Monday, December 7, 2009

KWA NINI WANAUME WANASHINDWA KULING'AMUA HILI?

Kuna wakati niliwahi kueleza juu ya wanaume kudhani kuwa kuwanunulia wake au wapenzi wao kila kitu kwa maana ya nyumba nzuri, magari ya kifahari na mavazi ya thamani, inatosha kupeleka ujumbe kwa mke au mpenzi wake kuwa anapendwa. Nilieleza kwa kirefu sana juu ya dhana hiyo jinsi isivyo sahihi na niliweka bayana kuwa, wanawake ni viumbe wanaohitaji kusikilizwa kuliko kitu kingine, bila shaka mlio wengi mnakumbuka makala hiyo.

Kwa asili wanaume wanapenda sana kuwasikia wake au wapenzi wao wakikiri kuwa wanawapenda na kufurahia tabia zao nzuri wema walio nao, vipaji walivyo navyo na sifa nyingine lukuki. Wanaume wanapopewa sifa za aina hii na wake au wapenzi wao hufurahia na kupata nguvu na kuona kwamba wana thamani kubwa mbele ya wake au wapenzi wao, kinyume na hivyo wanaume hukerwa na kutowajali wake zao.

Pamoja na kuoneshwa upendo lakini hata hivyo hiyo haitoshi kuwafanya wanaume wawapende na kuwajali wake au wapenzi wao. Kuna wakati mwanaume anakuwa na kazi nyingi sana na anatumia muda mwingi kwenye kujisomea au kuangalia Luninga, hata pale mke au mpenzi wake anaponyesha kwamba anahitaji kuwa naye kwa muda fulani. Kuna wakati pia mwanaume anajali zaidi kazi zake kuliko mambo mengine ambayo mkewe anayataka na kuyaona ya maana.

Naamini wengi mtakuwa ni mashahidi wa kauli hizi, “Yaani niache kazi zangu nikae kukusikiliza wewe na upuuzi wako, subiri nikipata muda tutaongea mambo hayo” kauli hizi ni sumu kali sana katika uhusiano, na huchangia kwa kiasi kikubwa ndoa na mahusiano ya wapenzi wengi kuporomoka.

Ni kweli kuwa kuna wakati mwanaume anaweza kuwa bize na shughuli zake,lakini pale mke au mpenzi wake anapohitaji ukaribu na yeye ni wajibu wake kuonesha kujali.
Kama mwanamke anahitaji kufanya jambo fulani ambalo inabidi mwanaume amsaidie, lakini inapotokea mwanaume kuonyesha kwamba hajali sana juu ya jambo hilo bila kujali kama yuko bize au hayuko bize, mwanamke huhisi kutothaminiwa na hiyo humuumiza sana kihisia. Lakini kama mwanaume ataonesha kujali hisia za mkewe na kumsikiliza kwa makini hata kama hatatoa ushirikiano hiyo tu inatosha kumridhisha mke au mpenzi kuhisi kuwa anapendwa na anasikilizwa.

Lakini utakuta wanaume wengi hawajali utashi wa kihisia wa wake zao na huamini kwamba wanawake wanachohitaji ni kupewa fedha au mali na kuhakikishiwa maisha ya kifahari basi.
Ukweli ni kwamba wanawake wanahitaji sana kusikilizwa hisia zao na kupewa nafasi pekee na mume au mpenzi wake pale anapohitaji nafasi hiyo ya kusikilizwa. Kumuonesha mwanamke kwamba hana thamani na hana nafasi ya kusikilizwa na badala yake kazi na kusoma, au kuangalia luninga kukaonekana ndio kuna thamani kuliko yeye ni kosa kubwa.

Ni jambo la msingi sana kwa wanaume kulifahamu hili kwa ustawi wa ndoa au mahusiano yao na wake au wapenzi wao, kwani wanawake wanahitaji nafasi kutoka kwa wanaume au wapenzi wao zaidi ya kitu kingine, maana hayo mengine yatakuja kujazia tu.

5 comments:

  1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 7, 2009 at 7:43 PM

    Si mnataka usawa? ndo huo basi....lol

    ReplyDelete
  2. INAWEZEAKANA WANG'AMUAJI WAPO ILA HAWAJULIKANI KAMA WANANG'AMUA.

    Tatizo hili siyo dogo, hata kama unamhitaji mwenzio jaribu kuangalia nini anchokifanya kwa wakati. Siku moja nilimsikia rafiki yangu akipokea simu ya rafiki yake wa kike...lakini alipomuuliza unasemaje, akasema anataka tu waongee kwani anaHAMU anye ingawa yupo kazini.

    Jamaa ikabidi aseme ninashughuli nyingi tutaongea muda mwingine. Lakini kabla ya hapo binti alihoji vipi mbona unachelewa kujibu au uko bize sana..... nikuache na ubize wako? aaah mi unaniudhi ninajikisia kuongea na wewe saizi.

    Mwisho jamaa akasema ninashughuli nyingi nawe unanichosha....kumbuka hii ndiyo inayonifanya nikupende wkani kabala sijaja kazini unanianda vema.

    lol haikuishia hpo yalikuwa mengi eti binti analalamika ubize wakati ANATAKA.

    ++++++++++++++++
    kwa mtazamo wangu mzee wa lundu nyasa, haya mambo yanahitaji muda, nafasi na umakini mkubwa. siyo kila wakati unaweza kumhitaji mwenzio halafu ukashindwa kujizuia kumhitaji kwani unaona wazi kuwa anakabiliwa na shughuli fulani.

    mfano anaweza kuwa mpenzi wa kipindi cha Larry King, Politica Mann, Fraed Zakaria GSP au Pimp My Ride kama mzee wa lundunyasa, kwahiyo ni vigumu kumwondoa katika kuangali TV.

    jamani kama ni usawa basi tuheshimiane tu hakuna jingine. Kubali unaHAMU ya kuongea na mumeo lakini unakuta anatzama TV au anafanya kazi zake...usimharibie... ila kumbuka wewe ndiye mali yake nawe ni mali yake UTULIVU muhimu sana. TUJISAHIHISHE

    ReplyDelete
  3. Lakini nisawa kaka markus m,nandio anavyo sema

    Ila pi wakina baba msijisaau sana mkapitiliza kwenye mambo yenu kumbukeni pia wake zenu wana itaji nafasi na nyie.

    ReplyDelete
  4. Hakuna kitu kibaya kama kusema samaki mmoja akioza basi wote wameoza. Ni hilo tu....

    ReplyDelete