Monday, August 10, 2009

SABABU NYINGINE ZA KUZINI ZA AJABU EH!

Leo nimeona tuanze wiki hii kwa kujua sababu hizi haya ebu soma hapa.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa zinazosababisha wanandoa kutoka nje ya ndoa, miongoni mwa sababu hizo nyingine ni kichekesho kabisa.
Inasemekana ni rahisi sana kujua kama mwenzako anatoka nje ya ndoa au la, na hiyo inafanyika kwa kuangalia dalili au mabadiliko fulani kutoka kwa mwenzako na kwa kuzingatia tabia yake ya awali uliyoizoea ni rahisi kugundua kuwa kuna jambo ambalo sio la kawaida linaendelea.

Kuna sababu nyingi zinatajwa kusababisha baadhi ya wanandoa kutoka nje ya ndoa.
Inasemekana kwamba sababu mojawapo kubwa ni kutokana na wanandoa kutokuwa karibu kama zamani walipokuwa ndio wameoana, ule moto wa awali unatoweka au kufifia kabisa, kama ni mume au mke anahisi kuchokwa na mwenzake, na hapo kuna uwezekano mkubwa akatafuta faraja kwingine.

Utakuta mume au mke anatoka nje kujaribu kutafuta anayedhani atautuliza mzuka wake wa mapenzi.
Lakini inasemwa pia kuwa kuna wengine hutoka nje ili kuonesha kuwa nao wanaweza, kuna baadhi ya watu kutongoza na kukubaliwa au kutongozwa na kukubali huchukuliwa kama kipimo cha kuonesha kwamba mtu anapendwa au anamudu.

Kuna wengine kutongoza na kukubaliwa huchukuliwa kama mashindano, yaani mwanaume kuwa na idadi ya wanawake wengi aliotembea nao nje ya ndoa huchukuliwa kama jambo la kifahari hakuna mfano.
Kuna wale ambao hawahisi kupendwa ndani ya ndoa zao, nao hulazimika hutoka nje ya ndoa ili kuthibitisha kwamba nao wanapendwa.

Sababu nyingine inayotajwa ni ile ya kisasi, unaweza kukuta mwandoa mwanamke au mwanaume anaamua kutoka nje ili kulipiza kisasi au kumkomoa mwenzake. Tena inawezekana jambo lenyewe likawa ni dogo ajabu lakini ili kuonesha ubabe mwanandoa anaamua kutoka nje ya ndoa ili kumkomoa mwenzake. Kwa mfano mke kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara au mume kushindwa kumtimizia mke mahitaji kama vile mavazi au vitu vya urembo, hiyo inaweza ikawa sababu tosha kabisa ya mwanandoa kusaliti ndoa yake kwa kigezo cha kumkomoa mwenzake. Mara nyingi kutoka nje ya ndoa kwa sababu hizi kuna madhara makubwa kwa muhusika

Kuna wale wanaume ambao umri umeenda, hawa nao hudiriki kutembea na vibinti vidogo vya kuwazaa ili kuthibitisha kwamba bado hawajazeeka na wanamudu kufanya tendo, hata wanawake vile vile wenye umri mkubwa pia nao wamo kwenye mkumbo huo wa kutembea na vijana wadogo, wenyewe huwaita Serengeti Boys, wakimaanisha ile timu ya soka ya vijana wa chini ya umri wa miaka 18.

Sababu za wandoa kutoka nje ni nyingi tena nyingine ni za kijinga kabisa, lakini je tunajua madhara tunayopata au tutakayopata kwa ujinga huu?
Ni kitu gani hasa tutakachofaidi kwa kutoka kwetu nje zaidi ya maumivu au hata kuvunjika kwa ndoa?

Siku hizi maradhi ya zinaa ni mengi mno achilia mbali ukimwi unaopigiwa kelele kila uchao katika vyombo vya habari. Takwimu za ugonjwa huo barani afrika zinatisha, lakini mtu yuko radhi kutoka nje ili kumkomoa mwenzake au kuonesha kwamba na yeye anaweza.

