Thursday, July 15, 2010

KILIO CHA MAUAJI YA ALBINO!!!

Festo kaduma ni mlemavu wa ngozi (Albino) ambaye amelazimika kuishi kwa mganga wa kienyeji Dr Antony Mwandulami ili kuyanusuru maisha yake na waauwaji wa maalbino tukio ambali linaelezewa kwa majonzi makubwa wa wadau mbali mbali akiwemo Bibi Yasinta Ngonyani mtanzani anayeishi nchini Sweden mwandishi wa makala haya Bw Francis Godwin anaelezea zaidi."..Nimekaa na kufanya tafakari ya kina kuhusiana na mauaji ya ndugu zetu Albino yanayoendelea kuisakama Tanzania. Dhana mbili zinajitokeza katika tafakari hiyo.
Moja ni dhana nzima ya ubaguzi wa rangi na pili ni tathimini yangu kuhusu mikakati ya serikali ya Tanzania kuwahakikishia usalama ndugu zetu Albino"Ukiangalia ubaguzi wa rangi uliokuwepo Afrika Kusini enzi za Makaburu, watu walipangwa katika makundi kutokana na rangi zao; weupe ( Wazungu ), watu wa rangirangi (coloured ) na weusi ( Waafrika ). Huduma zote, ikiwa ni pamoja na elimu, zilitolewa kwa kuzingatia rangi ya mtu.
Kulikuwa na kumbi za starehe kwa ajili ya watu weupe, ambapo mtu mweusi hakuruhusiwa kuingia. Kuna sehemu zingine ambazo mwafrika hakuruhusiwa hata kukanyaga kabisa. Akikamatwa, alipewa kipigo kikali na hata kutupwa lupango ( jela).
Ubaguzi wa rangi, hususani dhidi ya Mwafrika, ulikuwepo hata katika nchi za Magharibi. Nakumbuka nimeona picha zilizoandika “only for blacks and dogs here.” Hii ilikuwa hatari sana, kwani mtu mweusi alinyimwa haki zake kutokana na rangi ya ngozi yake .
Sasa tujiulize.Hivi Albinno ni mtu wa namna gani? Anaweza tambuliwaje kwa muonekano wake? Sintopenda kuingia ndani zaidi kuchimba sababu za kibaiolojia zinazo mfanya mtu azaliwe Albino. Hata hivyo mtu haitaji microscope ( darubini) wala elimu ya Chuo kikuu kumtambua Albino.
Nionavyo mimi, naamini bila pingamizi lolote kuwa mauaji ya Albino yanayoendelea kuitikisa Tanzania “Kisiwa cha Amani” ni mwendelezo wa dhambi ya ubaguzi wa rangi, lakini huu ni ubaguzi mkali zaidi katika historia ya mwanadamu kushinda hata dhambi ya biashara ya utumwa.
Nasema nimkali zaidi kwani unalenga kuondoa maisha ya mwanadamu kwa ukatili wa kunyofoa viungo, tofauti na ule wa kumzuia mweusi kutembelea mitaa fulani au katika upandaji wa mabasi n.k !Ni kwa kuangalia rangi ya ngozi yake, unaweza kumtambua Albino.
Kwa bahati mbaya, Albino anayezaliwa Afrika, ni tofauti na yule wa nchi za Ulaya na Marekani, kwani Albino wa nchi hizo, hatofautiani sana na mtu wa kawaida. Rangi yake inarandana na ya mzungu . Si ajabu kama naye angefanana na mwafrika, angebaguliwa na kuuawa.
Kinachonishangaza mimi, ni kwanini Tanzania au Watanzania kwa ujumla hatusemi ukweli kuwa mauaji ya Albino yanayoendelea, ni ubaguzi wa rangi ili tuweze kupambana nao ipasavyo na Jumuiya ya Kimataifa iweze kutoa msaada sawawa na ambavyo jumuiya ya Kimataifa, hususani Tanzania, ilivyojitoa muhanga kung’oa mzizi wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini?Kwa mtazamo wangu, Watanzania tumeaminishwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na hivyo sisi ni bora zaidi kuliko Taifa lolote kiutamaduni na kimaadili.
Hii si kweli na huu ni mtazamo potofu ambao tusipokuwa makini, utatufikisha pabaya.Kwa uzoefu wangu, kitendo cha ubaguzi kikifanywa na Taifa jingine mfano Burundi, Kongo, Afrika Kusini, Ujerumani, M arekani ama Israeli, tunawanyooshea kidole kuwa wamepotoka huku tukitamka wazi kuwa nchi hizo zinafanya ubagauzi wa rangi.
