Thursday, October 8, 2009

MTOTO AJIFUNGUA MTOTO MWENZIE!!!!!

Mtoto huyo ana miaka kumi na ana mtoto
Dunia hii sasa ni hatari kweli. Mtu na akili zake kabisa anathubutu kumfanyia unyama mtoto wa mwenzie. Kiasi cha kumpa mimba na kuzaa mtoto mapema. Kabla ya wakati wake wa kuzaa haujafika. Inaonekana huku tunakoelekea sasa ni hatari tupu au ni kweli labda ni mwisho wa dunia.

5 comments:

  1. Unaweza kubisha ya kuwa habari hiyo si ya kweli, lakini... Dunia hii ina mambo.
    Mimi mama kijana zaidi niliyepata kumuona alikuwa na miaka 13, sasa huyu duh!

    ReplyDelete
  2. Watu wanarekebisha mpaka vifaranga, huu sasa uchuro maana jamaa hapa alibaka kabisa
    Vyanzo vya mimba za utotoni ni umasikini uliokithiri mpaka mabinti wadogo kushawishiwa na hawa wakware wasio na utu kabisa

    ReplyDelete
  3. hii ilitokea kenya miaka kama miwili ama mitatu iliyopita. sina uhakika kama hamna 'kachumvi' katika umri wa dogo huyo ingawaje sibishi. alijifungua kwa 'siza' (cesarean).

    ReplyDelete
  4. Mkishangaa ya nairobari mtaona ya musoma. Huku mtoto mwenye umri wa miaka 10 hapa musoma aliwahi kuzaa a.k.a. kujifungua ntoto.

    YN, yawezekana aliyefanya hizo alikuwa ni mtoto mwenzie na si lazima awe ntu nzima...lol!

    Ama ilikuwa bahati mbaya kuwa walimdhania ni binti akapewa huyo mama mtoto awe analala naye chumba kimoja kumbe ya kiume ndo inachaji na ....lol! Ishatokea Bunda Mara huku kwetu kwa hiyo haya ndo maisha ya uswazi...lol!

    ReplyDelete
  5. Nilipoona hii picha nilishikwa na butwaa kubwa sana sikutegemea kabisa. Ina sikitisha na inauma sana kuona dunia hii ipo hivi. Tulio wazazi roho zinauma kweli.

    Asanteni kw mchango wenu. nadhani wote tumejifunza kitu hapa

    ReplyDelete