Ni vyema kama mwanandoa anahisi kama upendo wa mwenzake umepungua kutafuta suluhu, kwani kujadiliana kwa upendo ili kupata suluhu ni jambo la msingi kabisa ili kurejesha moto wa awali kama unahisi umepungua. Inashauriwa majadiliano hayo yafanyike kwa uwazi na katika njia ya kujenga, na ule upande wenye matatizo, ukubali kurejea katika mstari ili kurejesha amani nyumbani.

Si vizuri kutupiana lawama, hiyo haitasaidia kuleta maelewano, bali inashauriwa kila upande kubeba jukumu lake kwa mustakabali wa ustawi wa ndoa husika.

9 comments:

  1. Wananchi wenzangu, mmeyasikia hayo?

    ReplyDelete
  2. Nitanukuu.....

    "Kuna wengine kutongoza na kukubaliwa huchukuliwa kama mashindano, yaani mwanaume kuwa na idadi ya wanawake wengi aliotembea nao nje ya ndoa huchukuliwa kama jambo la kifahari hakuna mfano.
    Kuna wale ambao hawahisi kupendwa ndani ya ndoa zao, nao hulazimika hutoka nje ya ndoa ili kuthibitisha kwamba nao wanapendwa"

    Dada hapo umenena, kuna binamu yangu mumewe alizaa na House Girl kisa anachelewa kurudi kazini kutokana na majukumu, mume ni mfanyabiahsra na mara nyingi huwa nyumbani kwani ameajiri vijana wanamfanyia kazi na mke ni muajiriwa Sekta Binafsi.....Kaaazi kweli kweli.....

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kuwasilisha hoja.Yasinta na wewe??!!!!

    ReplyDelete
  4. Hili tatizo lipo sana katika kila jamii,bila kujali rangi wala dini kwa sisi waafrika,wanaume wengi sana wamekuwa wakizaa na hawa wasaidizi wa ndani,hii mimi inaniumiza sana kama Koero alivyosema,hivi hawa wanaume wanajua kweli thamani ya mwanamke na mtoto?nasema hivyo kwasababu hawa mabinti wengi wamekuwa wakinyanyasika kwa mababa wenye nyumba binti akimkataa anatishiwa kufukuzwa kazi,akipata mimba anafukuzwa kazi yeye na mimba yake,nini hatma ya mwanamke huyu na mtoto wake jamani ataishi vipi?????

    Kichekesho sasa kwa hawa wenzetu weupe,wao sasa ni mchanganyiko mwanaume anaweza kutembea na ndugu wote wa nyumba moja,tena hata mama mkwe wake asipokuwa makini nae atachanganywa,hapo huwa sielewi ni tamaa tu ya mwili au nikaugonjwa kanahitaji tiba?Kaka zetu tuelezeni jamani.

    ReplyDelete
  5. unapokosa kujua your suprime reality, mojawapo ya matokeo yaweza kuwa kama hayo.

    ila labda nadhani ngono ni tamu sana ehe? eti muifanyapo huwa mnajisikiaje?

    ReplyDelete
  6. Hii maada ni ngumu sana, ni kweli wengine hotka nje kwa sababu hawaridhishwi na wenza wao, ila wengine hota nje kama kujaribu akidhani labda kuna cha zaidi.

    Cha muhimu ni kutafuta muda wa kutosha wa kukaa na mwenza wako na kama kuna mapungufu msiyafumbie macho muelezane kinaga ubaga ingawa wengine wakielezwa ukweli huwa balaa

    ReplyDelete
  7. The devil made me do it...Wengine husingizia maumbile. Tazama hapa:

    http://matondo.blogspot.com/2009/06/are-men-wired-to-cheat.html

    ReplyDelete
  8. Ahsanteni. Inasikitisha kuona hili jambo linazidi kuendelea siku baada ya siku. Nadhani mwisho itakuwa ngumu zaidi. Kwani inaonekana kama wanaume wao wanachotaka ni kujitosheleza tu. Na mwisho ni kumwacha yule mwanamke au msichana pekee. Huwa najiuliza kama wana huruma au wanadhani wao ni akina nani:-(

    ReplyDelete