Tuesday, July 6, 2010

ZAHANATI YA GOMELO KIJIJINI KISAKI

Huduma zetu za afya
Hapa ni "wodini" katika Wilaya ya Morogoro, Tarafa ya Bwikila Kata ya Kisaki kijijini Gomela. Kweli hapo mgonjwa atapona au atapata nafuu?- Kitanda cha ngozi ya ngómbe au mbuzi "teremke tukaze". Na uvunguni mwa kitanda tunaona besen/karai ni kama choo hapo. Ukiangalia dirishani ndio sehemu ya kutundukwa drip zaidi tembelea blog ya Fautine, mzee wa Changamoto na Lukwengule. Je huu kweli ni uungwana? Viongozi wetu wapo wapi???? Je?? mnasikia vilio vyetuuuuu???????

9 comments:

  1. Wale wanaokimbilia kura kwa ajili ya kula na kutoa ahadi za uongo kwa wananchi na matokeo yake kuwaacha katika hali ya namna hii, hakika huu ni uhalifu!! Je yu wapi huyo mkuu wa mkoa wa Morogoro? Mkuu wa Wilaya na wakuu wa afya?? Huu si uungwana hata kidogo... Je yale mashangingi yaliyowasili majuzi si yasingeagizwa na badala yake kushughulikia hali hii?? Na yale mapesa ya EPA yaliyorudishwa??

    ReplyDelete
  2. Nimewahi kuishi kijijini hapo. Ni kweli tupu

    ReplyDelete
  3. Ukiangalia hii picha,cha kwanza kimenigusa ni huruma kwa hawa wagonjwa,kilichofuatia ni hasira hivi hii kweli ni Tanzania yangu ninayoipenda kweli?huko vijijini viongozi wanayaona haya kweli?haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania kweli?

    Halafu uchaguzi unakuja wananchi hao hao,wanawachagua tena viongozi hao hao?ni bora ya kugomea uchaguzi kama mambo yenyewe ndio kama hivi? maisha bora kwa kila mtanzania ni ndoto za alinacha.

    ReplyDelete
  4. Wananchi wenyewe wamekaa kimya ndiyo maana hali hii inaendelea.

    Ndiyo yale Yasinta unayosema "Tumejifunga mno" hata kusema tunaogopa.

    ReplyDelete
  5. Dada.

    hizi picha hizi,what image do we send to others?Jamani kila nyumba inamatatizo yake lakini nyumba hiyo hujitahidi kutabasamu kwa majirani zake ili kutuza siri za ndani.

    Je nani wa kulaumiwa?

    Mpiga picha au msambaza picha?

    Hata ughaibuni they have this beds.

    ReplyDelete
  6. pole sana mama na wanakijiji wa hicho kijiji kwa ujumla wake, hali hii haipishani sana na kijijini kwetu pia, huduma za afya na elimu ni kama hizi hizi tu, pole sana wananchi wenzangu wa Tanzania. Tuna safari ndefu kuelekea ukombozi na uhuru, heshima, utu, amani na upendo wa kweli.
    ushauri wangu: Watanzania wenzangu, umefika wakati wa sisi sasa kuamka kutoka usingizini na kuanza kuijenga nchi kuanzia mawazo yetu mpaka uamuzi wa nani awe nani katika nchi hii.

    ReplyDelete
  7. Sipendi mara nyingi kujibu comments za watu wengine. Ila kuna mtu mmoja hapa juu anasema kwamba hatuna haja ya kuweka hii picha na anaashiria kulaumu mpiga picha au msambaza picha. Mimi nafikiri swala linarudi kwetu sisi wenyewe wa tanzania kwanga viongozi ambao wanaangalia sana matumbo yao kuliko nchi na pili uzaifu ambao sisi wenyewe wananchi tunao. Mimi ni mtu wa Iringa vijijini huko mbunge anagombea akinunua pombe tuu sisi wahehe tunaridhika kabisa tunasahau kwamba hatuna chochote zaidi ya ujimbi. Sisi sijui tukoje lakini ukweli ni watu ambao mambo mengine tujipa wenyewe.

    Watu wanaongombea ubunge sasa hivi tz ni wengi wote wanaona malupulupu yaliyopo ndiyo njia pekee yakuwa instant milionea. Lakini ukiangalia kwa undani watu wanaotaka ubunge wamefanyanini au wana vision gani hamna. Kwenye ngazi ya taifa napo ndiyo hivyo hivyo tuu slogan kilimo kwanza au ali mpya kasi mpya lakini nini maana yake hakuna.

    ReplyDelete
  8. Also that we would do without your excellent idea

    ReplyDelete