Sunday, August 15, 2010

SWALI LA JUMAPILI YA LEO:- Msamaa ni nini?

Nisamehe



Je utaratibu sahihi wa kumsamehe /kusamehewa kwa mtu aliyekosa ni upi?

1. Mtu aombae msamaha kwanza/atubu ndipo asamehewe?

2. Asamehewe hata pasipo kuomnba msamaha au?

3. Vyote viwili ni sawa?



Jumapili njema wote na tuonane wakati mwingine!!!

12 comments:

  1. Jibu kwa KIFUPI:

    (3)



    Jibu kwa mwendo wa maringo:




    Hakuna utaratibu katika hili kwa kuwa kibinadamu inategemea tu na Limtu lenyewe lililo kukosea.

    Kikristo inashauriwa usamehe waliokukosea hata bila wao kukuomba msamaha. Na kwa kawaida kitu kikishauriwa na Yesu maana yake ni kawaida kwa watu kwenda kinyume na hilo.

    Kwangu mimi binafsi ni rahisi sana kusamehe TOTO ZURI lakike ambalo na udhaifu nalo, TOTO DOGO ambalo nahisi halijui litendalo kuliko njemba nikumbukalo lilikuwa linanionea wakati mdogo.:-(

    Nazungumza hivyo kwa uzoefu.

    Kuna TOTOZ moja ilikuwa inanisaidia kujisikia na girlfriend enzi hizo MOROGORO niliwahi mpaka kulifumania na Muarabu mmoja na mara ya pili Mhindi mmoja enzi hizo , na haki ya nani kesho yake YATUKIO nililisamehe kisa liniangaliavyo tu na kunililia kuwa halita rudia tena.[Ok kisiri nilihisi nisipolisamehe ni mimi ntakosa tamutamu kwa kuwa lilikuwa linajulia kweli kuneemesha utamu.:-(]

    Ila mpaka leo nimeathirika , nikisikia Msichana katoka Morogoro nahisi anahusudu Waarabu na Wahindi kuliko Watu weusi.:-(

    Kwa aijuaye Morogoro atakumbuka kuna kipindi wasichana warembo walikuwa zao sana Kujigonga kwa Waarabu na Wahindi.

    Samahani kwa KUPITILIZA katika KUJIBU.

    ReplyDelete
  2. kusamehee/kumsamehe mtu ni kitu muhimu sana kwa binadamu.hasa unapo msamehe bila yeye kujuwa,naanapo kuja kujuwa wewe unakuwa ukombali katika kutokuwa mtu wa visasi.pia kwa afya ni vizuri kusamehe.usibebe mzigo kwa maisha yako yote,kama kakukosea msamehe na wewe umemkosea mtu omba samahani .ni hayo tu wewe kasichana ka kingoni.nawewe nimekusamehe kutokana na ulivyo kazuri doo! kaka s.

    ReplyDelete
  3. Kabla ya kumsamehe mtu ni lazima ajue kosa lake, ingawa tunaambiwa kwenye vitabu tuwasamehe kwa maana hawajui watendalo

    ReplyDelete
  4. mmmh! A na B zote ni sawa.

    Kumbuka tu kusamehe kunakusaidia wewe zaidi ya anayesamehewa.

    Pamoja daima kama vodka....lol!

    ReplyDelete
  5. ila sasa, kwangu mimi hakuna kosa, wewe tenda utendalo, mimi nakupenda na kukuchukulia ulivyo, usiombe msamaha, hujanikosea, ila tenda utendalo tu

    ReplyDelete
  6. Kusamaheana ni wajibu kwa kila binadamu, na ili kusamehe kuwepo lazima kuwe na kukoseana. Kama binadamu hatuwezi tukaakmilika, ninachokiwaza mimi sio lazima kiwe sawa na mwenzangu, na kwahiyo kunatokea kusigishana! Kusigishana kukiendelea kunaleta chuki ambayo mataokeo yake ni kukosana, sasa utajiuliza kwanini tukoseane, ina maana mimi sijawaho kumkosea mwenzangu, ukifikia hatua hiyo unaona kuwa kuna umuhimu wa kusameheana. Kwasababu leo kakukosea mwenzako vile, kesho wewe unaweza ukamkosea mwenzako hivi, mukiwa mumejenga tabia ya kusameheana, basi kunakuwa hakuna matatizo.
    Je utamsamehe vipi mwenzako? Kama mumejenga tabia ya kusameheana, jibu lipo wazi, kwanza inabidi ukiri moyoni kuwa `ingawae kanikosea, yeye ni binadamu kama mimi, basi namsamehe, kwani jana au juzi nilimkosea yeye akanisamehe!

    ReplyDelete
  7. hellow,

    mtu yampasa aombe kwanza msamaha kisha atubu, akitubu bila kuomba msamaha sidhani kama mungu atapokea, kwani yule aliyemkosea bado atakuwa anauzunika.

    siku njema wa kunyumba.

    ReplyDelete
  8. Kuomba msamaha kuko ndani ya moyo wa mtu, sio rahisi mtu mwingine ajue vile unamaanisha, unaweza jinyenyekeza mbele za watu kuonyesha kuomba msamaha lkn kumbe rohoni ni tofauti kabisa, mimi nadhani katika siri zilizofichika hii ni mojawapo, ndio maana unajikuta leo unaomba msamaha na kesho unarudia kosa lile lile.

    ReplyDelete
  9. kuomba msamaha ni kuanza kujutia kosa
    ulilolifanya kwa yule uliye mfanyia
    kabla ya kumtamkia kwamba naomba unisamehe

    ReplyDelete
  10. kuomba msamaha ni kuanza kujutia kosa
    ulilolifanya kwa yule uliye mfanyia
    kabla ya kumtamkia kwamba naomba unisamehe

    ReplyDelete