Tuesday, October 20, 2009

KWA NINI TUNAWAPA WATOTO WETU MAJINA KAMA HAYA????

Ni juzi tu nilikuwa naongea na rafiki mmoja kuhusu majina. Nimeona niandike machache na tujadili kwa pamoja:-

Majina yenyewe ni kama haya:- Matokeo, Maneno, Sikujua, Zawadi, Mashaka, Matatizo, Asante, Baraka, Wasiwasi, Sikudhani, Shida, Huzuni, Halimoja, Majuto, Bahati, Mapambano, Tuombe, Maombi, Tumaini, Masikitiko, Maua nk.
Na huku kwetu kusini yaani Songea (wangoni) wanawaita watoto majina kama haya wa kike Kachiki na wa kiume Kadoda. Maana ya majina haya angalia kwenye kamusi ya kingoni:-)

20 comments:

  1. Afadhali kidogo majina ya kwetu, ukienda kwenye baadhi ya nchi za Asia ya kati, maana ya majina yao kama ukiweza kutafsiri, du yanatisha. Sababu kubwa ya kuwapa majina mabaya , ati mashetani watayachukia hayo majina kwa hiyo hawawezi kuwaingilia watu hao. Kule mtu kuitwa Bichwa, Mbwakoko, Mauti, Kikojozi nk ni kawaida. We utasikia mtu anaitwa Maung..., uliza tafsiri yake, he heeeeee

    ReplyDelete
  2. Wacha nirejee maoni ya mtu kwenye post yangu moja iliyofanana na hii.

    Yasinta Ngonyani said...
    inawezakana kwani ninakotoka mimi mtoto akilia sana hasa usiku eti analilia jina kwa hiyo wanamshikia kuku na kutaja majina yote ya mababu na mabibi waliokufa. Akinyamaza katika jina lile walilotaja basi ataitwa hivyo. Na pia hii mtoto kuitwa matatizo, huzuni, shida hutokea mara nyingi kama wazazi/familia wamepatwa na jambo la kusikitisha kabla ya mtoto kuzaliwa.

    hizi ni fikra zangu

    Maoni haya yalitolewa kwenye post iliyobandikwa tarehe 24 Nov 2008. Ikumbuke kwa kuisoma hapa
    http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/11/ni-kweli-majina-yetu-huathiri.html

    ReplyDelete
  3. hakika jibu kwa nini tunawapa watoto majina kama haya sina, ila naamini wakati mwingi majina yanaathiri mwenendo mzima wa mtoto husika.

    ReplyDelete
  4. Majina kama hayo nadhani hayafai. Mi siyapendi na kila kitu.
    Nimerudi wajameni.

    ReplyDelete
  5. Unachakuandika..funga blog

    ReplyDelete
  6. Chochote awezacho kuitika mtu ni JINA!

    Na kwa kuwa chochote chaweza kumkasirisha mtu , ni TUSI!

    Na jamii zote zina majina ya ajabu kwa kuwa kitu chaa ajabu hutofautiana kutoka mtu na mtu , jamii na jamii!

    Kuna waliokuwa wanamshangaa jina Rais Bush na hawajiulizi KIKWETE maana yake nini!:-(

    ReplyDelete
  7. Dada Yasinta, nafikiri kupeana majina kunaenda na utamaduni unaomithilisha mantiki kulingana na mazingira/maana/tukio n.k. Kusema jina fulani ni baya/ lina mkosi n.k nako kunaendana na tasfiri inayojengwa na utamaduni vile vile. majina haya si mabaya kwa vile yanaonesha tamaduni..ubaya unakuja pale tunapotafsiri kwa upande hasi tu.

    ReplyDelete
  8. jina upewalo hata kama halina maana kwa mwenzio laweza kuwa na maana halisi katika maisha yako ya kila siku...lol!


    Ukiitwa shida yawekana ukawa na shida ama ukwa shida hata kwa mkeo/mumeo...lol

    ReplyDelete
  9. F. Mtanga majina mengine mboni mazuri tu hapo juu.

    nadhani ni vema kuwapa watoto majina mazuri ama yenye kuashiria mambo mema. sidhani kama ni vema kumpa mtoto majina kama ya kizaramo ya havintishi, chuki, siwema n. eti kwa kuweka kumbukumbu ya tukio fulani. afanaleki! hivi mtoto wako ndio awe kumbukumbu ya mambo mabaya!

    pamoja na yote majina nisiyoyapenda sana ni haya yafuatayo kwa kuwa hayaonyeshi utamaduni wa kiafrika:

    John
    simon
    yasinta
    yakobo
    emmanuel
    james
    julius

    nk

    ninayoyapenda ni kama
    alinanuswe
    kadoda
    muberwa
    chacha
    ghati
    tulijako
    nisajile
    ndimbuni
    babeiya
    nk

    ReplyDelete
  10. Mwaipopo mbona nawe unalo usolipenda na unalolipenda?...lol

    kwa hiyo wewe ni vuguvugu?...lol

    ReplyDelete
  11. Hahahaha,umenikumbusha kadoda! kuna kaka mmoja mngoni tulikuwa tunamtania sana na hilo jina lake.

    ReplyDelete
  12. eti twambie nini maana ya yasinta!!!!!!!!

    naitwa Lutatinabigambobyabantukyomakyamukulanyondoetelaamabelelusindurankonge

    na ninajua maana yake hilo

    bora kuitwa mkosi na ukajua maanayake kuliko kuitwa majina ya wanaoaminika kuwa ni watakatifu ulimwenguni eti kwa kuwa walikubaka kiroho

    ReplyDelete
  13. Hahahahaaaaaaaaa
    Nimependa jina la Kamala. Yaani jina linaandikwa kwenye passport kisha unaambiwa "p.t.o" ili kumalizia ukurasa wa pili.
    Hahahahaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  14. Yasinta, kwa nini usitafute jina lingine je tukubatize?...lol

    ReplyDelete
  15. Ni furaha kuona maoni yanye mitazamo tofauti. Lakini ngoja niseme hivi mimi sijapanga kubadili jina na wala kubatizwa tena kwa mara ya pili. Kwanza nalipenda sana jina langu Kaka John wewe kama hulipenda sio mbaya lakini muhusika nalipenda sana tena sana tu. Na pia ni jina TAKATIFU sana nadhani wote mnakumbuka wale watoto watatu wa FATIMA. Jina langu halina maana mahimu zaidi ya Yasinta ni jina.

    ReplyDelete
  16. Na hapa je?

    Masangu Matondo Nzuzullima Balya Malugu

    ReplyDelete
  17. Kaka! "Masangu Matondo Nzuzullima Balya Malugu" Je na jina lako hili ndefu lina maana gani?

    ReplyDelete
  18. natamani ningekuwa na jina lenye mahadhi ya matondo nzuzulima

    ReplyDelete
  19. natamani ningekuwa na jina lenye mahadhi ya matondo nzuzulima

    ReplyDelete
  20. Mimi naunga mkono kwamba sio lazima kubatizwa kwa mara ya pili.Binafsi naona muhimu kuwa na jina lenye maana fulani,tusijali lugha mama. Kwetu sisi tuna majina ya utoto/kifamilia typical kwa Wangoni (wakina Nakomba hao): Kadebedebe; Kadoda (mdogo wangu) na Kadala...sister wetu mpendwa wamwisho.

    ReplyDelete