Saturday, August 29, 2009

UGONJWA WA MIGOMBA WAVAMIA AFRIKA

Ugonjwa wa ndizi waikumba Afrika

Wataalam wa masuala ya chakula wameieleza BBC kwamba upatikanaji wa chakula utakuwa hatarini barani Afrika baada ya kuzuka magonjwa yanayoshambulia migomba na kuathiri ndizi.
Mazao hayo yameathirika kuanzia Angola hadi Uganda, ikiwemo maeneo mengi ambapo ndizi ndio chakula kikuu.

Wataalam wamewashauri wakulima kutumia dawa za kuangamiza wadudu au kubadilisha aina ya migomba na kupanda ile inayoweza kukabiliana na magonjwa.
Wanasayansi wamekuwa wakikutana nchini Tanzania kuamua namna ya kupambana na m

Nchi zinazolima ndizi kwa wingi ni Ethiopia, Uganda, Rwanda, Kenya, Tanzania, Gabon, DR Congo, Jamhuri ya Congo , Kaskazini mwa Angola na kati mwa Malawi

Imeandikwa na mwandishi wa BBC.

7 comments:

  1. Mungu ainusuru TZ inatakiwa serikali ichukue hatua haraka kabla haujaingia ugonjwa huu TZ au sivyo watu watafuka njaa, kila siku na miaka ikienda ndio kila aina ya magonjwa yanazidi.

    ReplyDelete
  2. Ohoooo sasa Wachagga na wahaya itakuwaje? NI vizuri hatua za haraka zichukuliwe kunusuru kabla ya kuenea

    ReplyDelete
  3. Mamaaaaaaa!! Da Yasinta, hivi blogu yako inafika kwa bibi kule Bugabo?
    Kama haifiki nimtumie text aandae majivu ya kuua vijidudu.
    Ngoja ntamuuliza Kaka Bennet anipe ushauri wa nini cha kufanya
    Asante kwa taarifa

    ReplyDelete
  4. Hii nimeichukua kwa kaka Bennet kwa kirufu zaidi ingia hapa http://mitiki.blogspot.com

    MAGONJWA
    Ugonjwa wa hatari sana ulioingia hivi karibuni katika wilaya ya Muleba na maeneo mengine mkoani Kagera kutoka nchi jirani ya Uganda ni wa Mnyauko wa migomba unaosababishwa na bakteria (Banana Bacterial Wilt). Magonjwa mengine yanayosumbua zao hili ni Kuoza tunguu, Ugonjwa wa panama, Ugonjwa wa majivu nchani mwa tunda, Sigatoka, na Moko.

    WADUDU WAHARIBIFU
    Wadudu wanaosumbua zaidi hili ni Minyoo fundo (Banana nematodes), na Vifukuzi (Banana weevils).

    UDHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
    Magonjwa na wadudu hawa huweza kuepukwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hili. kama usafi wa shamba na kuchagua chipukizi bora. Au kupanda miche iliyozalishwa kwa chupa (Tissue culture banana seedlings) Hata hivyo mara mataizo haya yakitokea muone mtaalam wa kilimo aliye karibu ili aweze kukupa ushauri wa dalili za ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaosababishwa na bakteria

    ReplyDelete
  5. kuma mdudu anaitwa banana root borer kama jina linavyojieleza yeye hushambulia mizizi ya migomba, matumizi ya madawa inakuwa ngumu kidogo kwa wale wanaolima mabondeni maana utaua na viumbe wa kwenye maji, njia ya uhakika ni kumwagia migomba na maji ya moto tatizo njia hii ni ngumu sana labda kama una migomba michache

    ReplyDelete
  6. Ugonjwa unaouongelea hapa ni huu wa mnyauko wa migomba (rejea makala yangu) ambao husambazwa na bakteria aina ya xanthomonas, kwa Afrika mashariki utafiti unafanyika Arusha katika kituo cha utafiti wa madawa ya kilimo IITA (international institute of tropical Agriculture) ugonjwa huu huweza kuathiri kiasi cha asilimia 60% ya migomba shambani

    Kusambaa kwake ni karibu kwa njia zote yaani upepo, wadudu, vifaa vya shambani, mbegu n.k

    Njia ya kienyeji kukabiliana na ugonjwa huu ni kutumia pilipili au pilipili manga ambapo zinasagwa na maji, kuchujwa na kupuliziwa shambani

    ReplyDelete