Wapo watu ambao nyoyo zao ni kama lulu au almasi inayongáa kwa usafi, hazibebi chuki, choyo wala kejeli, bali hubeba mapenzi, imani na ukarimu. Hakika hata wewe unayesoma hapa ni mmojawapo. NAWAPENDA NYOTE. . NA NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA KUMI IWE NJEMA. NA PIA, NI JUMAPILI MUHIMU SANA KWA NCHI YETU YA TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA PIA WATU WAKE ILI UCHAGUZI UWE SALAMA!!!!
Asante sana Dada Yasinta, kwa ujumbe mzuri wa kufurahisha. Nawe pia na familia yako ninawatakieni Jumapili njema sana na yenye Amani tele. Pia ujumbe kwa Watanzania wenzangu wote, tudumishe Amani na upendo daima, hasa katika siku ya leo ya uchaguzi. Uchaguzi mwema sana.
ReplyDeleteChibi.
Ahsante kwa maneno yaliyojaa busara tele. Mimi na familia tunakutakia furaha na baraka tele wewe na familia. Mkae salama..
ReplyDeleteUjumbe ni bomba na pia mdada unawakawaka kweli.
ReplyDeleteMlongo umependeza sana ligwanda likupendizi kweli kweli. Asante kwa baraka za jumapili, Ni kweli ni siku muhimu kwa nnchi yetu siku ya leo, tunawaombe mungu uchaguzi upite salama. Jumapili njema kwako na familie yako.
ReplyDeleteBombi umetoka bombi kweli kweli,asante sana kwa ujumbe mzuri wa j'pili na wewe pia.
ReplyDeleteJamani umependeza!!!!!!
ReplyDeleteWanasema kwa mwanamke ni `muonekano' kwa mwanaume ni `mtizamo'.
ReplyDeleteHeri ya Jumapili hii ilitakiwa kwa kila mtu na kila anapoingia ndani ya chumba cha uchaguzi aombe kuwa anayemchagua awe mwema. Lakini sikumbuki kuwa tulifanya hivyo. Kama tulifanya hivyo natumai mema. Kwani ukipanda mbigili utaraji mbigili, na ukipanda maharage utapata maharage!
Naamini wote mmekuwa na jumapili njema na familia, ndugu pia marafiki kwani hii ni siku ambayo tunaweza kukutana wote na kubadilisha mawili matatu. Binafsi nilikuwa na familia yangu na tulifanya yale tusiyoyafanya na ukizingatia nilikuwa off..lol.jumapili njema nanyi pia. UPENDO DAIMA.
ReplyDeletelakini dada yangu hapa ulipendeza sana kwakweli nimependa vazi lako mpaka wewe mwenyewe.
ReplyDelete