Thursday, November 11, 2010

Jamani huu kweli ni Uungwana?/ BOT tunaomba mkopo kujenga hii shule Tafadhali,

Hekalu Takatifu la kifisadi, wakati wadogo zetu huko Kigoma na kwingineko wanasoma kwenyevumbi
wakitafuta Kifua Kikuu na magonjwa mengine. Hii ni nyumba ya watu wawili,

Hekalu la Gavana wa BOT......why all these greediness?

Billioni moja nyumba ya Gavana wa Banki Kuu, wadogo zetu wanasoma kwa kudra, mvua ikinyesha shule inafungwa. Kweli jamani tutafika?


Kama tunaweza kutumia Billioni moja kujenga nyumba ya gavana wakati magavana wa baadaye ndo hawa wanasoma kwenye darasa kama hili, nini hatima ya nchi yetu. tunaipeleka wapi nchi yetu jamani. Nawaomba mniambie kama gavana angeishi kwenye apt halafu tukajenga hii shule hata kwa makuti, Mungu si angetuongezea hata mibaraka jamani.

Picha na habari nzima nimeizipata hapa. baada ya kuziangalia roho imeniuma sana na nikaona si vibaya nikiziweka hapa Maisha na Mafanikio hata kama tumesiona lakini kurudia kuziona kunaleta mafundisho zaidi.

9 comments:

  1. lazima iwe hivo kwa kuwa baadhi ya pesa zetu zinatunzwa huko kwenye nyumba yake :-(

    ReplyDelete
  2. Mhhhh, hii ni nyumba ya mtu, nilifikiri zinga la ofisi ya wadhungu...mhhhh, naiota kama nyumba yangu ya peponi...mmmh, thamani yake shillingi ngapi vile, siunaweza ukaandika masifusifuri yakajaa chumba cha jibu!
    Kasheshe kweellli

    ReplyDelete
  3. mimi nakubaliana na bwana Chacha kuwa nyumba hiyo lazima iwe imara sababu pesa zinatunzwa hukooo!! aaw hell no!

    ReplyDelete
  4. mambo yakiwa hivi, kuwa wengine wanaishi peponi wangali duniani na wengine wanaishi jehanamu wangali duniani ndio 'amani na utulivu' wenyewe huo.

    ReplyDelete
  5. Kwa sasa hali ya watanzania,itazidi kuwa mbaya zaidi,nikinukuu maneno ya Mwl.Nyerere pale Dodoma mwaka 1995,alitutahadharisha juu ya Kiongozi anayefaa kuiongoza Tanzania,matokeo yake sasa ndio haya,tunayoyaona.Watanzania hatukuufanyia kazi ushauri wake.Tanzania ndani ya miaka mitano tumekwisha kabisa

    ReplyDelete
  6. Hivi kuna ambaye anajali? viongozi wote sasa hari mpya awamu mpya!! wamewekeza katika uchaguzi na sasa ni wakati wa kurudisha pesa zao walizotumia kuwahonga wananchi!!

    ReplyDelete
  7. hizi ndio nchi za Afrika, viongozi wanajijali wao tu, hivi huko ni wapi? hakuna mbunge? utakuta na safari hii pia kagombea na kushinda uchaguzi wakati wanafunzi wanasomea kwenye vibanda jimbono mwake

    ReplyDelete
  8. Lakini wote tuko hivo tu hakuna wa kulaumu kwa kuwa sisi kama sisi tumefanya nini kwa hawa vulnarable class na huku tukiwa na uwezo? Tuache mtima nyongo jamani! Ila umefanya vizuri kutolea mfano kigoma ila kwa sasa Kigoma Kama Dubai.

    ReplyDelete