Thursday, April 22, 2010

BWANA MATATA HAJUI KUSOMA+KUMBUKUMBU

Je? huyu naye ni bwana matata?


Mada hii nilishawahi kuiweka hapa kibarazani, lakini leo katika pitapita nimekukta picha hii nikakumbuka na nimeona si mbaya kama tukijadili tena kwa pamoja picha nimeipata hapa Haya soma haabari yenyewe hapa chini kuhusu bwana matata.

Namshukuru babangu kwa kutunza kitabu hiki leo nimefurahi sana nadhani hata wenzangu mtafurahi pia kukumbuka hadithi hii:-
Bwana Matata yupo mjini, anauliza uliza njia ya hospital. Kuna kibao hapo njiani, lakini haui kusoma kibao.Bwana Matata anaona aibu kuuliza njia tena, anaona aibu kwa sababu hajui kusoma. Sasa anafuata njia ya bomani
Bwana Matata amechoka sana. Amechoka na safari, pia amechoka kuuliza uliza njia. Amelala kwenye kibao, kibao kinasema HATARI. Lakini Bwana Matata hajui kusoma, tena amechoka mno. Amelala njiani kwenye kibao

Bwana Polisi anapita, anamwona Bwana Matata amelala kwenye kibao. Bwana polisi anamwita, mzee vipi? Kwa nini unalala hapa? Huoni kibao? Lakini Bwana matata amechoka sana amelele kama gogo. Polisi amawita tena, kwa nini unalala hapa kama gogo? Kuna hatari hapa. Lakini bwana matata hana habari ya hatari hajui kusoma.

Bwana Matata akaamka, akasimama na kumwambia polisi, nataka kwenda hospitali. Mtoto wangu yupo hospitali ni mgonjwa sana, lakini nimepotea njia. Bwana polisi akasema, umepotea njia? Fuata hii Bwana Matata akafuata njia ile. Kinachoendelea naadhani mnajua

4 comments:

  1. Yasinta shukrani kwa kutuletea kumbukumbu hii, Leo nimeisoma habari hii kwa jicho tofauti na lile nilipokuwa mtoto. Zamani niliangalia sana umuhimu wa kujua kusoma katika kitabu hiki, lakini leo nimeangalia tatizo kubwa tulilonalo watanzania la kuogopa kuuliza unapokuwa hujui kitu kwa kuhofia kuchekwa, sijui hali hii ilitokea wapi? utakuta mtu anakubali kubaki mjinga kuliko kuuliza ilhali asionekane hajui. Jamani inabidi tubadilike.

    Yasinta mpe shukrani zangu Mzee Ngonyani kwa kutunza vitabu maana leo vinatusaidia wengi.

    ReplyDelete
  2. Da Mija: Tatizo linaweza kuwa ni zaidi ya kutotaka kuuliza.

    Ni suala la uelewa tu. Kama huyo anayesoma SMS ameshindwa kuona hilo tangazo ama kulitilia maanani ni tatizo kubwa. Kwani hujawahiona kibao cha 'usikojoe hapa' lakini utashangaa ndipo nyasi zimeungua ama sehemu kubadilika rangi kwa kukojolewa? Na baadhi wa wanaokojoa hapo ni walewale waloweka kibao hicho!

    Ama hujawahi kusikia wananchi wakipiga kelele kama Da Mija kuwa uongozi ni mbovu ilhali huyo huyo alipiga kura baada ya kupewa kanga na sukari, t-shirt na kofia na sh 500 na vikamfanya akavutiwa na sura ya huyo anayempa shida sasa?

    Its too complicated!!! :-(

    ReplyDelete
  3. Jamani sheria zimwewekwa ili zivunjwe, zisipovunjwa haziwezi kutungwa mpya jamaa anajitahidi kuzivunja.
    Anyway mie nafikiri ni msongo wa mawazo, maana ukiwa na mzigo wa mawazo huwezi kujua hata kinachoendelea katika maisha yako.

    ReplyDelete
  4. Mija shukrani kwa baba zimefika.Na nahisi tu huyu mzee ana vitabu vule vya Juma na Roza. Zamani kweli ilikuwa safi.
    Ahsante Chaha na Edna!!

    ReplyDelete