Thursday, September 30, 2010

Picha ya wiki na ya mwisho kwa mwezi huu:- HAPA VIPI JAMANI????

Nimeipenda hii picha nimecheka kweli na nimeona iwe picha ya wiki na pia sikupenda kucheka peke yangu nimeona na wenzengu tucheke pamoja na tunenepe pamoja. Kaazi kweli kweli!!! Sijui huko tuendako itakuaje?

13 comments:

  1. huyu ni mbuzi wa kike na sijui kavaa nguo kuficha nini na atafichaje, si unajua kazi ya ngua ni kuficha kijulikanacha kipo na kimekaaje??

    ReplyDelete
  2. Kapendeza mwenyewe, sijui anaenda wapi?
    Yasinta umenisaidia kuumaliza mwezi huu kwa kuniumizia mbavu zangu. Duh!

    ReplyDelete
  3. Da Mija..ndiyo kapendeza lakini mie nasubiri kumuona akirembua na mawani yake hayo....lol!

    ReplyDelete
  4. Mhhh, mi naona kama wanawadhalilisha wanyama...lakini imekaa sawa, kwani kuna jamaa kasema hukoooo mbeleni, wanyama watavaa nguo na sie wanadamu tutakuwa kama wanyama, alisema hivyo alipomuaona binti mmoja kavaa nusu uchi na bwanawake suruali imeshuka nusu ya makalio...

    ReplyDelete
  5. Mambo ya kitchen party hayo meee!! kaalikwa kwenye kitchen party...kweli inachekesha sana nimeipenda hii.

    ReplyDelete
  6. watanzania hatuna tabiya za ajabu na mila za ajabu leo myama kavalishwa nguo kesho atatafutiya mwanaume wa kulala naye huo ndiyo mwazo wa kuiga ujinga za wazungu huwavisha wanyama nguo kisha huwatamadi na kuwaingiliya na kuwazalilisha kijinsiya nisawa na kuwavisha watoto wao nguo za ajabu kisha huwabaka na kuwanajisi yote hayo yamesababishwa kutokuwa na tamaduni mila na desturi kama tulivyo sisi waafrica

    ReplyDelete
  7. leo nimefurahi sana kuona picha hii ya mbuzi.sijui umepata wapi ? kweli tunakoelekea sijui maisha yatakuaje ?

    ReplyDelete
  8. Ni furaha kwa mimi kuona wasomaji wa maisha na mafanikio wanafurahi. Picha hii kwa kweli kuna mtu alinitumia ni msomaji wa maisha na mafanikio pia. Ombi Naweza kuyaweka maoni yako hapa kibarazani ili wengi wasome na kujifunza? ntafurahi mimi pia....

    ReplyDelete
  9. kweli nimekubali picha hii ni kali kweli dada yasinta mnajitahidi kuchekesha na
    kufundisha big up jpili poa kwa kiluga chetu tunaseme amoor

    ReplyDelete
  10. Hahaaa Yasinta una vituko wewe, akapendeza mwenyewe na tenge lake...Na hilo pochi mimi hoi.

    ReplyDelete
  11. Aisee amekuwa mrembo, watu wana akili za ajabu, hv huyu aliwaza nini na huyu mbuzi, kuna story ya mbuzi huko Mombasa (Kenya) inahusu Mbuzi mtu alizaliwa
    check YOU TO BE "si mbuzi si binadamu"

    ReplyDelete