Thursday, September 10, 2009

LEO NI MAZISHI YA BABY D

Ndiyo tunakubali kuwa Mungu alitoa na Mungu anachukua lakini inapokuja kwa mtoto huwa inaumiza kidogo nahasa mtoto huyo hata hajaishi kama inavyotakiwa. Na pengine hata hajabebwa na waliompenda. Mtoto D amekuwa katika dunia hii kwa muda wa siku 18 tu. Naomba wote tuchukua angalao dakika na tumwombe mtoto D. Mama, baba, wajomba, shangazi na ndugu wote watakuwa wanakukumbuka kila siku, ustarehe kwa amani peponi. Amina. Zaidi soma hapa. http://changamotoyetu.blogspot.com/ mada aliyoandika jumapili 6/9 na mada yenye kichwa cha habari Rest in peace baby D.

3 comments:

  1. Poleni sana Wafiwa!
    Na kweli inauma sana kuondokewa na mumpendaye!:-(


    Lakini ya Mungu tumuachie Mungu!



    Kwa imani zangu binafsi naamini mtu hufariki dakika Mungu aliyoamua au muda tu iliobidi afariki kwa hiyo ni vigumu kwangu kukubaliana na Yasinta kuwa Marehemu hakuishi ilivyotakiwa.

    Na mimi binafsi nikifariki na Kama ni kweli kuna peponi na ni kuzuri kama inavyodhaniwa, Nisingependa nilazwe huko peponi.

    Ningependa niishi macho na nisilazwe mahali popote nikiwa huko peponi hasa kama ni kweli hakuna kuchoka na mambo ni mswano huko.


    Samahani kama kwa komenti hii kuna mtu nimemkwaza!

    ReplyDelete
  2. Pumzika kwa amani mtoto D. Poleni sana wafiwa yaani kuishi siku kumi na nane tu ni uchungu sana.

    ReplyDelete