Tuesday, April 27, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA DA MIJA/MWANAMKE WA SHOKA!!

Mwanamke wa shoka Da Mija Shija Sayi


Ni furaha kuwa na rafiki kama Da Mija na leo ni siku tukufu kwako. Ni siku ambayo ulitokea hapa duniani . Napenda kukutakia yote mema, uishi miaka mingi uwe bibi kizee na wajukuu wengi uwe nao. Mija, kama wote tunavyomfahamu alizaliwa hapa dunuani ili awe mwanamke wa shoka nakuheshimu na pia nakupenda sana .HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA RAFIKI YANGU na MWANAMKE WA SHOKA WETU!!!!!!

14 comments:

  1. Epi besdei da Mija. Mungu akubariki.. amen.

    ReplyDelete
  2. Da Mija. Sijui kama utakielewa hiki Kisukuma kwani ni chenyewe hasa kile cha ndani ndani...

    Ikalaga na myaka mingi, ugiguluhe mpaga usache lino limo giti lya ngili. Seba Agulanghane, usiminze bulunde na nyawe!!!

    Ubarikiwe wewe pamoja na hao wanawake wa shoka bila kumsahau shemeji...

    ReplyDelete
  3. nami nitumie fursa hii kukupongeza sana sana Da Mija. Uwe na maisha marefu yenye mafanikio.

    Kumbuka kulinoa shoka lako mara kwa mara

    ReplyDelete
  4. Da Mija HONGELA sana kwa siku yako tukufu.

    Kama alivosema kaka Masangu, ujaaliwe mamyaka mengi na mola akuongeze katika kila mapito yako.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Da Mija kwa siku yako ya kuzaliwa, yale unayoyatamani moyoni mwako na yatimie.

    ReplyDelete
  6. Kila laheri na jema katika haya maisha.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana kwa kuifikia tena siku yako hii muhimu katika maisha yako,pia ni wakati wa kumshukuru sana mungu kwa kukuwezesha kuiona tena.

    Uwe na siku nzuri mkema wa mbasa!!kaka Masangu kamaliza kila kitu,imebidi nicheke sijui hiyo msg. umeielewa? maana inachekesha.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana.Ila nilitaka kujua kwanini ni mwanamke wa shoka!! shoka kwanini??

    ReplyDelete
  9. Happy Birthday Da Mija Mungu akujalie maisha marefu yenye furaha na afya tele

    ReplyDelete
  10. 'ongela' sana dada mija kwa kushusha kalenda nyingine na kuanza kuhesabu nyingine.

    ni siku njema kwako kutafafari yaliyojiri mpaka leo na kujipanga sawa sawa katika miaka ijayo (ikiwezekana kwa mola iwe mingi sana)

    mambo ya mtu wa kwenye picha ya Israel G Saria hapo juu yatakuwepo?

    ReplyDelete
  11. Yasinta niseme nini kwa heshima uliyonitunuku leo. Asante sana kwa kunipatia nafasi kibarazani kwako nina furaha kuliko maelezo.

    Wadau wote ninashukuru sana kwa moyo wenu wa kujali, Mfalme Mrope, Matondo, Fadhy Mtanga,Ngw'anambiti, Edna, Chibiriti, Passion4fashion, Israel, Mumhery, Mwaipopo na wengine wote Mungu awabariki sana.
    @Matondo nimeelewa nusunusu, huwezi amini kisukuma kinanipiga chenga ila mwaka huu nitakikazania sana.

    @Mwaipopo nimekupata hayo mambo yatakuwepo sema wewe sasa ndio unamiss.

    @Israel nimelipenda swali lako, umenipa wazo la kuandaa makala juu ya maana ya mwanamke washoka, ila kwa ufupi kila mwanamke ni mwanamke washoka maana ana roho maalumu ambayo Mungu amemuwekea ambayo hutakaa uipate kwa mwanaume yeyote. Da' Yasinta au nasema uongo?

    Nawatakia kila la heri wadau wote, nawapenda mno.

    ReplyDelete
  12. Da mija Ahsante kwa kushukuru ni furaha yangu kukuweka hapa kibarazani kwangu kwani kumbuka sisi sote ni ndugu ni watoto wa baba mmoja. Na Da Mija uko sahihi kabisa kuhusu Mwanamke wa shoka.
    UPENDO DAIMA!!

    ReplyDelete
  13. mwanamke wa shoka kweli, i can see!

    ReplyDelete