Wednesday, November 10, 2010

Brrrrrrr! Msimu wa baridi umeanza/theluji imeanza kuanguka tangu jana jioni na inaendelea!!!

Sasa kimeanza kipindi kile cha baridi theruji imeanza kuanguka tangu jana jioni hapa ni leo asubuhi saa moja na nusu hivi. Yaani hapa kaazi kwelikweli natamani ningekuwa napigiwa na jua....
Na hapa babu Erik anajiandaa kwa kwenda shule na baiskeli yake. Ni saa mbili kasorobo asubuhi hii.

Hapa saa tatu asubuhi. Mmmm baridi we acha tu.


Na hapa mzee wa nyumba naye anaaga ni saa tatu na nusu kuelekea anakowajibika.



13 comments:

  1. Oh, poleni sana, kama ingewezekana kipindi kam hiki ndio ungekuwa ukichukua likizo, unakuja kwenu bongo, manake huku ni kinyume chake joto mtindo mmoja!

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana. Hiki ni kipindi kizuri sana cha mwaka, hakuna bakteria na hewa ni safi kabisa, mwili hauchoki wala kuzeeka haraka katika baridi..! Hongereni sana kwa kweli ni kipindi cha uzima.

    ReplyDelete
  3. Ahsante Mtani!

    MMM!Ni kweli tungeweza kuchukua likizo msimu huu, ila huwa tunafanya tofauti na mwaka huu ni dhamu ya kuwa hapa. Ila umenitamanisha hilo joto hilo:-)

    Mija wewe! mwenzako naungua na baridi wewe unasema hivyo:-( Lol ni kweli usemavyo lakini we minguo tunayovaa na mwisho unaonekana kama tembo vile Maisha haya kaazi kwelikweli....

    ReplyDelete
  4. poleni sana duuh inaonekana ni baridi kali sana,,lakini bongo ndugu yangu huku ni joto kwa kwenda mbele

    ReplyDelete
  5. Poleni sana Bongo ikija baridi na barafu kama hio tutakufa huku tumesimama kwa kuganda na theluji.

    ReplyDelete
  6. ni kipindi kizuri kama hulazimiki kutoka nyumbani

    ReplyDelete
  7. ni kipindi kizuri kama hulazimiki kutoka nyumbani

    ReplyDelete
  8. Uzuri wake baridi unaizowea,nakumbuka mimi miaka miwili ya mwanzo kipindi kama hiki cha baridi,nilikuwa napata tabu sana nilikuwa nawashwa mwili mzima,lakini wee ukae ndani huku siutakaa karibu mwaka mzima? unapigana nayo kikumbo mpaka mwili wenyewe unazowea du!hongereni sana napenda sana snow.

    ReplyDelete
  9. Ah we acha tu! Huku Baltimore mambo ndiyo yanazidi kupamba moto. Haijashuka bado ila baridi ni kali ya kuunguza!! Bila kujijaladia basi ukitoka huko nje makamasi yaweza ganda!!

    ReplyDelete
  10. Duh!! sisi huku ni msimu wa joto kali

    ReplyDelete
  11. Ni kipindi muafaka sana cha kukaa pamoja na kuangalia uwezekano wa kuongeza famili, maana sio rahisi kucheza mbali na mwenzako!

    ReplyDelete