Wednesday, December 23, 2009

BINTI YULE AKANILETEA KIDAMISI: MLETA HABARI ANAOMBA KUFUNGA MJADALA

"Wasomaji wapendwa, hii ni email kutoka kwa mleta habari baba Gabby, na mimi naiweka kama ilivyo"

Dada Yasinta, ahsante sana kwa wema wako wa kuiweka ile email yangu hapo kwenye blog yako na hivyo wasomaji kupata fursa ya kuchangia na kutoa maoni yao na mitazamo yao.

Kwa kweli sikutarajia kuwa habari yangu hiyo ingeleta malumbano kiasi hicho, lakini nashukuru kuwa pamoja na malumbano hayo lakini kuna jambo nimejifunza.

Nasikitika kusema kwamba, sitaweza kumshirikisha mke wangu katika huu mjadala kwa sababu ni kutaka kuibua jambo ambalo tumeshalimaliza kwa sasa, ila nashukuru kwa kuwa wote yaani mimi na mke wangu tumejifunza kutokana na tukio hilo.

Amani imerejea katika nyumba yetu na ninashukuru kwa kuwa mke wangu amenielewa na sasa uhusiano wetu umeanza kuimarika kama mwanzo.

Dada Yasinta, naamini kuwa hata wewe unafahamu kuwa katika maisha ya ndoa changamoto haziepukiki na mara nyingi huhitaji pande mbili kufanya kazi kwa pamoja katika kuzikabili changamoto hizo na hivyo maisha ya ndoa humarika zaidi na zaidi, kwani kama mkishindwa kuzikabili changamoto hizo kwa njia ya busara basi kati ya pande hizo mbili, upande mmoja ni lazima utakuwa ni dhaifu.

Nakushukuru sana wewe na wasomaji wa blog yako kwa ushirikiano mlio unyesha, na sasa naomba nifunge mjadala huu.

Idumu Bloga ya Maisha.

Ahsanteni sana.
Ni mimi Baba Gabby

17 comments:

  1. Haya Godwin, kiko wapi, sema sasa, mwenye mke wake kafunga mjadala.

    Binti mleta kidamisi, limemshuka, na katoswa, na maisha yana songa mbele....Big Up baba Gabby, maana wapambe walikuwa nuksi kweli kweli ...LOL

    ReplyDelete
  2. Pamoja na kumaliza mjadala ndugu yangu nilikuwa nafikiria kuandika waraka wangu jkwako ingawaje najua hainihusu sana.

    NAKUBALIANA NA KAKA GODWINI kuangalia kanuni za mazingira.. hata katika hukumu ndiyo maana wengin wanakimbilia kuangalia vipengele vya NATURAL USTICE(akiwemo waziri wenu lowassa).

    Ukitazama mazingira ambayo baba Gabby unayazungumizia nina uhakika na wala siwezi kumlaumu huyo binti kwa kukufanyia hilo unalolaumu na kuliona shule.

    KWANINI ULISEMA HUNA SIMU HALAFU UKATOA NAMBA ZAKO? aibu yako kakangu!

    KWANINI UBADILI NJIA KUMKWEPA KIUMBE ALIYEZALIWA NA MWANAMKE ETI KUEPUSHA SHARI????

    Ninakupenda sana naandika wala sina hiyana kwani hainiumi ila tunafundishana hapa jukwaa huru.

    ukisoam baru yako ina mtanziko mkuu kuhusu kile GODWIN anachokueleza ....lazima tutazame pande zote(natural justice),

    ETI KAKUACHIA MAPAJA? ha ha ha ha unachekesha wewe yaani unaitishika na mapaja/mishkaki hiyo?
    Na UKATOA NAMBA YAKO KWA KURIDHIA WALA TUSIDANGANYE ETI KUONYESHA USTAARABU HUWAZI LOLOTE.......ebwana baadhi yetu tunaelewa ukimiliki gari unakuwaje....ndiyo hayo NYAMBIZI LIKAKUINGILIA NA KUTKA KUKUVUNJIA KITOWEO CHAKO.

