SALA YA ASUBUHI
Siku mpya inaanza, Nimuabudu Mungu kwanza: Mungu wangu baba yangu, Upokee shukrani yangu. Wewe kwa usiku mzima, ulikuwa kwangu daima: kunilinda kwa amani na mitego ya shetani. Kwako baba wa milele, Ninaomba neema tele: Niepuke dhambi zote, Nikutumikie pote. Ubariki kazi yangu, Shida na furaha Zangu. Mama safi ee Maria, Nipe msaada wako pia. Ee malaika kiongozi, Nipeleke kwa Mwokozi. Yesu nijalie neema, Niwe daima mkristo mwema. Amina.
NIA NJEMA
Nia na kusudi langu, Kumheshimu Mungu wangu. Najiunga kwa imani Na mkombozi msalabani. Roho, mwili chote changu Pendo na uzima wangu, Wazo neno tendo lote, Namtolea Mungu yote. Mungu wangu nakupenda, Wala dhambi sitatenda. Iwe kazi, nipumzike, Amri zako tu nishike. Utakalo nitimize. Kila kazi nimalize. Litukuzwe jina lako, Siku nzima iwe yako. Kwa utii navumilia Shida na matata pia. Nipe, Bwana neema zako, Niongeze sifa yako. Amina.
SALA YA JIONI
Sasa siku inakwisha. Kwako, Mungu, napandisha. Moyo wangu kwa shukrani, Nipumzike kwa amani. Mema mengi umenipa, Ninashindwa kukulipa. Baba mwema, ondolea Yote niliyokosea. Yesu mpenzi, Unijie, Ombi langu usikie: Unifiche mtoto wako Ndani ya jeraha zako. Ewe mama, nipe neema, Raha na usiku mwema. Roho mlinzi, ukakeshe, Pepo asinikoseshe. Naiweka roho yangu Mikononi mwa Babangu. Bila hofu napumzika, Mwisho kwako nitafika. Amina.
NA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA. NI JUMAPILI YA 19 YA MWAKA HUU NA YA PILI YA MWEZI HUU WA TANO!!!!
Nimeshasali sala ya leo, mpango wa kwenda "chachi" sasa haupo tena!!
ReplyDeleteJumapili njema na kwako pia
Ameen!
ReplyDeleteAsante sana, nawe pia na wapendwa wako wote hapo. Kila laheri.
ReplyDelete