubadilika kwa kutenda tutafika
mahali kila mmoja wetu atakuwa na furaha ya kweli . Maana inasadikiwa na ndio ukweli
ulivyo KATIKA KUTENDA HAKUNA KUSHINDWA ILI KUNAKUPA MATOKEO YASIYOTARAJIWA
na kama tukiamua kwa nia ya dhati mabadiliko yatakuja kwa haraka, tuache kukata tamaa
haraka na kutarajia kuwa mabadiliko yatakuja haraka kama unavyotuma mesege. Maana
tumekumbwa na electronic life style na kufikiria kila kitu kitatokea kwa mkabala wa
electronic.

Watanzania tusherehekee mwaka mpya kwa mtazamo kuwa mwaka ni suala la mabadiliko katika Nyanja mbalimbali za maisha na mabadiliko hayo yanatakiwa kutufikisha katika kuona maisha ni mazuri na ya kuvutia.

KILA LA KHERI KATIKA KUELEKEA MWAKA MPYA

8 comments:

  1. Da yasinta nafikiri umekusudia

    "2010 KUELEKEA MWAKA MPYA 2011"

    ReplyDelete
  2. Alikuwa na kusudio hilo ,nahisi kutoka mwaka 2010 kuelekea 2011. Na nshukuru kuwa swali limeulizwa na kupewa majibu mazuri. Nafikiri muulizaji au mshenenezaji ni mnajimu!
    Kwangu mimi mwaka mpya, ni kuanza kwa mwaka unaofuatia, na hii ni kwa ujumla, ila kila mtu ana mwaka wake mpya! Na pia miaka hii inaweza kuwa kutegemeana na imani za watu! Ila huu unao-ongelewa sana nii mwaka wa GREGORIAN! Natumai wataalamu wa mambo hayo wanaweza kutoa ufafanuzi!

    ReplyDelete
  3. Mwaka Mpya ni kama siku za hedhi za mwanamke si kila kila wakati katika KUKOKOTOA KALENDA zitaangukia siku ile ile itarajiwayo.

    Kumbuka DUNIA haijatulia katika mhimili[Orbit) wake na kuna wakati inacheza kidogo katika mhimili (tilt) na ukizingatia kuwa hata spidi yake katika kulizunguka jua si sawasawa ndani ya kila kilometa na ukichukulia kuwa hata mzunguko wenyewe sio mduara sahihi kama iaminikavyo,....
    ....na tukiongezea ukweli kuwa KALENDA zimebuniwa tu na watu;....
    ... utagundua kuwa aidia nzima ya BINADAMU kuwa na siku waaminiyo ni siku ya kwanza ya mwaka ni jitihada tu za KIBINADAMU za kujaribu KISAIKOLOJIA kujielewa na kukabili ya kibinadamu na kuyafanya yawe na MAANA MOJA katika kuleta maana.


    Nachojaribu kusema:
    Binadamu kama ahitajivyo JINA ili kutambua nani ni nani katika KUNDI,..
    ...anahitaji KALENDA na vielelezo vingine kama vile ni lini SIKU YA KWANZA ya mwaka , ...
    ...ili tu kujaribu kukabili mazingira na UBONGO aka MIND ili kibunadamu asichanganyikiwe KIRAHISI.

    Kwahiyo:
    Kila siku ni siku ya kwanza ya MWAKA.:-(

    ReplyDelete
  4. nataka kuinunua sentensi yako ya mwisho ya mada...shilingi ngapi itakuwa?


    Kweli, kila siku ni mwaka mpya @Mt Simon

    Unadhani hata ingeitwa siku ya shetani isingekuwa ya mwaka mpya? andalieni waethiopia...wanaadhimisha mwaka mpya tofauti kabsaaa!

    ReplyDelete
  5. Tafsiri iliyotolewa katika mada kuu, inafanana fanana na tafsiri za sheikh Yahya Hussein!

    ReplyDelete
  6. Mie kwangu mwaka mpya ni tarehe 19/February, hiyo ndio siku ya kuuaga mwaka wa zamani na kuingia mwaka mpya na siyo January 1 kama wafanyavyo wengine! Kama wewe ulizaliwa may 10 kwa mfano, iweje usherekee mwaka mpya January 1 wakati hujaingia huo mwaka mpya? Ila kama unazungumzia mwaka mpya kikalenda upo sawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Sawa kaka kitururu,bado sisi kama watanzania tunawasidiaje watanzania katika kubadilika na kukabiliana na dunia kwa mkabala wa mabadiliko ya kijamii,kumbuka wenzetu wao wanatumia kila sekunde katika kuona kuwa wanafanya mmambo ya msingi na ya maana lakini kwa upande wetu bado tuko katika lindi la usingizi. Mfano wakati wenzetu wanaitumia vema fursa ya UFAHAMU NA MAARIFA,kama lugha yao ongozi katika maisha ya kila siku sisi tumejikita katika kitu nianchoweza kukiita lugha ongozi ya STAREHE NA BURUDANI,hii inathibitishwa na juhudi kubwa zinazofanywa katika mfano mashindano ya kuibua vipaji vya wanamuziki BBS bongo star search.
    Badala ya kusisistiza kujipanga na kukabiliana na mabadilko ya kijamii sisi tunajikita katika kulalamika na kulaumu bila kuchukuahatua za msingi na za maana zinazoweza kututoa katika tafrani ya maisha ya ugiligili.

    ReplyDelete
  8. Hata kama Sheikh Yahaya angetusaidia kujibu hili swali, sidhani kama angetoa jibu la kina kama la Baba Mtakatifu!

    ReplyDelete