Tuesday, February 23, 2010

KAMA MASIHARA: BLOG YA MAISHA YATIMIZA MIAKA MIWILI LEO!

Sijui hapa nipo wapi au kweli ni mimi?

Ni kama vile mtoto azaliwapo na kukua katika hatua tofauti tofauti, na mara nyingi hatua hizo huenda sambamba na mabadiliko ya kimwili na kiakili. Nakumbuka ilikuwa ni kama mzaha hivi, siku moja nikiwa kazini, tena nikiwa nimechoka , nikaanza kuwaza na kujiuliza, hivi kuna akina Yasinta wangapi hapa duniani. Sikujua kwa nini nilijiuliza Swali hilo, kwani sisi binaadamu huwa tunapitiwa na mawazo mengi sana, kama sikosei niliwahi kusoma pale kwa kaka Shabani kwenye kijiwe chake cha Utambuzi na Kujitambua kuwa kwa kawaida sisi wanaadamu huwa tunapitiwa na mawazo 5000 mpaka 6000 kwa siku…..ajabu eee!!!

Basi swali hilo lilinifanya nijaribu kufanya utafiti kupitia Google, na pale nikaandika neno Yasinta, nililetewa habari nyingi sana zinazowahusu akina Yasinta, lakini nilivutiwa na habari iliyoandikwa Kiswahili na nilipofungua nikakutana na Blog ya kaka Markus Mpangala ya KARIBU NYASA.

Nilikutana na habari nyingi sana za nyumbani na nilivutiwa na sana baadhi ya makala zake na maoni ya wasomaji mbalimbali, niliisoma habari ile ya Yasinta kwa kirefu sana, ilikuwa ni simulizi nzuri mno iliyoniondolea uchovu kwa siku ile na si hiyo tu bali nilijikuta nikipitia blog mbalimbali za wanablog wengine ambao Markus aliwaunganisha na blog yake.

Nilishikwa na hamasa na nikaona ni vyema niwasiliane na kaka Markus ili niweze kumfahamu zaidi, nakumbuka nilipomtumia email hakukawia kunijibu na ikawa ndio tumefungua ukurasa mpy wa mawasiliano kati yetu.

Ni katika kipindi hicho ndipo nilipopata wazo la kutaka kublog na kwa msaada wa kaka yangu huyu Markus Mpangala ndio hapo mnao tarehe 23/02/2008 blog hii ya maisha ikazaliwa.

Leo hii Blog hii ya Maisha inatimiza miaka miwili kamili huku nikijivunia mafanikio niliyoyafikia tangu nilipoianzisha blog hii. Kama nilivyosema hapo awali kuwa mtoto anapozaliwa hukua katika hatua tofauti tofauti na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa blog hii ya Maisha, kwani nilianza kama masihara kuandika habari mbalimbali za kijamii, za kufurahisha, za kuhuzunisha na za kuburudisha pia, na kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kujifunza mambo mengi sana, kiasi kwamba siwezi kusahau mafanikio niliyoyafikia, na ndio maana, hivi karibuni nikaboresha jina la blog hii na kuiita MAISHA NA MAFANIKIO, kwani mafanikio niliyoyafikia ni kutokana na maoni na ushauri kutoka kwa wasomaji na wana blog wenzangu.

Sitaweza kuyataja mafanikio ya blog hii kama sitawashukuru wale wasomaji ambao kwa kuvutiwa na blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO wamekuwa wakinitumia habari zao na kunitaka niziweke hapa kwangu nan hivyo kuleta changamoto kutoka kwa wasomaji wengine.

Kusema kweli siwezi kumtaja mtu mmoja mmoja, wale wote waliofanikisha uwepo wa blog hii kwani ni wengi sana na ninaamini nitawachosha kwa kusoma, ila ningependa kuwashukuru wooote mliofanikisha uwepo wa blog hii, bila ninyi naamini nisingiweza kujivunia mafanikio haya niliyoyafikia.
Naomba msichoke kutembelea Blog yenu hii na bila kusahau kuwa michango na maoni yenu ni muhimu sana katika kuiboresha blog hii.
Pia napenda kumshukuru dadangu Mariam Yazawa kwa kunitumia hiyo picha hapo juu. kwa kumsoma zaidi gonga hapa
Nawashukuru sana na ninawatakia kila la kheri katika shughuli zenu za kila siku Mungu awabariki wote.

