Sunday, December 6, 2009

JUMAPILI YA LEO NAPENDA KUSALI SALA HII KWA WAGONJWA

Na tuwaombee wagonjwa
EWE Baba Mwenyezi, Mpaji wa maisha na afya, twakuomba uwaangalie kwa rehema wagonjwa wote, hasa wao wanaotakiwa maombi yetu, ili kwa baraka yako juu yao, na juu ya wao wawatumikiao, ikiwa mapenzi yako warudishiwe afya yao ya -mwili na ya roho, nao wakutolee shukrani katika kanisa lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

5 comments:

  1. Da Yasinta hakika wapaswa kupewa shukrani kwa upendo wako kwa watu ambao wapo shidani. Twaamini Mungu ameipokea sala yako.
    Ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  2. Na sisi tusio wagonjwa tutaombewa lini! :-)

    ReplyDelete
  3. Fadhy! asante, najitahidi kufanya hivyo.

    Chib! mbona una haraka kakangu. Haraka haraka haina baraka. Tulia siku yako itafika. jana ilikuwa ni siku ya wagonjwa.

    ReplyDelete
  4. Asante sana dada, nimebarikiwa, naimani kwa mapenzi ya Mungu watapona wagonjwa wote wa saratani ktk hospital ya ORCI

    ReplyDelete