Sunday, May 23, 2010

TUMKARIBISHE DADA MAISTARA NA BLOG YAKE TEGELEZENI KARIBU SANAAA!!


Napenda kumkaribisha dada Maistara Wastara na blog yake iitwayo Tegelezeni zaidi ingia hapa http://maisarawastara.blogspot.com/

9 comments:

  1. Da Maisara karibu sana tujumuike pamoja

    ReplyDelete
  2. Nami pia nampongeza Dada Maisara kwa hatua hii. Halafu, ameanza blog yake na mada ya kusisimua. Namtakia kila la heri. Wadau tupo.

    ReplyDelete
  3. Ajiandae tu kupambana na akina ANNONY...
    Dada Maisara kublog yataka moyo dada yangu kuna mengi ya kujifunza na ya kukera pia tafuta mtaalamu wa ushauri nasaha kungali mapema kabisa, maana kwa mada yako hiyo naanza kuona timbwili likianza...LOL

    Nakutania dada karibu uwanjani usiogope wala nini kaza buti mwayego.......Tunakutegeleza

    ReplyDelete
  4. Karibu sana dada. Nafurahia ujio wako. Naona unaongeza nguvu kwenye timu ya kina mchungaji Koero, sista Yasinta, mwanamke wa shoka Da Mija, fundi mitambo Subi na wengineo.

    Kuwa ngangari. Hakuna kurudi nyuma.

    Karibu sana.

    ReplyDelete
  5. Kariiiiibu sana Da Maistara katika ulimwengu wa kublogu.

    ReplyDelete
  6. Karibu sana dada. Tuko pamoja nawe na usisite kuuliza kunako kigugumizi

    ReplyDelete
  7. Nawashukuruni sana kwa kunikaribisha, ni bahati mbaya kuwa blog yenyewe imetengenezwa na mpita njia ambaye ni mteja wetu hapa ofisini kwetu.

    Nawaombeni radhi kwani kuna mapungufu mengi sana na ameniahidi kuyashughulikia leo hii jioni.

    Kwa kifupi, Bado blog ipo katika matengenezo madogo madogo nawaombeni sana msisite kunifahamisha pale mtakapoona kuna tatizo.

    Email yangu ni hii hapa:
    wastaramaisara1@gmail.com

    Naomba ushirikiano wenu wa dhati kabisa.

    Wakatabahu
    Ni mimi mdogo wenu na dada yenu

    Maisara Wastara

    ReplyDelete