Sunday, May 23, 2010

Wikiend njema na pia Nawatakieni jumapili njema:- kwa sala hii ya nasadiki!!!!!

Haya ndugu zanguni unganeni nami na tusali sala hii
Nasadiki kwa Mungu baba mwenye enzi, muumba Mbingu na dunia. Na kwa Yesu kristu, mwanae wa pekee bwana wetu, aliyeumbwa kwa roho mtakatifu , akazaliwa na bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akasurubiwa, akafa, siku ya tatu akafufuka katika wafu,akapaa Mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu baba Mwenye enzi. Toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa roho Mtakatifu kanisa moja takatifu katoliki la kitume. Maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele. Amina.

Jumapili njema kwa watu wote wa dunia hii.


5 comments:

  1. Nawe pia uwe na Jumapili njema. Ahsante kwa sala.

    ReplyDelete
  2. Siku itakuwa njema tu pale utashiba,lakini ni wangapi wanasiku njema?

    ReplyDelete
  3. At least nimepata kusali. dada Am back tafadhali karibu unitembelee.Jumapili njema!

    ReplyDelete
  4. Hodi humu, mie ni mgeni hapa, naomba ushirikiano wako

    ReplyDelete
  5. Ukizingatia pia kuwa leo ni siku ya Pentekoste, na watu wakanena kwa lugha za mataifa wanayo yafundisha baada ya kujazwa uwezo huo na Roho mtaatifu. Mambo ya Kiimani hayo..... Jumapili njema Dada

    ReplyDelete