Wednesday, September 15, 2010

NIMEUPENDA MSEMO HUU!!

"HAKUNA ANAYEJUA UPWEKE UNAOSABABISHWA NA YEYE KUTOKUWEPO MAHALI FULANI"

MTU AKIONDOKA MAHALA HUACHA UPWEKE, NA UPWEKE HUO HAUSIMULIKI. INA MAANA NI LAZIMA UWEPO ILI KUUHISI.
NA UPWEKE HAUWEZI KUWEPO KAMA WEWE UPO

INA MAANA:- NI LAZIMA WEWE USIWEPO ILI UPWEKE UWEPO NA HAKUNA NAMNA YA KUUSIMULIA UPWEKE, HIVYO NI LAZIMA UWEPO ILI KUUJUA
KWA HIYO, HAKUNA AJUAYE UPWEKE USABABISHWAO NA YEYE KUTOKUWA MAHALA FULANI KWANI NI LAZIMA ASIWEPO ILI UPWEKE UWEPO NA HAKUNA NAMNA YA KUUSIMULIA MPAKA UWEPO."
Hii ni nukuu nzuri sana na mimi napenda sana:- Ukitaka kujua nimeipata wapi basi sikiliza kwa kakangu Mubelwa.

7 comments:

  1. kumbe! ngoja na mie nione upweke wangu utanipelekapi... :-(

    ReplyDelete
  2. Naamini kuna tofauti ya KUWA PEKEE na kuwa MPWEKE.

    Naamini kilichonukuliwa hapa ni ``KUWA PEKEE´´ na sio UPWEKE.

    Naamini unaweza kuwa MPWEKE hata ukiwa umezungukwa na WATU ambao unadhani ndio tibabu la UPWEKE.

    NI mtazamo tu!

    ReplyDelete
  3. Ni ujumbe mzuri na pia naungana na KITURURU kwa tafsiri nzuri ya UPWEKE.

    ReplyDelete
  4. Huo msemo unaniachaga hoi yaani!!

    ReplyDelete
  5. NIMEUPENDA MSEMO HUU!!

    ReplyDelete
  6. Chacha kama unataka kufanya majaribi haya Karibu tu:-(

    Kaka Simon Upo sahihi kabisa.
    Edna:-)

    Upepo mwanana! ni safi kupata fikra hapa na pale.

    Penina! ni msemo tu kumbuka hata ukiwa na watu bado utajisikia upweke.

    George:-)

    ReplyDelete