Monday, October 4, 2010
KITAMBI/UNENE: Ni dalili ya afya au ugonjwa?
Katika baadhi ya jamii zetu nyingi hasa kutoka bara la Afrika, kumejengeka dhana kuwa kitambi /unene huashiria utajiri. Mila, imani na desturi hii kwa kiasi fulani huchangia watu kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora, pengine hii inatokana na mwamko mdogo wa elimu ya afya jamii.
Wakati hali ikiwa hivyo miongoni mwa watu toka bara letu la Afrika, kwa upande wa nchi zilizoendelea, watu huamini kuwa unene/kitambi ni dalili tosha ya ugonjwa. Siyo hivyo tu bali pia historia ya magonjwa katika fani ya elimu afya jamii inatueleza hivyo.
Kuna unene wa aina kuu mbili, kwanza ni ule unaosababishwa na kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora / balance diet. Kwa mfano ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta na wanga, unywaji wa mara kwa mara wa pombe kama vile bia pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo. Aina ya pili ya unene ni ule unaotokana na urithi japo kwenye mada hii msisitizo zaidi ni kwenye aina ya kwanza ya unene.
Kuna matatizo mbali mbali yanayo ambatana na unene/kitambi. Mosi, madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari aina ya pili /diabetes type II. Pili, madhara ya kisaikolojia, hasa pale mtu anapojishuku kupoteza mvuto/ aesthetic beauty. Hali imeshamiri sana hasa katika nchi zilizoendelea ambapo watu huchukulia unene/kitambi kama ulemavu fulani wa kimwili.
Pamoja na hayo, nadhani wakati mwingine tunafanya makosa kuwahukumu binadamu kulingana na mwonekano wa maumbile yao, kwani hakuna hata moja kati yetu anaweza kuingilia kazi ya uumbaji, ninasema hivi kwasababu hatuwezi kujua ni nini chanzo hasa ambacho kinapelekea mtu kuwa mnene au kuwa na kitambi. Kama nilivyosema awali, kuna aina ya unene/kitambi kinachotokana au kusababishwa na urithi.
Namna ya kukabiliana na matatizo yatokanayo na unene/kitambi, wakati watu katika mataifa yanayoendelea, hujikita zaidi kwenye matumizi ya magari hasa magari binafsi, kidogo hali ni tofauti katika nchi zilizoendelea ambapo msisizito kwao ni kwenaye matumizi ya usafiri wa umma, matumizi ya baiskeli na hata matembezi ya miguu kwa sehemu zinazofikika. Kwa hili wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa vya kutosha kwa kuwekeza na kutenganisha barabara za magari na zile za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu.
Mwisho, njia pekee ya kukabiliana na changamoto hii ya unene/kitambi, ni kwa kuzingitia kanuni za lishe bora kwa
Habari hii nimeipata hapa.
Kitambi sio sifa , utajiri au afya, ni `ugonjwa' au `mlundikano wa mafuta mengi.
ReplyDeleteHili ni tatizo, lakini kwa vile watu wanpenda kuiga, au kuondoa huo udhaifu basi limehalalishwa kuwa kitambi ni sifa ya utajiri!
Nenda kwa madakitari watakufafanulia vizuri kuwa huo ni ugonjwa unaotokana na nini?
Kitambi ya baba, sio shibe ya familia.Hahahahahaha!
ReplyDeleteNina swali. Wapo wasemao kuwa kuna baadhi ya watu hupata vitambi baada ya kuridhika kimaisha,si kwa utajiri, just kwa kuipokea hali halisi ya maisha. Je, hili lina ukweli wowote.
kitambi naona kama kinaninyemelea na kamwe sikuamini kuwa vegeterian anaweza kuwa na kajikitambiz
ReplyDeleteKamala ndo hivyo ukishakuwa na mke basi unapata kitambi. Ndo hapo inapoonyesha ya kwamba umelizika na maisha. Ila angalia kisiwe kikubwa sana kina madhara yake.---lol
ReplyDelete