Je, kwa nini kitendo hicho kikitendeka Tanzania kama cha mauaji ya Albino, tunapata kigugumizi kutamka wazi kwamba ni kitendo cha ubaguzi wa rangi na tunaanza kutafuta majina mengine kama vile “unyanyasaji wa Albino” na k.n yasiyotoa picha halisi ya mambo yanayoendelea?Kwani ubaguzi wa rangi lazima kitendo kifanywe na mtu mweupe ( mzungu ) dhidi ya mweusi ( mwafrika ) ili kistahili kuitwa ubaguzi wa rangi? Vipi kama kitendo hichohicho kitafanywa na mtu mweusi dhidi ya mtu mweupe ( mzungu / albino ), hakiwezi kuitwa kitendo cha ubaguzi wa rangi?Au kama mtu mweusi atafanya kitendo cha kumbagua mweusi mwenzake kutokana na rangi yake kama vile mweusi sana , mweusi tiii! mweusi wa kati, nacho hakiwezi kuitwa ubaguzi wa rangi? Na vipi kama mtu mweupe ( mzungu ) akimbagua na kumnyanyasa mweupe mwingine kama vile Mchina , Mwarabu n.k, kitendo hicho kitaitwaje?Kwa uzoefu wangu, hasa baada ya kuangalia matukio ya hivi karibuni ambapo Waafrika Kusini waliamua kuwavamia na kuwaua wahamiaji kutoka nchi nyingine za Afrika, Tanzania ilikuwa mstasri wa mbele kukemea vitendo hivyo.
Tanzania ilitoa tamko kali na kwa uwazi kabisa ikisema, “ Dhambi ya ubaguzi bado inaitafuna Afrika kusini.” Nikaanza kuangalia mambo mengine ninayoyashuhudia kila kukicha huku Marekani. Mtu akifanyiwa kitendo fulani, kwa mfano, ikiwa ni mweupe kakifanya, hukimbilia kusema ni ubaguzi wa rangi. Sasa mimi najiuliza.
Je endapo Mtanzania mweusi mmoja ataenda nchi yoyote ya Magharibi kama vile kusoma au kufanya kazi halafu akauliwa na kunyofolewa viungo kama wanavyofanyiwa Albino, Tanzania itasemaje? Haina ubishi , kila mtu atasema “amebaguliwa na kuuwawa kutokana na rangi yake.” Swali langu la msingi ni hili:
Kitendo cha Albino kunyofolewa viungo vyake kinyama na hatimaye kuuawa na mtu mwenye rangi nyeusi kisa rangi yake ni tofauti na cha mtanzania mweusi aliyebaguliwa na kuuawa ugenini hususani katika nchi za magharibi? Kwa nini mauwaji ya Albino yasitajwe kama ubaguzi wa rangi? Maana Albino naye hutambuliwa kwa rangi yake! Kama tumefikia hatua ya kuuana kutokana na rangi zetu; moja nyeusi, nyingine ya rangirangi ( coloured ) na wote ni binadamu tena watanzania, tuanaelekea wapi ndungu zangu?Serikali ya Tanzaia inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kupambana na janga hili la mauaji ya albino.
Uamuzi wa kugawa simu kwa albino wote, pengine waweza kusaidia kwa kuwawezesha kupiga simu polisi wanapovamiwa.Lakini Serikali inawasaidiaje albino waishio kijijini ambako hakuna umeme? Simu hiyo inachajiwa kwa teknolojia gani? Je simu hizo hizitakuwa kivutio kingine na hivyo kuwafanya wavamiwe zaidi?Kama imefikia hatua albino hawezi kutembea peke yake au kutembea baadhi ya masaa hususani jioni, kama imefikia hatua Mbunge maalum ambaye ni albino lazima apewe ulinzi maalum ili asinyofolewe viungo vyake, falsafa ya Tanzania kama kisiwa cha amani iko wapi?Ndugu zetu wa Marekani wanaelekea kuishinda dhambi ya ubaguzi wa rangi, kwani hatimaye wamefikia hatua ya kumchagua mtu mweusi kuwa Rais wao kwa kuangalia uwezo wake, hoja zake na si tena kigezo cha rangi kama Dr. Martin Luther King Jr aliposisitiza katika ndoto yake ( I HAVE A DREAM). Mwaka 2010 kama mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa albino, tutakuwa tayari kumpigia kura endapo atakuwa na sifa za kutuongoza? Tafakari, Chukua hatua.