    Ndiyo maana nilisema wewe ni mzembe kutokana na maelezo yako ambayo kwangu yanamaswali ingawaje naelewa kuhusu hali ilivyo nyakati hizi.

    UMfunga mjadala kwa uamuzi wako lakini kumbuka SIJADANGANYIKA KWA HOJA DHAIFU KAMA HIZO....naelewa hali zetu zilivyo na wala unapohama njia eti kuepusha shari ni UZEMBE mwingine..........DUH AISE SIJUI NIITE HARAKATI ZA pIMBI AU KIPEPE
    ha ha ha ha ha ha ha ha ha
    UKITAKA KUMSHINDA ADUI SHAMBULIA NGOME YAKE

    ReplyDelete
  3. Niseme nini ilhali mjadala ushafungwa?
    Muhimu, bonge la shule.

    ReplyDelete
  4. Hajafunga baa Gabby labda anaogopa au ni fasihi tu...lol ha ha ha ha ha ha. hii mada tamu sana...natamani isifungwe kipindi hiki tuendele tu kubonyeza herufi. Wapi kunga kaka Fadhy nawe ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
    FUNGENI BASI TUWAONE LOL......

    ReplyDelete
  5. Katika kufunga mjadala, mwenyekiti wetu Da Yasinta unahitimisho gani? Maana hujatoa neno hadi wakati huu?

    ReplyDelete
  6. Mwanzo nilikuwa katikati, yaani nilikuwa sina uhakika kama ni baba Gabby au ni yule mrembo ndio aliharibu.

    Ila kwa hii njia aliyotumia kujitetea nimeshapata jawabu sahihi. HAPA HUITAJI KUWA MFALME SULEMANI KUONA KITU....

    Kikubwa..., Labda niseme shule nzito niliyosoma hapa, "TUNAPOFANYA MAAMUZI TUSIWE WABINAFSI" Ni na maana kama maamuzi yako yatamgusa mtu mwingine zaidi, inabidi kutafakari tena na tena kabla ya kuamua

    KUDOS kwa mama Gabby, Kafanya maamuzi mazito, si kwa sababu hajauona ukweli, Ila kaangalia pia madhara itakayopata familia yake, haswa mtoto mdogo asiye kuwa na hatia yeyote.
    Mara nyingi mifarakano ya wazazi ambayo mara nyingi sana inasababishwa na migogoro inayowezwa kutatulika inawahadhiri sana watoto.

    Labda tu nimpe ushauri wa bure baba Gabby. NJIA SAHIHI NA ILIYOSALAMA KUSHINDA VISHAWISHI, NI KUVIKIMBIA. NI VIGUMU SANA KUINGIA KATIKA VISHAWISHI NA KUVISHINDA. Haswa kwa mtu dhaifu kama yeye, kuona tu paja katoa namba ya simu.

    ReplyDelete
  7. Markus, ama kweli wewe ni MCHARUKO....LOL
    Wewe ndio wale ambao wakiona nyumba ya jirani inaungua wanapeleka Mafuta ya Petroli badala ya maji ili nyumba iteketee vizuri.

    Sijui ni kwa nini unamnanga baba Gabby kiasi hicho, au ungependa ndoa yao ivunjike? ili upate nini?
    au itakusaidia nini?

    Yaani kama kuna mtu anakutegemea kwa ushauri pale anapopambana na changamoto za maisha, nadhani atakuwa amekosea sana, wewe sio mtu sahihi wa kuombwa ushauri, maana ni rahisi kwako kumtumbukiza mtu shimoni, na kama ni wanandoa, naamini utakuwa ukichekelea kwa kijino pembe maana unajua kitakachotokea.....ndoa yao ni lazima itaota mbawa chini mwamvuli wako......LOL

    Kaka Godwin: nawe ingekuwa vyema kama ungesoma alichosema baba Gabby badala ya kumnanga bure baba wa watu......Namba ya simu ilitolewa kabla ya kuonyeshwa PAJA, RUDIA KUISOMA HIYO HABARI KWA MAKINI. kumbe ndio maana mmeshupalia kumnanga baba wa watu, kumbe hata hukusoma alichoeleza mwenzenu kwa makini, na kwa kuwa mlishamhukumu kabla hamkuwa na sababu ya kusoma alichoeleza between line.

