Thursday, September 23, 2010

SHUKRANI KWA WOTE!!!


Kwa ajili yenu wote kutoka kwa Yasinta Ngonyani!!!

Wanablog wenzani leo napenda kutoa shukrani zangu nyingi sana na za dhat kwa UWEPO wenu na pia UPENDO wenu kwangu, kwa familia yangu na kwa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO.

Kwanza kabisa napenda kuwashukuruni kwa UWAZI wenu kwangu, hapa nina maanisha kwa kuniambia yale niliyokuwa nayajua kuhusu mimi na yale ambayo sikuyajua kuhusu mimi. Ni jambo la kujivunia sana pia kufurahisha kuona unaambiwa mambo kama haya kabla hujaiacha dunia hii. Kama tunavyojua wengi wameiacha dunia hii bila kuja wametenda nini hapa duniani na wao ni akina nani? Na siku ile ya safari ya mwisho ndo watu wanapotamka yale yote mazuri na mabaya. Na mimi naweza kusema nina bahati kwani nimebahatika kuyajua na pia wengine kunijua. AHSANTENI SANA.

Kwa kujikumbusha unaweza kusoma hapa kwa mdogo wangu wa hiari Koero Mkundi na hapa kwa Mzee wa lundunyasa Markus Mpangala, pia hapa kwa Diwani ya Fadhili kwa mtani wangu Fadhy Mtanga na halafu hapa.

Pia kwa wengine wengi walioniandika na ambao sijawataja hapa, nawashukuruni sana wote wote kwa ujumla kwa UPENDO wenu.

7 comments:

  1. Da Yasinta tunashukuru sana. Lakini yote tunayoyaandika juu yako unayastahili ingawa sisi twaandika kwa uchache mno maana tungehitaji kurasa alfu lela ulela kuandika wasifu wako ambazo hata hivyo zisingetosha.

    ReplyDelete
  2. Nalia ukiwa MBALI, nachukia nisipo KUONA, najua ninapo KUUDHI, naumia unapo NITENGA, nateseka ukiwa KIMYA, na nafurahi UKINIKUMBUKA.

    pia nikukumbushe igizo la Romeo na Juliet;

    My only LOVE sprung from my only hate! too early seen unknown and known too late.

    ReplyDelete
  3. Hata sisi ambao hatujakuelezea hisia zetu kwenye vijiwe vingine, lakini kimoyomoyo tunakupenda sana na kukujali, hiloo usitie shaka.
    Wewe umekuwa dada mpendwa mwenye kutujali, nakiri kuwa kila mmoja unajaribu kumpitia kwenye kiwanja cheke kuhakikisha kuwa hajambo, na unajitahidi angalkau kuzungumza neno , hii ni kuonyesha wazi kuwa unamjali na kumpenda kila mtu.
    Wakati mwingine unaweza ukaandika usione mtu aliyebisha hodi, lakini wewe lazima utakuwepo... Wengine wewe ndiye uliyetutoa na kuonekana, je mtu kama huyo asipokushukuru akauwa nani, kama sio mosa fadhila!
    Ahsante sana na endelea na moyo huo, kwani upendo wa dhati huonyeshwa kwa vitendo.
    Mungu akubariki wewe na familia yako!

    ReplyDelete
  4. Amini kabisa anayefanya mambo mazuri anastahili pongezi hata kama wewe utashindwa kutoa pongezi ila wapo watakao toa pongezi hizo nasema hongera na unapaswa kupongezwa

    ReplyDelete