Kwa upande wake Bw Kaduma anasemakuwa ameona ili kujiokoa na wauwaji hao kuishi kwa mganga huyo ambaye ndiye aliyemuokoa kuuwawa baada ya kuwekewa mtengo na mkazi mmoja wa Mbarali ambaye alitaka kumuua na kuuza viungo vyake kwa zaidi ya shilingi milioni 2.

Kaduma anasema kuwa yeye alikuwa hajua chochote juu ya mpango huu ila alishangaa kuona polisi ,magnga huyo na mtuhumiwa wakifika kijijini kwao na kudai kuwa wamekuja kumwokoa baada ya mtuhumiwa huyo kukili kutaka kufanya mauwaji.

Bw Kaduma ambaye kwa sasa amekuwa akiishi nyumbani kwa mganga huyo na kufanya kazi ndogo ndogo huku akitembea na kisu kama ngao ya kujilinda na wauwaji hao ameomba serikali kuwawajibisha waganga wanaochochea mauwaji hayo ya maalbino na kuwabakiza waganga kama Dr Mwandulami ambaye ameonyesha kuchukizwa na mauwaji hayo na kujikita katika kutetea uhai wa maalbino.

Usikose wiki ijayo kupata undani wa tukio hili na maisha ya albino huyo pamoja na mwanamke mwenye familia ya watoto wanne anayeishi kwa mganga huyo akikwepa kuuwawa kijiji kwao.

Makala hii ilishawahi kusomwa lakini nimeona si mbaya kama tukiirudia tena basi gonga hapa

7 comments:

  1. Kwishnei.............!

    Muda utakuwa shahidi tunapotoka katika kizazi cha mawe na kuelekea kizazi cha dhahabu ambacho hakina madudu kama haya :-(

    ReplyDelete
  2. MAAUWA ni nini? Ni Kingoni au Kiswahili?

    ReplyDelete
  3. Wakati mwingine unapoandika kitu kwa hamasa unaweza ukakosea `spelling' najua alimaanisha Mauaji.
    Ama kuhus hili tatizo nafikiri adui ujinga na umasikini bado ni balaa kwetu. Mtu akielimika na kujua kuwa hakuna kitu kama hicho kuwa miili ya mtu inaleta utajiri na utajiri huja kwa kuzalisha, na vitu kama hivyo , hatakuweza kuingia katika mtego wa waganga wa kienyeji ambao kula kwao kunategeme `wajinga ndio wali-wao'
    Umasikini uliokithiri kwenye nchi yetu hii utazua mengi,na nina wasiwasi haya matabaka ya walio nacho na wasio nacho yatazidisha msuguano mbaya katika jamii yetu hii.
    Maoni yangu, ni kuwabanma hawa wanaojiita waganga wakienyeji, na njia njema ni hiyo ya kuhakikisha kila anayefanya hii kazi kasajiliwa na kujulikana ili kusiwe na upenyo wa kufanya ufisadi.
    Mungu atuepushie na hili balaa, kwani dunia nzima imeshituka kusika watu wanadanganyika kuwa utajiri huja kwa viungo vya wanadamu, hayo ni mawazo ya enzi za giza na hayana ukweli!