    Baba Gabby kaonesha uwajibikaji kitu ambacho ni aghalabu sana kwa wanaume wengi kufanya. Alichokifanya, yatupasa kumpongeza na kumpa moyo na sio kumnanga, na kumsimanga.

    Tumuombee ndoa yake idumu.

    Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  8. Mimi nabadili topic, nawatakia krismas njema, hata kwa wale ambao hawaisheherekei kwa sababu mbalimbali au bila sababu yoyote

    ReplyDelete
  9. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 24, 2009 at 11:21 AM

    kwenyu NYOTE: SIMU YA MKONONI...!

    Bila shaka kwa wale walio hapa bongo wanajua kuwa kuna kipindi ama tamthilia iitwayo SIMU YA MKONONI na wanaoifuatilia wanajua jinsi hao majamaa wanavoonesha jinsi simu za kiganjani zinavoharibu mahusiano.

    Nakubaliana na Ba-Gabby juu ya kuufunga mjadala kwani pamwe naye tumejifunza kitu japo wengine wawili bado wana ushahidi wa kimazingira kuhusu jambo hili ambapo badala ya kumtuliza Ba-Gabby yanazidi (kwa mtizamo wangu) kumfanya awe guilt saidi na saidi.

    Anyway, kuna kisa kimoja kimetokea wikiendi hii hapo Mwanza ambacho kwa kutumia simu ya kiganjani mahusiano yamelegalega kwa maswahiba wawili (ambao husali msikiti mmoja wa Kirumba pindi mmojawapo awapo Mwanza).
    Jamaa alimwalika rafiki yake katika shughuli wikiendi ilopita ambapo jamaa huyu alipaswa kuwa MC. Wakati huohuo kulikuwa retreat ya mwaka ya kampuni moja kwa siku kama tatu katika viunga vya zizi hilo la kandoro. jamaa aliingia zizini hapo kwa usafiri ulomfikisha hapo usiku kiasi cha saa tano.

    Jamaa B anadai kuwa simu yake yenye line 2 aliiacha nyumbani kwa kuwa hakutaka kubugudhiwa na simu za binafsi na za kikazi wakati akiwa retreat hiyo ambayo rafiki yake pia alipaswa kuwapo lakini akaomba udhuru kuwa hatokuwapo.

    jamaa B akawa amekwenda kwenye retreat na jamaa A akawa anamtafuta kwa udi na uvumba. jumapili saa 3.32 asubuhi alipiga simu ikapokelwa na mke wa jamaa B. Badala ya kumwambia yeye ni nani na ana shida gani (namba aloitumia haiko kwenye simu ya jamaa), akawa anataka tu kuzungumza na mwenye simu na kumuuliza juu ya mahali alipo mume wa huyo mdada. Mdada aligoma kumwambia kwa kuwa alikuwa anazungumza kwa namna ya kufoka hivo jamaa akakata simu na baada ya sekunde moja akapiga tena na alipoambiwa kuwa ampigie amtakae katika namba za zain jamaa likakata simu. Mke wa mtu akakasirika akazima simu jumapili nzima.

    Unajua hasira pengine zilihamia kwa mjamaa mwenye mke kwani alipopigiwa na swahiba wake jana saa 1 akawa anakata simu na asubuhi ya leo maswali yakaanza kumiminika na pia la mwisho likiwa 'WEWE NI TAPELI LA KIHAYA'!

    Kwa hiyo jamani tutazame hizi simu...ni nzuri kama zikitumiwa vyema lakini zaweza kuua kama tusipoangalia matumizi yake.

    Ni hayo tu... nasikitika kwa kuwahubiria wakati UPADRE ulinishinda.....lol!

