Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.
Na pia nakuomba:Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE JAMANI NA PIA NI JUMAPILI YA TANO NA YA MWISHO YA MWEZI HUU!!!!!!!!JANUARI
Nukuu :``Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA´´
ReplyDelete-Sina uhakika kama naielewa sehemu hiyo ya sala. Hasa nikiunganisha ``UIBARIKI´´ na ``katika dhambi´´.
Ila labda alengwaye kwa sala anaelewa .
Jumapili njema!
Asante nawe na familia yako.
ReplyDeleteAmani ya bwana Yesu iwe pamoja nawe.
ReplyDeleteMt. Simon hii sala nimetunga mwenyewe na baada ya miaka utaiona katika vitabu vya sala. si unajua sala zote kuna mtu ametunga au? Asante kwa kunitakia jumapili njema nimeimalizia kazini.
ReplyDeleteDada S. nami nasema Amina ingawa nimechelewa.
Edna ndugu yangu Asante sana.