Thursday, September 2, 2010

Tunaomba msaada wenu:- Ni vipi mchezo huu wa Bao/nchua uunachezwa?


Bao/nchua!!
Wakati nipo likizo na mpaka sasa kuna mvua kila siku na hata kunasababisha mafuliko sehemu fulani fulani. Sasa mimi na familia yangu baada ya kuona hatuwezi kufanya michezo mingine ya kuwafurahisha watoto tukakumbuka tuna bao/nchua ambayo tuliinunua Tanzania. Tukachukua kila tukijaribu kucheza ubongo haukumbuki kanuni inakuwa vipi. Nikaona mmmhhh! kuuliza si ujinga aulizaye anataka kujua na umoja ni uwingi. Kwa hiyo nimeona niwaulize je ni vipi kanuni inakuwa? Tutashukuru sana kama mkitusaidia.

6 comments:

  1. Hapa nadhani watu watashindwa hata kuelezea, na kwakuwa mie zee la nyeti za nyasa linajua huu muchezo a.k.a mchezo basi ngoja ninyamaze kwanza niwaone waungwana wanavyojuvika. ila unanoga kwelikweli

    ReplyDelete
  2. Bao linachezwa karibu sawa, lakini kila kabila lina ka-mtindo tofauti kidogo. Bao lililonoga ni lile la kizaramo.
    Mie mchezo huo, .... labda niende shule kwanza

    ReplyDelete
  3. Unaokota katika tondo mojawapo la kwako, unazigawa moja moja kila tundu kufuata msitari(upande wako), tembe ya mwisho itakayoishia kama kuna tembe kwako na kwa mwenzako, unakuwa umzila zile za mwenzako, unazichukua na kuziongezea na zile zako na zile zilizokuwa kwenye tundu uliloishia unaednelea kuzigawa, hivyohivyo, kushindwa kwako ni pale tembe ya mwisho itakapoangukia kwenye tundu lako, likiwa halina kitu!
    Nilicheza hivyo nikiwa mtoto, sasa siui ndio hivyo kwenye mabao ya wakubwa!

    ReplyDelete
  4. Mmmmh na mimi nasubiri kujifunza hapa.

    ReplyDelete
  5. unapanga katika kila kishimo soro mbili, alafu wakwanza kucheza anatakiwa aokote soro mbili katika kishimo kimoja kilicho upande wake na kuzunguka nazo kutoka kulia kwenda kushoto. zitakapoishia kama kuna soro anazibeba na kuendelea hivyo hivyo, akiangukia kishimo ambacho akina soro kama kikiwa upande wa ndani au ule wa mbele na upande wa mwenzake kutakuwa na soro mbele na nyuma atakuwa amekula. kama kutakuwa kuna soro upande wa nyuma atakuwa amelala. na katika mzunguko wake kama atakuwa ameangukia upande wa nyuma na akuna soro kiko tupu atakuwa amelala. natumaini umenielewa.

    ReplyDelete
  6. kuhusu mchezo huu itabidi tijitahidi kusogea karibu na mababu ili tuweze
    kuhufahamu mchezo huu lakini tukiendelea kukuka kwenye facebook zitatupita

    ReplyDelete