Jumapili ya kwanza ya majilio/Först Advent!!!
Nimeipenda sala hii ya kaka Baraka Chibiriti na nimeona ni vizuri kuitumia jumapili hii ya leo.Ukizingatia ni jumapili ya kwanza ya majilio haya hebu tusali kwa pamoja.
Nia yangu naileta kwako Bwana Mungu wangu, nakuomba Bwana unisikie ninalia kwa uchungu. Nakuomba uipokee sala yangu, sikiliza na sauti ya kilio changu. Ninajua Bwana siku zote wewe hupatikani kwenye gasia, ninajua siku zote wewe hupatikani kwenye vurugu.
Bwana nijaie utulivu wa moyo na nipe nguvu nimshinde mwovu shetani, shusha roho wako anipe faraja. Bwana niongoze ili nitimize nia yangu ya kuwa mtumishi wako mwema!
Ee Bwana upo wapi mimi ninakutafuta, nitazame kwa huruma nateseka Mungu wangu...nakuomba uipokee sala yangu na uisikilize sauti ya kilio changu.
Hata kama nipo kama takataka mbele za watu...lakini mbele yako mimi nina thamani kubwa sana siku zote, kwa hili niajua na ninauhakika kwamba wewe pekee ndiwe wenye kunithamini, nakuomba uipokee sala yangu na uisikilize sauti ya kilio changu.
Ee Bwana wangu nijalie nikabili njia zangu, nimshinde huyu mwovu shetani hanifai kabisa. Bwana Mungu wangu wewe ndiwe tegemeo la maisha yangu yote hapa Duniani, nitausifu na kuku tegemea wewe daima siku zote za maisha yangu!

Amen
ReplyDeleteaksante
ReplyDeleteamen ubarikiwe na bwana
ReplyDeleteAmin, twaomba dua ikubaliwe!
ReplyDeleteMmmmmmmmmmh!
ReplyDeletehata mi nimelipenda mlongo sasa ulikumbuka kuwasha mshumaa wa kwanza jana? nawatakia majilio kwa wote.
ReplyDelete