Friday, November 27, 2009

TAFAKARI YA LEO KWENU AU KWA PAMOJA!!!!


Wanaume wawili wamekaa na wanavua samaki.Na huku wakiwa na filosofia jinsi wanaume wanywavyo bia/pombe. Baada ya kukaa kwa masaa kadhaa John anamwambia Thomas:
"Mimi nadhani nataka kumwacha mke wangu. Mke wangu hajaongea nami kwa muda wa miezi miwili sasa"
Thomas amekaa kimya kwa muda huku akinywa bia yake kabla hajamjibu john:- Na baadaye akamjibu:- "Mimi ninakushauri jaribu kufikiri kwa makini zaidi. Wanawake wa aina hii ni ngumu sana kuwapata.!!!!!!!

13 comments:

  1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!November 27, 2009 at 9:24 AM

    mh! hapo patamu....lol

    Kama ni mimi anafunga virago na sintosikiliza ushauri wa namna hiyo...lol

    lakini hujatwambia kwa nini alinyamaa bila kuzoza...je ni kwa vile alinyimwa ama alikuwa anafanya meditation?

    cheers with ugimbi kwa wingi ...lol TGIF

    ReplyDelete
  2. nafikiri nimelewa bia wanayokunywa au homa ya weekend. Sijaupta vizuri ujumbe wa picha na hayo mazungumzo, maana nawaona wamekaa kwenye kisiwa cha barafu

    ReplyDelete
  3. Mwanamke anayekaa kimya ndani ya nyumba anapunguza makelele, ndio maana jamaa akamwambia ni wagumu sana kuwapata
    Akimwacha huyo atampata anayeongea kama chirik(kuna mtu humu pia yuko hivyo lol)

    ReplyDelete
  4. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!November 27, 2009 at 2:36 PM

    Nadhani hapo tunarudi kule kuleeeeeeeee!!!!!

    stay tuned...lol

    ReplyDelete
  5. Tafsiri yangu :

    Ujumbe una maana kuwa kuna WANAUME wengi hufikiria kuwa wanawake zao hawaishiwi maneno yakerayo a.k.a KULOLOMA .:-(

    Yani kila muda kuna jambo wanataka liongelewe AU WASIKILIZWE mpaka hata kuangalia mpira kwenye TV kidume unaweza kuzinguka kwa kustukia vilawama vinaendelea au kuhisi unamtenga demu ambaye wakati huo angependa umshike mkono muangali The Oprah Winfrey SHOW .

    Kwa hiyo aliyeko kwenye uhusiano wahivyo hupenda mwanamke afungaye bakuli mpaka asemeshwe. Na ambaye ukitaka msosi ghafla uwe wa mezani au wa chumbani jibu ni NDIO BABA WATOTO na sio kwa hilo muanze kujadili mpaka shopingi za kesho:-(

    ReplyDelete
  6. umegusia bia, mie sitaki kuongelea kitu hapa nimezira leo

    ReplyDelete
  7. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!November 27, 2009 at 3:05 PM

    Mt. simon, bravo....lol

    bado nasubiri kusikia saidi ya hapo...lol

    ReplyDelete
  8. bennet:-(

    sikujua kama kuna kasuku humu bloguni. labda yasinta ngonyani atuambie ni nani huyo?

    ReplyDelete
  9. Unacholalamikia bila shaka wengine wanakihitaji. Sio kila kwako baya ni baya kwa mwenzio, asiombe kupata mwanamke mwenyegubu. Basi na mungu amuwezeshe kuchukua ushauri wa rafikie

    ReplyDelete
  10. LOL ...
    @ Simon...DUH! eti NDIO BABA WATOTO??? Naona tutaanza ugomvi hapa ... hamna tatizo na kujadiliana shopping ya Krismasi!!

    ReplyDelete