    ReplyDelete
  10. Unauhakika na unachokisema Koero. Kama ndio, basi hii hadidhi ulivyoiandika na kutufikishia si sawa na ulivyofikiria kabla ya kuiandika.(HAPA SIHITAJI KUWA KAJURA AU SHEIKH HUSSEIN KUJUA KUWA WEWE NDIO MTUNZI WA HADIDHI HII).

    Somo ulilotaka kulifikisha limefifihishwa sana na mazingira uliyo"SETIA". HAPAKUWA NA UWIANO KATI YA FANI NA MAUDHUI. ndio sababu kila mtu alisoma kwa jinsi alivyoona.

    KWA HILI NARUDIA NI VEMA TUKAKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA
    Kwangu itabaki kuendelea kuwa BABA GABBY SI MSAFI KAMA UNAVYOTAKA KUNI"KOMVISI"

    ReplyDelete
  11. Duh! Kaka Edwin, yamekuwa hayo tena....basi naacha.
    naona nimegeuziwa kibao.

    Hii mada imenishinda naomba kujitoa maana sasa nahusishwa na muandishi wa barua hiyo.....Kaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  12. kila njia inakona na wahenga walinena 'MAKOSA HUTAYARISHWA...LAKINI MAKOSA HAYAKUTAYARISHI WEWE.

    Koero ni bora umebaini LiMtupU liitwalo Markus siyo jitu Bora la kuombwa ushauri....Duh safi sana.

    Kimsingi naangalia chanzo cha tatizo kwanza, kisha najipelekeka katika suluhisho...LAKINI nadhani Baba Gaby kama siyo yeye, basi alisimuliwa na akaamua kuandika....LOl...Binafsi kuna mambo nimeshajiuhukumu ni mzembe...na nakiri yalinitokea kwa uzembe...

    Kama kweli kisa hiki kimeandikwa na Bbab Gabby nitamwambia ulisimuliwa....au ukampatia mtu akanakshi yaliyomo.

    NAMPONGEZA SANA MAMA Gabby, na namuombea busara zaidi. Nafahamu uzito wa kutengana na kuachana katika ndoa, nafikiri hakuna jambo bora kama kujadili matatizo yenu na utulivu ukarejea. Mama Gabby kila kitu kina gharama zake hapa duninai....kulinda ndoa kunahitaji umakini mkubwa... usichukulie ndoa kama fasihi simulizi ama sinema ya A TRIP TO THE MOON. Ndoa ni ajira kubwa kuliko zote ulimwenguni.

    Hata hivyo naamini ukiamini basi unafahamu yaliyomo. Leo utamboa ushauri kwa shosti wako, lakini unagundua ndiye aliyekusaliti, keshokutwa utaomba ushauri kwa mwingine utaona unahabarisha umma zaidi.

    Ndoa yako ni wewe, MINI KIMYWA CHAKO....huwezi kufundihwa ndoa kwa kulishwa kama kinda.

    Kwa msingi huo basi ziko falsafa USIOMBE USHAURI KATIKA WAKATI MGUMU. Amini kimywa chako. Ukitegemea ushauri wa limtu Markus utakuwa unajisumbua bureeee wakati naona kabisa CHANZO CHA TATIZO NI UZEMBE.

    KOERO NAOMBA TUKUBALIANE KUTOKUBALIANA KWA HILI.

    Simaanishi kumwunga mkono Godwini nataka ndoa ivunjike! simaanishi kuwa itanisaidia kitu. Nasema mtazamo wangu kwalo...labda kuna uhusiano wa Koero na hii stori mbali na maoni yetu....(rejea swali la dada Mija, katika stori ya mwanzo).
    sitawasikiliza baba gabby au huyo mdoli ulioomba lifti.

    Kwa maana nyingine nawatazama kama ile stori ya Shylock na Antonio katika Mabepari wa Venice................. mgoja nakunwa maji nina kiu sana............................................................ okey sasa, pole sana baba gabby, jambo hili hatujadili kwa nia ya kukukandamiza kama alivyosema kaka Chacha bali nadhani katika maoni yetu kuna jambo unajifunza.

