Mwanamke mmoja alitoa kioja baada ya kudai talaka kinguvu huku jamii iliyomzunguka ikimshangaa kwa kilichosemekana kuwa amepata mwanaume mwenye fedha.
Mwanamke huyo, alipokuja kwa wifi yake,kumueleza akamwambie kaka yake ampe talaka kwa kuwa alichoshwa na tabia zake,na kumuamuru akiwa hajampa talaka hiyo ataondoka hata kama hajapewa talaka.
“Mimi namuomba talaka kaka yako hataki kunipa ana maana gani? mimi simuhitaji tena nimechoshwa na dhiki mimi, anipe karatasi langu niondoke nyumbani kwake” na asiponipa naenda bakwata lazima aitoe” alifoka dada huyo kwa sauti bila hata aibu
Wifi huyo alijaribu kumuuliza alikosewa nini na kaka yake huyo, na swali hilo hakutaka kulijibu na kumueleza kuwa yeye anachohitaji ni talaka hahitaji maswali,
Hata hivyo mwanamke huyo ilifahamika na ndugu zake kuwa,alikuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwingine ambaye alimuona atambadilisha kimaisha kwa kuwa ndugu zake hao alidai mwanaume huyo alikuwa na fedha zaidi ya mume wake wa sasa. Habari hii nimeipata Simon wa samvande

jamani kweli kunavisa huku duniani. Watu wanakuwa wanawathamini wenye hela na kuwatenga maskini, sasa huyo dada kama kweli alimuacha mume wake kwenda kwa mwenye fedha basi hapo hamna mapenzi ya dhati. Atakachokifwata ni hela za jamaa tuu. Kweli binadamu tuko tofauti dah.
ReplyDeleteYasinta,dada yangu,Hii uliyo leta leo nikali.Lakini kwa uzoefu wangu,kama ningekuwa ni mimi mkewangu anadai talaka,kwa sababu hiyo aliyo toa huyo dada, ningempa.Kwa nini nasema hivyo,sabaubu kubwa ni moja,hanitaki,hivyo kumzuia akae haita saidia, itakuwa nalazimisha penzi amabalo kwa mwenzangu halipo.kueepusha shali nibora aende.
ReplyDeletenihayo tu,kaka s.
yaani siku hizi ni mapenzi ya pesa kwa kwenda mbele.
ReplyDeleteMbona hakuna jipya hapa?. Pengine huyu dada ni "gold digger" tu na sasa amegundua kwamba alifanya kosa kwa kuolewa na masikini. Wanawake (na wanaume) wa aina hii wamekuwepo tangu zama za kale.
ReplyDeleteKwingineko: Pesa ndiyo mtawala kwa sasa. Zile falsafa za Mwalimu Nyerere za utu, upendo, umoja na mengineyo zimeshakufa.
Pengine badala ya kumlaumu huyu dada, tuangalie jamii nzima inaelekea wapi. Wakati ambapo watu wanaotuhumiwa kuiba mabilioni ya pesa za umma wanaonwa kama mashujaa (mbunge wangu Chenge alipokelewa kwa mapokezi ya kufa mtu aliporudi nyumbani baada ya ile kasheshe yake ya vijisenti), kuna ubaya gani binti huyu naye akikata njia ya mkato ili kufikia ndoto zake?
Hili ni tatizo la jamii nzima; na matabaka mawili kinzani (matajiri sana wachache kwa upande mmoja na masikini sana wengi kwa upande mwingine) ni ushahidi tosha kwamba maisha yemezidi kuwa magumu kwa walio wengi. Na tutasikia njia za kila aina za masikini kuweza kujikomboa ikiwemo ya huyu dada. Tatizo ni kwamba sina uhakika kama hii ndiyo njia sahihi! Vipi kuhusu masikini wengine? Wao wafanyeje? Tuendelee kuchekecha!!!
Pesa sabuni ya roho imemponza hata nani vile???
ReplyDeleteLakini wahenga walisema, mpende akupendae, asiyekupenda achana naye. Sasa huyo kadhihirisha kuwa hampendi jamaa, anapenda `mali'...na huko anakokwenda jamaa akifirisika naye anapigwa buti...lakini mwisho wa siku ua litanyauka!
Naxy! karibu tena hapa maisha na mafanikio! nakubaliana nawe apendae pesa basi hapa hakuna penzi kabisa.
ReplyDeleteUsiye na jina! umenena la maana kwa nini kumzuia au kumnyima talaka mtu asiyekupenda. kwani akibaki haitakuwa amani kabisa na wala penzi.
Adela.D.K!! Yaani kaazi kwelikweli mapenzi yananunuliwa. sijui tutafika wapi?
Kaka Masangu! itabidi tumfuate Dr. Remmy mke mbaya aolewe na mume mbaya na mume mzuri na mke mzuri. Lakini Hata hivi pendo liko wapi???
Tutachekecha na jibu sijui kama tutalipata.
emu-three! kaazi kwelikweli na masiha ni safari ndefuuuu.
Kazi kweli kweli!!!!!ni kweli sikuhizi watu wanapenda mteleko .
ReplyDeleteDada Maisha na mafanikio na mimi nitafutie mzungu basi nimecho na wanaume wa bongo utulivu ziro
DB
Mapenzi ya siku hizi ni ya pesa na ndicho kinachowaponza dada zetu kwani wanadhalilishwa kisa pesa
ReplyDeleteNatafuta mchumba rangi yoyote mwenye mapenzi ya dhati mimi naitwa steve namba yangu ni 0762165898 nitamjali na kumtunza tuma meseji kama uko tayari tufahamiane kabla ya yote kwa sababu kufamiana ni vizuri zaidi kabla ya kuingia kwenye uhusiano
ReplyDelete