25 comments:

  1. Hakika ni faraja saaana kuona UNATIMIZA MIAKA MIWILI na bado waendelea kupenda kutupa MAISHA NA MAFANIKIO.
    Sina ninaloweza kukutakia zaidi ya KUKUOMBEA MIAKA MINGINE KUMI ZAIDI KATIKA KUELEZANA MAISHA NA MAFANIKIO.
    Amani kwako Dada na kwa blogu yetu.
    Asante kwa Kaka Markus kwa kuanzisha hii na Dada Mariam kwa kuinogesha.
    Mwisho kwa ushirikiano wako na familia yako kwetu sote.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. HAPPY BIRTHDAY TO MAISHA - sasa ndio MAISHA NA MAFANIKIO!

    "Wadau" wako sisi tupo...au sijui nijisemee mwenyewe ila mie ndio nilikuwepo (japo sikuwepo mwaka huo ilipoanzishwa), nipo na nitakuwepo. Pia asante kwa yote hapa ya kufurahisha, kuhuzunisha na kuelimisha katika MAISHA.

    Tunaendelea!

    ReplyDelete
  3. Kuna nyakati katika maisha yangu, huwa naishiwa maneno kabisa. Nyakati ambazo jambo fulani hunifurahisha kupita kiasi.
    Leo tena, nimekutana hili la blog ichangamshayo hisia halisi za maisha.
    Kwanza nataka nikupongeze kwa jina tu la blog yako. Unajua waweza kuanzisha kitu kama masikhara pasipo kufahamu kitu hicho kitateka hisia za wengi kwa namna gani! Jina tu la blog liliashiria umaarufu wa blog yako.. Na hilo limefanikiwa.

    Lakini pia, umaridadi wa yale uyawekayo katika blog yako. Nani angepita mbali pasi kupita kwako ili kuokota mambo muhimu ya maisha?

    Niseme tu pengine, unastahili pongezi. Kazi yako nzuri sana. Nasi twajivunia hili.

    HONGERA SANA DA' YASINTA NA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana kwa kublog bila kusimamama kwa miaka miwili sasa. Kila la heri

    ReplyDelete
  5. MAISHA NA MAFANIKIO.
    hakika sina zaidi ya kusema ASANTE kuwa mmoja ya watu waliohusika kwa uandishi wa KITABU hiki cha BLOG yako. Kwangu naamini duniani tupo kwaajili ya wengine yaani watu.
    Nakutakia mafanikio mema maishani na idumu blog ya Kingoli, Litumbadyosi,Ruhuwiko n.k MANI IWE NAWE UPENDE UWE NAWE

    ReplyDelete
  6. Naomba nikiri kuwa, mimi ni mmoja wa wasomaji wa blog hii ya maisha ambao sipendi kupitisha siku bila kuitumbulia macho, kwani karibu kila siku nakutana na changamoto ambazo huifanya akili yangu kutafakari sana. Kwa kiasi kikubwa nimekuwa nikijifunza mengi kupitia blog hii ya MAISHA.

    Pamoja na kumpongeza dada yangu Yasinta kwa blog yake kutimiza miaka miwili, lakini pia ningependa kumpa hongera kwa kuliboresha jina la blog hii ya maisha kwa kuiita MAISHA NA MAFANIKIOI.
    Ni kweli katka safari ya miaka miwili, naanimi yapo mengi umefanikiwa nayo. kwa hiyo umeitendea haki blog hii kuiita jina hilo.....

    Naitakia blog hii maisha marefu na idumu kwa miaka kumi na zaidi kama alivyoserma kaka yangu Mubelwa Bandio...

    Blessings

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Yasinta, Hongera mwanakwetu, Tunamshukuru sana Mungu kwa kutuletea ili atuletee MAISHA NA MAFANIKIO BLOG. Kwa kweli mbali na kujifunza mengi huwa naburudikia sana na posti zako.

    Basi ubarikiwe sana na uzidi kutufunza mengi Mwanamke wetu wa shoka.

    Ameni.

    ReplyDelete
  8. Hongera Mwaniwane!
    Idumu BLOGu ya MAISHA na MAFANIKIO!

    ReplyDelete
  9. Da Yasinta-Nanukuu: 'Naomba msichoke kutembelea Blog yenu hii na bila kusahau kuwa michango na maoni yenu ni muhimu sana katika kuiboresha blog hii'. MWISHO wa kunukuu.

    KWA WALE WOTE WAOTEMBELEA HAPA MAISHA NA MAFANIKIO: Biblia yaseama "Ee Yerusalem, nikikusahau wewe, mkono wangu unyauke" NANYI WASOMAJI: Mkiisahau blogu hii mtajiju...lol

    Happy birthdate Maisha naMafanikio!

