Sunday, February 7, 2010

Jumapili hii ya sita ya mwaka tusali sala hii!!!!!!

Ee Mungu unifanya niwe chombo cha amani yako. Penye chuki nilete mapatano, penye kukata tamaa nilete matumaini, penye huzuni furaha, Amina

9 comments:

  1. Habari ya huko?

    nilikuwa nimepotea sasa nimerudi tena.Natumaini wadau woote mu wazima.

    Nimepita kuwajulia hali..

    siku njema

    wasalaam

    edo

    ReplyDelete
  2. Ngoja niendeleze.......
    =Penye njaa tuletee shibe...
    =Penye ukame tuletee Mvua..
    =Penye kufeli tuletee kufaulu...
    =Penye ugumba tuletee ujauzito..
    =Penye giza tuletee nuru...
    =Penye barabara za vumbi tuletee za Lami..
    =Penye wagonjwa tuletee nafuu na uzima...
    =Pasipo na kujitambua tuletee Utambuzi...
    =Penye useja tuletee ndoa kama ya Kamala...
    =Penye ujinga tuletee werevu...
    =Penye maoni mbofu mbofu, tuletee MCHARUKOOO.......

    =MWISHO NAWAOMBEA WALIOKO UGHAIBUNI WAREJEE NCHINI TUIJENGE NCHI WAKATI NDIO HUU NA KAMPENI ZIMEKWISHAANZA....LOL

    ReplyDelete
  3. Ee Mungu unifanya niwe chombo cha amani yako. Penye chuki nilete mapatano, penye kukata tamaa nilete matumaini, penye huzuni furaha, Amina


    Mungu wasaidie BINADAMu wakubali ubinadamu!

    Kwenye chuki wakumbuke chuki ni msaada kwa binadamu kuwa binadamu.

    Kwenye kukata tamaa wakubali ni kuachia wasio kata tamaa wapate ulaji kwa hilo na ndio UBINADAMU ambao ufanyao MATUMAINI yawe na maana.


    Penye HUZUNI watu wahuzunike vizuri kwa kuwa ni ukichaa kwenye huzuni watu wasipokuwa na ufanisi wakuhuzunika.

    Na labda wenye furaha WAINGIWE huzuni mara kwa mara KATIKA kuwasaidia wastukie ukichaa wa kuwa na furaha hasa katika dunia hii iliyojaa HUZUNI ambayo imegeuka ni ujanja kudharau yote mazuri yachangiwayo na HUZUNI.

    Amen!:-(

    ReplyDelete
  4. ahsante dada kwa sala...mbona kimya sana upooooo...ubarikiwe

    ReplyDelete
  5. Nimegundua wote tungekuwa tukitafsiri maisha kama Mtakatifu Kitururu tusingekuwa na stress kabisa kabisa!

    ReplyDelete
  6. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 8, 2010 at 6:40 AM

    Amina!

    ReplyDelete
  7. Ng'wanambiti hukufumba macho halafu umeitikia Amina!!!! Ahsante dada kwa sala nzuri. Tubarikiwe sote.

    ReplyDelete
  8. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 8, 2010 at 8:38 AM

    @Lulu: Umijuaje kama sikufumba macho?

    Na unadhani kuna tofauti kati ya kufumba na kutofumba macho wakati wa kusali? :-(

    ama ndo habari ya kulia na kucheka zote ni kelele?

    ReplyDelete
  9. Sala maarufu niipendayo ya Mtakatifu Fransisko wa Assisi.

    ReplyDelete