Wednesday, October 27, 2010

Chai inapunguza mshtuko wa moyo!!!

Unajua kuwa kunywa chai vikombe vitatu kwa siku au zaidi kunapunguza mshtuko wa moyo kwa asilimia 21. Haya jamani tunywa chai!!!!

10 comments:

  1. Ahsante dada kwa zawadi hii, inaonyesha jinsi gani unavyotujali! Unaonyesha pia unavyoijali taaluma yako kwa ajili yetu!

    ReplyDelete
  2. Asante kwa taarifa hii. Na mimi ninavyopenda chai...sasa ndo itanitambuwa kweli kweli!!!!

    ReplyDelete
  3. emu3! Ahsante sana lakini ni muhimu kupeana lile ulijualo kwani si vizuri kunyimana elimu.

    Kaka Baraka! unasema wewe ni mpenzi wa chai Ningependa siku moja tufanye mashindano na tuone nani mshindi. Maana mimi nisipopate chai siku nzima napelekwa hospital kulazwa.....

    ReplyDelete
  4. Ni chai ipi? Yenye maziwa na sukari kibao au ni ipe upendayo wewe na Mjengwa (ya rangi na bila sukari?) Ni hii wanayoita Green Tea au ipi?

    Nauliza maswali haya kwa sababu wanasayansi weshanichosha na habari zao hizi kanganyifu. Leo watasema kahawa inapunguza blood pressure, na kesho tena watasema kahawa inasababisha magonjwa ya moyo. Ukanganyifu unazidi pale kunapokuwa na migongano ya aina hii na halafu hawasemi tufanye nini. Kwa hapa Marekani ukisikiliza tafiti mbalimbali zinazochapishwa na wanasayansi hawa wallahi unaweza usile cho chote. Eti bia zinaleta matatizo kibao ya kiafya, na wakati huo huo tena watu wanaokunywa bia ndiyo huishi maisha marefu - ali mradi vurugu tupu.

    Msimamo wangu: nilishaacha kuwasikiliza hawa watu. Ninachofanya ni kutumia kile kitu ambacho nakipenda kwa muda kidogo na halafu nabadilisha tena. Kwani maisha ni nini hata mtu usile nyama ya mkia wa ng'ombe uipendayo eti tu kwa sababu wanasayansi wamesema nyama (nyekundu) ni mbaya?

    Exercise, eat well and die anyway...

    Samahani Da Yasinta kwani naona nimebwabwaja sana. Hili ni suala linalonikera na nilishaanza hata kuandika makala halafu sijui ikafilia wapi. Nitajitahidi kuimalizia makala hiyo yenye mifano kibao ya tafiti hizi kanganyifu!

    ReplyDelete
  5. Big Up Matondo, kabla sijatoa dukuduku langu nikakuta ujumbe wako.
    Nilikuwa mstari wa mbele katika kupinga hizi tafiti, kwani hazina mantiki kwa watu wote, utafiti unaofanywa Maryland au South Carolina, unahusisha watu wenye asili ya uzungu, ambao vinasaba vyao vina kasoro zinazowafanya wawe kwenye nafasi kubwa ya kupata magonjwa hayo, hakuna anayeenda kufanya utafiti umasaini, kwa watindiga, mbilikimo wa kongo au mabedui wa jangwani. Wakija na ka kitu, basi wanaloloma. Majuzi nilipokuwa NY niliona wenyeji wangu wameng'ang'ania kufakamia samaki wabichi (sushi), majani mabichi(salad), sukari bandia, diet coke na magome ya miti at inasaidia kupunguza magonjwa ya moyo. Lakini cookies, vyakula vingine sukari na mafuta kibao. Sasa ukila dagaa wa kigoma wabichi na minyoo ile iliyojaa, ha ha haa. Kusema ukweli mimi ninakula vyakula nilivyovizoea kwa nafasi yangu nikiangalia afya yangu. Kwani genetically nipo tofauti na wale waliofanyiwa utafiti. Hujagundua kuwa watu wengi wa asili fulani wenye umri sawa na wewe wanaonekana wazee sana kuliko wewe! Samahani kwa wale watakaonitizama kivingine

    ReplyDelete
  6. Chib: umegonga penyewe hasa!

    Hizi tafiti si za kukurupukia hivi hivi. Nimependa uchambuzi wako unaohusisha vinasaba. Wanasayansi ndiyo kwanza wameanza kuelewa mchango wa vinasaba na mazingira katika kuleta magonjwa n.k. Bado wanashangazwa kwa mfano ni kwa nini watu wengine wanavuta sigara na bado wanaishi zaidi ya miaka 100 na wengine wakigusa tu sigara wanapata kansa ya mapafu na kufa mapema sana. Ndiyo maana Mmasai anaweza kula kisusio chake (mchanganyiko wa maziwa na damu ya ng'ombe) na bado akawa salama bila matatizo. Chakula kama hiki mzungu nadhani hata kukisikia hataki kwani ni chakula cha "hatari" sana!

    Uliyoyaona huko NY ndiyo yale yale. Unashindilia samaki wabichi (sushi) bila kwanza kuuliza hao samaki wametoka wapi, na wamekuzwa katika mazingira gani. Ukiambiwa kwamba wametoka katika mabwawa ya China na wana kiwango kikubwa cha madini hatari ya Mercury yenye kusababisha matatizo makubwa ya kiafya basi unashangaa. Eti tu umesikia wanasayansi wamesema kwamba samaki wabichi wana faida za kiafya basi unaanza kuwafakamia. Upuuzi mtupu!

    Nitakula ninachopenda na kuangalia afya yangu bila kujali tatifi hizi kengeufu za wanasayansi. Mpaka siku mtu atakapokwenda kufanya utafiti Usukumani na kuonyesha kwamba chai ina faida basi pengine ndiyo nitabadilisha mawazo!

    By the way, mambo ya mshituko wa moyo yanatoka wapi kwa watu wanaoshinda shambani wakilima na kula vyakula vilivyokuzwa kwa njia za kiasili????

    ReplyDelete
  7. Hi Matondo, kwenye makongamano yetu tumekuwa tunawabishia sana hawa watu wanapokuja na data zao za kwao, na kuleta makadirio kwa Afrika, na kusema, tatizo hili kwa Afrika linakadiliwa kuwa....., yaani is estimated ....
    Tunawauliza swali, huo utafiti mliufanya sehemu gani Afrika. Siku hizi wameanza kubadilika, na hawaleti hizooo. Imechangia kwa kiasi kikubwa kuondoa ujumla, ndio maana kwenye mambo ya uzito-body mass index, siku hizi wanasema wanaangalia tumbo zaidi kuliko hips na manini yale ya nyuma, kwani tafiti zao zimegundua mapaja makubwa na mat... hayana uhusiano hata kama yanaongeza uzito kwa sana. Njoo Rwanda au nenda kwa Wanyankole Uganda. Cholesterol level iko kawaida despite nanihiii nyingi tu na uzito wa kupindukia.
    Lakini... Nawashauri, chungeni afya zenu. Msijipe sana mioyo na kusahau kula kadri ya mwili wako unavyokuruhusu

    ReplyDelete
  8. ha ha ha haaaaa! kaazi kweli kweli!

    @Chib & MMN-watafiti wa kwetu wako wapi ama ndo twafanya utafiti kuridhisha wanaotupa njulugu?

    ReplyDelete