Mwenzenu nimeulizwa hili swali na watoto wangu niimeona ni vema kama nikipata msaada wenu kwani kwangu lilikuwa swali gumu kidogo. Swali lasema hivi:- Hivi kwa nini viumbe hai vyote vizaliwapo havina meno na baada ye huota meno? Na kwa mfano binadamu, baada ya kukua na kufikia miaka 4 mpaka labda 13 meno ya utatoni hutoka na kuota mapya. Na halafu jinsi wazeekavyo hupoteza meno yote. hivi ni kwanini?
sio watoto wako tu, tupo wengi tunasubiri majibu hapa.
ReplyDeleteMAPENGO wakati wa kuzaliwa na wakati wa kuzeeka: duh!
ReplyDeletenadhani yanakuwapo kwa kuwa hayahitajiki wakati huo na yanapotea (meno kuota) wakati meno kuhitajika...lol
Kijasho kimenitoka...
ReplyDeleteItabidi tumtafute kaka Chib atupatie funguo ya chumba cha vilaza...lol
@Da Mija: :-) Nilitaka kukwepa kujibu swali hili maana sikupenda sana kujulikana kama na mimi kwa swali hili naelekea kuwa kilaza :-)
ReplyDeleteNaanza kwa kusema uongo ufuatao
sio viumbe wote huanza kuishi bila meno, wanyama kama kobe na kasa huzaliwa na meno ambayo hayang'oki mpaka wafe labda ndo ukayang'oe(Mtadai kasa hazaliwi kwa sababu anatoka katika yai :-(
Mnyama mwingine anayezaliwa na meno ni hamster - Da Subi atatutafsiria hilo neno kwa kiswahili, mie nimesahau kidogo. Na huanza kutafuna moja kwa moja anapozaliwa, ndio maana wanamwita ya kuwa anazaliwa kula tu!
Kwenye mada sasa... nakuna kichwa kwanza, labda niulize swali tu
Kwa nini hususan binadamu mchanga na mzee kikongwe wanafanana japo kiasi katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na akili, maana kibabu anaweza kulilia pipi ati,..., umbo, meno aka kibogoyo, kazi, kuona, vyakula wanavyokula, maana sijamuona kijeba anatafuna mfupa.
Sorry nilikuwa najitahidi kukimbia ukilaza, natumaini mmenielewa
Siku ukirudi ruhuwiko kawaangalie wale ndama ulioowaacha au wapigie simu jamaa zako, watakwambia kwamba mpaka na wao wameshazaa lakini bado hajaota meno ya mbele ya juu, sasa sijui kwa nini?
ReplyDeleteNg'ombe huwa hawana meno ya juu ya mbele ila chini yako nane, na yale ya canine hawana juu na chini (kuna uwazi tu kama mapengo) halafu yanafuata premolars 12 (juu 6 na chini 6), na mwisho molars 12 (juu 6 na chini 6)jumla 32
swali nzuri..da mija msifunge mlango wa Vilaza tafwadhari(tone ya mrisho kwenye salam kwa mjomb rudi)
ReplyDeletenasubiri JAWABU..au niwachagulie mji mnipe jibu..Nang'urukuru
mbona hawaulizii nywele?? bado wadogo nini?? kama ndevu, mav%@& na bustani yamapenzi (love garden / garden love?)
ReplyDeletekuna jamaa alijikata kichwani ili kuona kama kuna mizizi yanywere, hakuiona, alilia na kusaga meno
Mmmh!kumbe kina vilaza tuko wengi,hapa kuna mengi ya kujifunza.
ReplyDeletemimi najua ila sitaki kuwaambia, mkitaka niombeni niwaambie
ReplyDeleteUsiye na jina 10.02 pm, tafadhali nakuomba uniambia napiga hata magoti TAFADHALI.
ReplyDeleteNshaghairi mie, sisemi!! mkitaka tafuteni mtandaoni nimeweka majibu!!
ReplyDeleteAnony tafadhali tuko chini ya miguu yako.....
ReplyDeleteKwa kweli hatamimi nimeona swali ni ngumu kidogo mimi kwa jibu langu ni hivi binadamu wanapozeeka meno yao hupekechwa na wadudu na baadaye kung'ooka
ReplyDelete