Monday, December 14, 2009

zijue dondoo muhimu za kutunza kucha zako

Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.

Wanawake wengi na hata Wanaume pia wanaume hupenda kutunza kucha zao, kwani hujikuta wakikutana na vikwazo vya kushindwa kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha zao, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.

Kwanza kabisa ni marufuku mtu kula kucha zake kwani nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu ambao hupenda kula kucha zao, hivyo husababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.

Tumia glovsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele.

Dawa hizi za nywele ni kali sana hivyo huleta madhara makubwa endapo itashikwa bila kizuizi chochote na kusababisha rangi hiyo kushindwa kukaa vizuri.

Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu.

Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu. Kwani watu wengi hupenda kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha zao, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.

Usitoe hovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.

Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa.

Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, baada ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembeau kitu chenye makali.

4 comments:

  1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 14, 2009 at 9:57 AM

    umesema ni marufuku kula kucha lakini hujasema wenye uroho wa kuzila wafanye nini waache....lol

    zangu zimekatika nipe dawa ya kienyeji tafadhali....lol

    ReplyDelete
  2. Chacha he heh hee
    Weka pilipili kwenye kucha kila siku asubuhi kwa mwezi mzima. Utaacha kabisa

    ReplyDelete
  3. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 14, 2009 at 11:33 AM

    @Upepo Mwanana, Kwa wengine pilipili inaleta apetaiti....lol

    si itakuwa ishu hapo tena wawezakuta viganja vimebaki bila vidole hasa kama mtu mwenyewe ni mkurya ama mmaasai ambaye kula nyama mbichi ni RUKSAAA....lol!

    halafu hujasema pilipili ya aina gani...lol

    ReplyDelete
  4. Jamani sasa sisi ambao tunakula kucha na pilipili tufanyeje?

    ReplyDelete