Sunday, November 15, 2009

NI JUMAPILI/DOMINIKA YA 33 YA MWAKA B

Sala ya baba yetu
Basi nanyi salini hivi:-

KISWAHILI
Baba yetu uliye Mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,hapa duniani kama huko Mbinguni.
Utupe leo riziki yetu,
Utusemehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.
(Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele Amina)

Mt. 6, 9-13

DADI WITU

Hinu nyenye pemwisali, msala naha:-
CHINGINI/KINGONI
Dadi witu,
Witama kunani kulihundi,
Lihina laku lihyuwanike,
Ubambu waku utibwerele,
Chewifuna wenga vakiti vandu,
pamlima apa ngati chevikia kunani kulihundi,
Utiletele lelu chakulya chitu cha magono goha,
Utiwusile getihokili,
ngati tete tukuwawonela lipyana vevahoki kwa tete.
Ukotoka kutileka kulemala nichihaki,
nambu utiwusile vihaki.
(Ndava ubambu waveve na makakala na uvaha, magono gaha. Pepayi)
Mt. 6, 9-13.

DOMINIKA YABWINA KWA WOHA/JUMAPILI NJEMA KWA WOTE.!!!!!!!!!!

7 comments:

  1. Usinisome KATIKA SALA kama weye ni bingwa wa kukwazika na imani yako haikuruhusu kufikiri kwanini sala ni imani kwa kuwa sala nyingi ukizifikiria ni kama vile wasalio wanafikiri MUNGU MJINGA kwa kuwa kama MUNGU NDIYE ajuaye vyote labda haihitajiki kumuomba akusaidie uvumilie kunitukana au tu kukusaidi usitamani MAMBO MENGINE kuonjea sehemu za siri.


    Sala ya Dada yasinta , Mtakatifu SIMON KITURURU REMIX:


    Baba yetu uliye Mbinguni,
    KWANINI Jina lako litukuzwe,
    Na kwanini Ufalme wako uje wakati tunaambiwa wewe ni MFALME,

    Huhisi ni UBINAFSI kama ni kweli mpaka siye walala HOI Mapenzi yako tuyatimize,hapa duniani kama huko Mbinguni kwako ambako hatukujui?

    Na hakiyanani kwa jinsi tuhangaikavyo kweli unahitaji tukuombe Utupe leo ridhiki yetu na
    utusemehe madeni yetu, HATA KAMA sisi nasi hatuwasamehei wadeni wetu KWA KUKUIGA wewe kwakuwa TWASIKIA unampango wa baadhi yetu kutotusamehe ili utuchome JEHANAMU.

    Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu unafikiri kwa binadamu uliowapa akili inaeleweka?


    (NA kwa kuwa ufalme ni wako , na pia nguvu, na utukufu, basi LABDA UAMUZI PIA NI WAKO milele Amina)


    Kama umenisoma na kukwazika kuniombea kama weye unafikiri ndio huna dhambi na kwako RUKSA kunipiga jiwe , KUNIPIGA JIWE RUKSA. Au kama hutaki kupiga jiwe kuombeana ruksa na kama unaomba niombee pia na swala langu lakutaka kumpa mimba mtu!.

    SAMAHANI KWA KUKUKWAZA MHESHIMIWA ambaye kwakukwazika KIBONGE.:-(

    ReplyDelete
  2. Simon haya mawazo yako kweli ni makali na ukiangalia yana ukweli, kwenye historia tunaambiwa kwamba dini ilikuja ili kutufanya tuwe wajinga na rahisi kutawaliwa yaani tukubali kila jambo tutaloambiwa

    ReplyDelete
  3. Mtakatifu Simon Kitururu sijui kama kuna jipya ulilotoa...soma Biblia uone mwenyewe. Anza na kitabu cha Waroma (esp.1:18"Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wa wanadamu ambao kwa uovu wao wanauficha ukweli usijulikane.").

    ReplyDelete
  4. ulivyosema anonimas ni sawasawa kabisa kwani hivyo ndivyo tulivyofundishwa isipokuwa hatukufundishwa kuwa wadadisi kama mtakatifu kitururu. yaani tuliambiwa religion is a dogmatic thing: believe it as it is. usiulize, usidadisi, usiuliza maswali, ogopa kufa na vitu kama hivyo.

    niliwahi kusikia mapandri wa wakoloni walitumia vitubio vya waumini kubaini wakorofi na kuwaripoti kwa gavanana kesho yake walikamatwa na kutiwa rumande.

    ReplyDelete
  5. Naungana na Mube kusema yangu macho: Kwa ujumla dominika yangu iilikuwa nzuri ingawa nilikuwa sina raha sana. Na nina hakika wengine wote mmekuwa na dominika njema.

    ReplyDelete