Mimi sipendi masarau
Mmasai alikwenda maeneo ya Jolly Club jijini Dar, na kuopoa changu (Wasichana wanaojiuza) na kuondoka naye hadi Kinondoni kwenye Guest House aliyofikia.
Lakini kabla ya kuingia chumbani kujivinjari na binti yule aliamua kupata bia mbili tatu kabla ya kujivinjari na kimwana.
Waliagiza Bia na nyama choma na wakati wanaendelea kunywa na kula nyama choma yule binti akambusu (Kiss) Mmasai kwenye shavu la kulia.
Mmasai: We ndito acha hiyo…….
Binti: Akambusu tena shavu la kushoto
Mmasai: (Akifoka kwa hasira) Aaagh….. nimesema acha hiyo wewe haisikii…
Binti: (Akiongea kwa kulegeza sauti kimahaba) Kwani vipi sweetie….
Mmasai: (Akafoka kwa hasira) Nimesema acha hiyo masarau lakini wewe bado nafanya hiyo masarau yako….eh!
Binti: Basi Honey, naomba yaishe kama hutaki….
Mmasai: (Akinyanyuka kwa hasira) naona wewe umesidi masarau yako.
Mmasai akatoka nje kumuita mlinzi wa ile Guest na kuja naye pale kwenye meza waliyokuwa wamekaa na yule binti.
Mmasai: Askari, mimi nimekuja na huyu binti hapa, lakini yeye ameanza masarau. Mara ya kwansa alinisonya kipande ya huku (akionyesha shavu la kulia) nikamwambia acha masarau, lakini yeye akaendele na masarau yake kwa kunisonya kipande ingine ya huku ( akionyesha shavu la kushoto) nikamwambia bado tu naendelea na masarau yako, lakini yeye akainiita Fisi (Yaani alipoitwa Sweetie) nikamwambia mimi sitaki hiyo maneno lakini tena ikaniita Nyani (Yaani alipoitwa Honey) sasa askari hiyo sio masarau?
Mimi nasema hivi, nataka utoe hii ndito nje, sitaki kuona mtu mwenye masarau.
Watu waliokuwa karibu walivunjika mbavu kwa kicheko………..
Habari hii nimetumiwa na rafiki toka nyumbani Tanzania na nikaona niiweke hapa ili isomwe
nanyi wenzangu pia. JUMAMOSI NJEMA JAMANI!!!
Usingisi naisa sasa njeeree!
ReplyDeleteNgoja nkatafute kitanda sasa! Jumamosi njema nawe!
bila shaka inakukubusha maandalizi ya mechi kabla hujamwonyesha masarau mumeooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
ReplyDeleteHii unaweza kuandika RIWAYA kabisaaaaa.
ReplyDeletestori imenikuna sana yaani hapa mbavu nazipeleka gereji...... lol
klabu ya Jolly imenikumbusha sana, stori za pale unaweza kuandika kitabu hakika..... lol nakumbuka enzi zileeeeee mitaa hiyooooo
Duh!!! kazi kweli kweli, Hao machangu nao waangalie watu wa kuchukuliwa nao jamani watakuja jikuta wanapata kibano hv hv, Wamasai wenyewe mimi naona kama zimewapindia mihasira ni papo kwa papo + ushamba wa kukaa maporini, wapo kama disign za kinyama wanyama, yataka moyo kuopolewa nao ingawa mabinti zetu ndio wapo katika biashara lakini kha!!!!!
ReplyDeleteIna maana Penina ukimpata rafiki/masai hakuopoi? mhh unacheza wewe,akikutaka lazima umpe kagugu!!
ReplyDeleteWamasai wameendelea sana. Mpaka jolly wanafika ama ni story tu?
ReplyDeletePenina: si wamasaai wote ni wanyama...lol! Kwa hiyo ukipata mmoja we nenda yae tu akufundishe namna ya kutafuna nyama bila kunona...lol
Stori za humu zinachekesha. Sijui kama Yasinta ndizo zimfurahishazo.
ReplyDeleteNi za kitoto sana ndiyo maana mimi nimecheka, lakini sio kwa jinsi zilivyo ila kwa kwa jinsi zilivyo vya kitoto.
Lakini habari yoyote inaletwa jinsi ilivyo na mtu hulazimishwi kuisoma.
"Black" mie nimeiona hii stori na kuishobokea na kunifanya niiseme. Sina sababu kubwa.
This Is Black=blackmannen