Thursday, October 14, 2010

Tumepatwa na ugeni kutoka Tanzania Ni vijana waliokuja kwenye Ziara ya Mafunzo hapa Sweden!!

Wanapata chai na Kahawa kidogo
Chai na kahawa inaendelea!!

Ni jambo la kufurahisha sana kufikiwa na ugeni huu. Wote tulifurahi sana ingawa ilikuwa dakika chache tu. Na watakuwa hapa Sweden kwa muda wa miezi mitatu hivi.!!!!

8 comments:

  1. Karibuni wageni, Yasinta hukupiga nao picha?

    ReplyDelete
  2. Yasinta swali la kizushi,Hao wageni wametoka mbombi mbili kule kwa mfaranyati au? kama wametoka huko sikupataii picha utakavyokuwa unabonga kibombi nyumbi hahaaa.Anyway karibu sana wageni wetu.

    ReplyDelete
  3. Mija! unajua sikuwepo nyumbani si unajua majukumu /pilikapilika kila kukicha na halafu walikuja ghafla.

    Edna! Bahati mbaya hawakutoka Bombi mbili ndugu yangu lakini wageni wa nyumbani ni Raha ilioje kuwapata. Nami nasema KARIBUNI SANA.

    ReplyDelete
  4. Hapo lazima ujihisi upo nyumbani kwa muda, hongera kwa kupata wageni

    ReplyDelete
  5. Pole kwa kutokutana na wageni wa kutoka kunyumba Yasinta!Na uliposema walikuja ghafla nikastukia kweli wewe umekaa ughaibuni muda mrefu kwa kuwa Bongo ni kawaida pia wageni wakitokea wanapotokea na haiitwi ghafla na ndio maana Jogoo wa X-mass anaweza kuwa hayati kabla ya desemba Bongo.:-(


    Karibuni Wageni!

    ReplyDelete
  6. ni raha sana kupata wageni kutoka nyumbani ukiwa ughaibuni.
    naona Africafe kwa mbali pale.

    ReplyDelete
  7. Shukrani sana kwa taarifa hii. Nami nimefurahi kuona hiki kikopo cha Africafe. Wageni wanaonekana wamefurahi kukutembelea mwenzao wa nyumbani kabisa, yaani bomb' hii nyumb' hii :-)

    Taarifa ya safari ya wageni hao niliiona jana kule kwa Mjengwa. Soma hapa.

    Shukrani, na kila la heri.

    ReplyDelete
  8. Hongera kwa ugeni,na pole kwa kutokutana nao,nazani ulisononeka sana uliposikia walikuja na wameondoka hukuwepo.

    Bado wapo huko kwahiyo nikupanga tu siku ukiwa na nafasi unaweza kuwatembelea au kuwakaribisha tena,nyumbani kwako.

    ReplyDelete