    emu-three
    Karibuni kwangu tunaendelea na kile kisa chetu cha: uchungu wa mwana sehemu ya tano:http://miram3.blogspot.com/2010/07/uchungu-wa-mwana-5.html

    ReplyDelete
  4. Emu-three asante kwa kumjibu asiye na jina. Ni kweli sisi ni binadamu na kila binadamu ana kosea. Labda wewe usiye na jina hukosei.

    Kaka chacha itakuwa mwisho wa dunia:-(

    ReplyDelete
  5. Nisiye na jina kwani nimekosea nini? Naona hamtaki kukosolewa. Mtu utaandikaje maauwa ukimaanisha mauaji? Mimi nilifikiri pengine ni Kingoni. Kama mnakereka NENDENI MKAJINYONGE!!!!!!!!!! Au fanyeni proof reading kabla hamjaposti huu upupu wenu! Don't get me started aka!

    ReplyDelete
  6. Mungu wananusuru hawa wenzetu wanaowindwa kama wanyama pori

    ReplyDelete
  7. nimetembelea blog yako hongera nadhani wewe ni mwandishi mzuri. Ila habari ya albino imenigusa zaidi kuliko zote. Kuhusu vision yangu ni kweli ni jambo zito ila halina janja. Matatizo tunayo kumbana nayo ya kitendaji serikalini, vitko ndani ya jamii sehemu kubwa ni matokeo ya mifumo ya malezi, Mtoto umuleavyo ndivyo akuavyo. Ukweli mfumo yetu ya malezi inamapungufu makubwa. Kuna sehemu kubwa wazazi wanatakiwa kujua nini na namna gani ya kumelea mtoto kiroho n.k. Mifumo yetu ndiyo inayo tupa viongozi na watu wabovu ambao hata kama watakuwa na PhD hawawezi kuifaa jamii inavyositahili.

    Ukichungza nchi nyingi kwa mfano korea mara baada ya mapinduzi walijikita zaidi ktk kutengeneza miundo mbinu mzuri ya kanda watoto wakiamini kuwa mapinduzi waliyo yapata hayawezi kudumu bila kuyalisisha kwa watoto wao. Halikazalika nchi nyingi, mtoto anajengewa mitazamo ya uzalendo kupenda nchi n.k na mzazi wake. Walimu wa kwanza wa mtoto ni Baba na Mama rejea Musa na wana wa Israel hadi sasa wazazi ndio wanao mjenga mtoto ktk kipindi cha miaka minne hadisaba n.k. Walimu shle na material mbalimbali huongeza zaidi.Kila taasisi ina sehem yake. Asilimia kubwa ya watu wetu hawajui lakini personality ya mtu na utu uzima wake inatokana na ile miaka ya kwanza namna alivyo kuwa sheped na socialized na familia na jamii. Socialization ajents zote ni dhaif ktk jamii yetu mfano Familia(Households),
    Schools, na n.k na jamii kwa ujumla. Tutapataje viongozi wazri wakati wanazaliwa wazuri ila mfumo yetu ya malezi ndiyo inawaharibu.

    Mfumo yet ya Elimu nayo inatisha haiandai watu kuthubutu kujaribu bali inatandaa kwa tegemezi.Pia vipawa na vipaji havizingatiwi na kazi za wat hazithaminiwi. Ita tghalim sana, Kazi ya kwanza kubwa ni lazima kjenga upya mitazamo na watu kuwa na fikira sahihi, fikira zinazotazama kfanya mambo yawezayo kleta masilahi kwa baadaye.

    Niishie hapa kazi ni ndef ila ni lazima kfanya pale inapowezekana kwani kila kizazi kinawajibu wake. Nashukuru kwa kunisikiliza ubalikiwe sana.

    ReplyDelete