Sunday, May 30, 2010

LEO HAPA NI SIKU YA AKINA MAMA/MORS DAG!!!


mama na bintiye 1997 Mahumbato/Mbinga

Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi akina mama wote duniani bila kumsaau mamangu.Ingawa hayupo nasi kiwili lakini kiroho yupo nasi Ahsante mama. Pia napenda kuwapongeza akina bibi, shangazi, mama wakwe na mabinti woote katika dunia hii


Hapa ni binti mwingine na mama yake jana 29/5 /2010 Sweden

Hapa Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mametu mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mametu hasa akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka.( kwa niaba ya mama) Pia pongezi nyingi kwenu akina kaka babu, baba, mjomba na vijana wote kwani bila uweopo wenu basi tusingekuwepo hapa duniani.

Hakuna sherehe bila mziki nami nimeona mziki huu utafaa siku hii ya leo Haya karibuni tumsikilize dada Emmy Kosgei akiuliza nani kama mama? katika wimbo wake huu!!







NA PIA NATAKA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TANO MUWE NA WAKATI MZURI SANA WOOOTE JUMAPILI NJEMA SANA!!

10 comments:

  1. Hongera Yasinta na kina mama wote. Kweli wanao wamekusoma na inawezekana kabisa wanakuchokoza makusudi ili wapate kila kitu. Hii nimeipenda.

    Salamu zao.

    ReplyDelete
  2. Happy Mother's Day to all caring mothers who are proud to be mothers and also proud of their children. Pia hongera dada Yasinta kwa binti mrembo kabisa (naona anazidi kukua na kesho kutwa tu atakuzidi urefu hehe).

    ReplyDelete
  3. Mum!
    You are a very good person but i can't say how much i love you with words, i hope that you understand.

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa kuwa mama mwema.
    Yasinta you have a great family, god may bless you and your family.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Sis Yas na akina mama wote huko Uswidini. Mungu akujalie na kukuzidishia milele amina

    ReplyDelete
  6. Wow nice picture,mmependeza sana mama na mwana,he yaani Camila sasa unalingana na mama urefu? hongera sana.

    Happy mothers day,kweli kwenu imechelewa sisi huku imepita siku nyingi na sasa tunasubiri fathers day,hongera wanawake wote duniani na mungu azidi kuwapa moyo wa uvumilivu na upendo siku zote.

    ReplyDelete
  7. hapo kwenye picha ya pili sio Yasinta/ na huyo ndo binti yake? she is so cute, thanks to lord

    ReplyDelete
  8. Hongera zangu nyingi sana kwako wewe Dadangu na akina mama wote wa huko na wote duniani. Pia mmependeza sana na mwanao kwenye picha hiyo, nimeipenda. Hongera sana.

    ReplyDelete
  9. sijachelewa waama jamani kila lililo jema

    ReplyDelete