Friday, January 29, 2010

Napenda kuwatakia mwema wa juma hili pia ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa kwanza!!

Kunywa lakini kumbuka pombe si maji (na kumbuka kama utaendesha usinywe ugimbi mwingi)

Wazee na vijana wa kijiji cha kibaa wakicheza bao kama sehemu ya kupoteza muda baada ya kumaliza kazi.
Au ngoja tumsikilize Dada Saida Karoli ili wenye kuselebuka

Muwe na wakati mzuri wote

15 comments:

  1. Eh...vile ni ijumaa ya mwisho wa mwezi...yaani siku zinaenda kama upepo!! hata huzioni!!! hehe

    Asante kwa nyimbo hiyo..naweza kuisikiliza kila mara na wala siuchoki kabisa.

    ReplyDelete
  2. Samahani! unauhakika gani hao wazee katika picha ya pili walienda kazini?

    ReplyDelete
  3. Candy1! Ni kweli siku zimepepea kama nini juzi tu nilitimiza miaka leo mwezi tayari ushaisha... Candy1! huu wimbo mwenzangu ninavyoupenda leo hii ninamaumivu ya kicha lakini we acha tu nimecheza...mpaka kijasho.

    Simon mt. Asante kakangu!
    Simon! nina uhakika kwani kazi ni kazi hata kuwa kirabuni ni moja ya kazi au hata kushinda hapo na kucheza hiyo bao hapo kutwa yote ni moja ya kazi sio lazima kuwa ofisini au?

    ReplyDelete
  4. UMKOMBOTHI HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  5. Weekend njema kwako pia.....Huyo mzee anakunywa ulanzi au Komoni?

    ReplyDelete
  6. yasinta mambo ya kutukumbusha komoni jamani. ngoja leo niende kilabuni nikagonge japo lita moja hivi. hii picha inantoa udenda ati!!

    ReplyDelete
  7. Huyo Mzee anafanana na wachagga, na hiyo chubuku na kofia. I bet ni mchagga.
    Weekend njema dada

    ReplyDelete
  8. Unanikumbusha mbali mpaka vilabu Matetereka na Madaba.

    ReplyDelete
  9. Sasa nakumbuka vilabu Matetereka na Madaba.

    ReplyDelete
  10. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 31, 2010 at 2:02 PM

    @Mt. Simon: hiyo kazi wanayoifanya hao wazee nayo ni muhimu ati :-(

    Nimependa huyo mzee hicho anachochangamkia...imenikumbusha Shirimatunda enzi hizo tunatoroka shule pale Moshi Technical - Karanga kwenda kupata 'kitochi' kimoja :-)

    ReplyDelete
  11. Dada ana sauti nzuri sana huyu,ila huo uchezaji wa wenzetu inabidi uwe umekula matoke ya nguvu,maana inahitaji uwe mkakamavu.

    ReplyDelete
  12. weee dada Yasinta, mwenu inywa kindi, komoni, ulai au myakaya? Akimaliza hiyo ataanza kuimba: a teresia wiganda, wiganda gani mbona wilya, unakula maganda ndizi bado za wenyewe.
    Blog yako huwa inanikumbusha kweli ungoni... MAKI

    ReplyDelete