    MPENDE MKEO, SIYO BIDHAA AU UKADHANI NI SAMBUSA, NAKUSHAURI PIA JARIBU KUVISOMA VITABU VYA MAREHEMU MUNGU TEHENAN gwiji la utambuzi.
    u make mistakes but mistakes dont make u.
    kaka Chacha amekwambia kuhusu simu ya mononi.....basi nakuongezea hii sinema ya Johan Strachan inaitwa Cellular.

    MFANYE MKEO AWE RAFIKYO WA KWANZA BABA GABBY utajiju wengine a.k.a MCHARUKO ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha LOl......

    ReplyDelete
  13. NIMERUDI TENA
    punde tu sikufahamu uko mtandaoni da Koero....
    unaweza ukapinga kuhusishwa kwako na hii habari, lakini ukiona mtu anakutaja anavigezo vyake ,,...labda tumwombe atwambie yaliyomo.

    USIJITOE TAFADHALI, TAFADHALI SANA NI MUHIMU WEWE KUWEPO KULIKO HAYA DA YASINTA KATIKA MJADALA HUU
    .... NA Godwin kangangu umeingia mawazoni mwangu kuhusu STTING ya hii habari na mkondo wa maoni ya da Koero ingawaje tunaambiwa mjadala umefundwa.

    kinachofanya uhusishwe Koero vipo vigezo na sababu. Lakini hongereni sana kwa KUFANIKISHA.

    ReplyDelete
  14. Godwin Habib Meghji said...
    "Unauhakika na unachokisema Koero. Kama ndio, basi hii hadidhi ulivyoiandika na kutufikishia si sawa na ulivyofikiria kabla ya kuiandika.(HAPA SIHITAJI KUWA KAJURA AU SHEIKH HUSSEIN KUJUA KUWA WEWE NDIO MTUNZI WA HADIDHI HII).

    Somo ulilotaka kulifikisha limefifihishwa sana na mazingira uliyo"SETIA". HAPAKUWA NA UWIANO KATI YA FANI NA MAUDHUI. ndio sababu kila mtu alisoma kwa jinsi alivyoona.

    KWA HILI NARUDIA NI VEMA TUKAKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA
    Kwangu itabaki kuendelea kuwa BABA GABBY SI MSAFI KAMA UNAVYOTAKA KUNI"KOMVISI" mwisho wa kunukuu:- Ndugu zanguni, au niseme kaka Godwin, hii mada Koero hahusiki KABISA katika uandishi na wala sio hadith baba Gabby yupo na pia amekuwa akiufutilia mjadala huu. Wala sio hadithi kuwa Koero au mimi tumetunga HAPANA. Nimeona ni vema niwaeleze ukweli ni hayo tu.

    ReplyDelete
  15. Ninanukuu Mija Shija Sayi said..."Katika kufunga mjadala, mwenyekiti wetu Da Yasinta unahitimisho gani? Maana hujatoa neno hadi wakati huu?" mwisho wa kunukuu:- Da mija mi nipo na nafuatilia mjadala. Nimefurahi kuona ndoa yao imefufuka tena na wana amani tena kwani unajua ndoa ikiwa haina amani wanaoumia zaidi ni watoto kama kuna watoto.

    ReplyDelete
  16. MWENYEKITI; ninahitaji sana mchanganuo wa hoja, katika kusema unatakiwa kufunga mjadla nadhani kuna uchambuzi wa kina au upembuzi yakinifu.
    Kwanini amefunga mjadala mapema hivi?

    tujadili mambo kwa kina bila upendeleo...tutazame mazingira halisi siyo kushabikia.......subiri.........nakunywa uji........ Oke ukitaka kujua mazingira yana nguvu gani katika maamuzi na ushauri someni THE CLASSIC kinachoelezea kesi na hukumu ya gwiji la falsafa Sacrotes.

    Nadhani mwenyekiti umefunga mjadala kwa kutoniridhisha....yesu nilapa naha sijaridhika na utongoaji wa fani na maudhui hapa.

    LAKINI...haya weeeeee kwaheri kwa leo, karibu MBEYA leo rahaaaaaaaaa sana xmass

    ReplyDelete