    ReplyDelete
  10. Hongera sana! Endelea na juhudi zako za kutuonyesha na kutuelimisha kuhusu Maisha. Kila la heri!

    ReplyDelete
  11. Pongezi kwa blogu nzuri yenye kuelimisha. Naloweza kusema ni kwamba mimi kama msomaji wa blogu yako ninatarajia kujifunza mengi sana kubwa likiwa ni uzoefu, upeo, kubadilisha mawazo, kuwasiliana na pia kutatua masuala mbalimbali kwa njia ya hoja. HONGERA SANA

    ReplyDelete
  12. HONGERA SANA DADA YETU KATIKA FAMILIA YA WANA BLOGU MUNGU akubariki ZAIDI NA ZAIDI

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Maisha au Ruhuwiko blog kwa kutimiza miaka miwili,kiukweli unastahili pongezi hii ni kama safari ndefu mnaianza mkiwa wengi,lakini wengi huishia njiani na mnajikuta mnaobaki mpaka kufika mwisho wa safari ni wachache,naamini kabisa kuna wengi walifungua blog lakini hazikufika mbali ziliishia njian,kublog kwataka moyo hasa wa kujituma,vinginevyo utaishia bombambili na utashindwa kufika mfaranyaki....LOL,hongera sana binafsi nimejifunza mengi na naendelea kujifunza mengi kutoka maisha blog.xoxo!

    ReplyDelete
  14. hongera kwa kuvuta bange ya kublogu kwa miaka miwili mfululizo, tena kwa mafanikio. kublogu ni addiction kama ile ya sigara, bange n.k. tofauti ni kuwa addiction ya kublogu ni chanya tofauri na hizo nyingine. hapa unajifunza, unafurahi na unahabarishwa. nakutakia miaka isiyohesabika ya kuendelea kublogu kwa maisha na mafanikio.

    ReplyDelete
  15. MAISHA NA MAFANIKIO ni kisima cha mengi mazuri yahusuyo maisha. Dada, tunashukuru sana kwa kutujali kwa kutumia muda wako kutuelimisha na kutuburudisha kwa namna mbalimbali za kuvutia. Sio siri kuwa tunajivunia sana uwepo wako kwani mbali na kuihudimia vilivyo blogu yako ktk harakati za kutuelimisha na kutuburudisha,pia umekuwa muhamasishaji mzuri sana ktk maendeleo ya blogs nyingine.Hongera kwa hili na hongera sana tena sana kwa blogu yako kutimiza miaka miaka miwili.

    ReplyDelete
  16. Nakipongeza sana kijiji hiki kwa kutimiza miaka miwili!Ni kijiji ambacho kinatuunganisha kama ndugu na kututia hamasa ya kuendelea na MAISHA ili kupata MAFANIKIO. Nakupongeza dada yangu Yasinta kwa kuboresha ustawi wa kijiji chetu hiki. Sisi wakazi wake tuna kila furaha kushuhudia tunaufikia mwaka wa pili na tuna matumaini ya kuzidi kufikia miaka mingine lukuki! Hongera sana!

    ReplyDelete
  17. Dada Yasinta na Blog yako ya MAISHA hongera sana kwa kutimiza miaka miwili toka kuanza kwa blog yako. Dada tunafarijika kuona kazi zako nzuri BIG UP!

    ReplyDelete
  18. big up..maisha + mafanikio yaendelee...

    ReplyDelete
  19. Hongera sana, kikubwa sio miaka miwili peke yake bali na mengi ambayo sisi wasomaji wa kijiwe hiki ambayo tumeyapata HONGERA SANA na MUNGU AKULINDE

    ReplyDelete
  20. Hongera Yasinta kwa kuifikisha Blog ya Maisha hapo ilipo

    ReplyDelete
  21. Blog ya Maisha Juuuu,juuuu zaidi na idumu milele.Nakutakia kila laheri katika safari ya kuelimisha jamaii.

    ReplyDelete
  22. Hongera Dada Yansita kwa kutimiza miaka 2 blog.
    Mie mdau mpya hapa,ndio kwanza leo nimegundua blog yako.

    ReplyDelete
  23. Hongera sana, sie wengine bado hata nusu mwaka hatujafikisha, tutaendelea kujifunza mengi kutoka kwako.

    ReplyDelete
  24. Dada Yasinta,

    Hongera sana kwa Maisha na mafanikio kumaliza miaka miwili.

    Kama ni mtoto sasa naona anapaa hewani.

    Keep it up

    ReplyDelete