Nimepata email kutoka kwa msomaji wa blog hii (ameomba nihifadhi jina lake) amenitumia taarifa ifuatayo ambayo imesikitisha sana, nami bila kusita kutokana na kuguswa na habari hiyo nimeona niiweke hapa kibarazani ili kuomba msaada kwa wadau walioko nyumbani Tanzania jijini Dar Es Salaam, wasaidie kumuokoa binti huyu. Naomba kuwasilisha.
Dada Yasinta,
Nimeshawishika kuwasiliana na wewe ili kujaribu kutafuta namna ya kumsaidia mtoto Fina ambaye ni yatima anayeishi katika mazingara ya mateso makubwa kupita kiasi.
Najua hunifahamu na wala sijawahi kuwasiliana na wewe hata siku moja lakini ningependa ufahamu kuwa mimi ni mmojawapo kati ya wasomaji wazuri wa blog yako.
Kwa kuwa nimeona kuwa blog yako inasomwa na wasomaji wengi nimeona nipitishie kilio cha binti huyu kupitia blog yako ili kutafuta namna ya kumsaidia.
Mimi naishi maeneo ya Tabata Kisukulu lakini ninaye girlfrind wangu anayeishi Tabata Kimanga jirani na mama huyo anayemtesa binti huyo yatima asiye na baba wala mama. Nimekuwa nikimtembelea Girlfrind wangu karibu kila siku na nimekuwa nikishuhudia mateso anayofanyiwa huyo binti
Nyumba anayoishi mama huyo iko Tabata Kimanga, unashuka kituo maarufu kiitwacho njia panda, mbele kidogo unafuata njia ya kushoto, utakuta gereji, ukiuliza kwa mama Enok au mama Frank maarufu kwa kuwauzia mafundi gereji maji ya baridi utampata.
Baada ya kuona mateso anayofanyiwa binti huyo, niliijaribu kuwauliza baadhi ya majirani na walikiri kuwa hilo ni jambo la kawaida, kwani binti amekuwa akipigwa kila siku takribani mara tatu kwa siku kwa makosa yasiyo na msingi kabisa.
Naamini wote tunafahamu malezi na namna ya kumuadhibu mtoto, lakini ikiwa mtoto anaadhibiwa hadi kuchomwa moto hiyo ni hatari, na tena kwa jinsi alivyo makini humchoma sehemu za mapajani ili isiwe rahisi kuonekana.
Nimefanya uchunguzi makini katika kipindi hiki cha mwishoni mwa juma na nimepata habari muhimu kadhaa ambazo mtu asipokuwa makini anaweza kudhani kuwa binti huyu haonewi. Huyu mama kwa kutaka kujenga mazingira ya kutoonekana kwamba anamtesa huyu binti, amekuwa akimsingizia mambo mengi kwa majirani na hata shuleni anaposoma ili ionekane kwamba ni mtoto jeuri, malaya na asiyesikia.
Ni mzuri kwa kutengeneza uongo na anaongea sana, ila naamini hata majirani watakuwa ni mashahidi wazuri katika kuthibitisha hili. Ni mateso makubwa sana anayopata binti huyu na hata kama ni mkosaji lakini adhabu anayopewa ni kubwa kuliko kawaida. Inaniuma sana na ninahisi si siku nyingi anaweza hata kumuua. naomba nikiri kwamba katika maisha yangu yote sijawahi kuona mateso ya namna hii, tena yanayofanywa na mwanamke ambaye na yeye anao watoto na anayejua uchungu wa kuzaa............ sasa nimejua ni nini maana ya roho mbaya tena mbaya zaidi naishuhudia kwa mwanamke.........
Nakuomba sana dada Yasinta uiweke habari hii katika blog yako ili jamii ya Watanzania na vyombo vinavyohusika vifahamu. Niliwasiliana na Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), na waliahidi kufuatilia swala hili.
Ukweli ni kwamba dada kila nimuonapo binti huyu roho inaniuma sana na nimeshindwa kuvumilia unyama huu. Naamini labda mungu anayo makusudi yake, kwamba nilione hili ili nichukue hatua, na hatua yenyewe ndio hii ya wewe kunisaidia kumuokoa mtoto huyu. Jamani dhamira inanishitaki na naona kuna kitu kinanisukuma nimsaidie binti huyu kama binadamu mwenzangu....
Nimefanya uchunguzi wa kujua shule anayosoma na jina la mwalimu mkuu na namba yake ya simu, na nimepata taarifa zifuatazo:
Jina la Binti ni Filimina (Jina la baba yake sijalipata bado)na anasoma darasa la Tatu C
Jina la shule ni Tumaini Tabata Kimanga
Jina la mwalimu mkuu ni Mwalimu Mang’enya
Namba ya simu ya mwalimu mkuu ni +255 718 900190
Naomba ushirikiano wako,

Jamani, nimesikitika sana sana kusoma habari hizi za binti mzuri kama uyu. ni kweli kuna watu apa duniani hawana huruma kabisa. Natumani watatokea wasamalia wema wenye uruma na uwezo wa kumsaidia uyu binti. Mungu ni muwezaji wa yote, uyu binti atafanikiwa tu. Ubarikiwe wewe kaka uliyeleta hii habari, tuombe Mungu ili uyu binti aweze kusaidiwa.
ReplyDeleteKUNA MAJITU BADO YANATESA WATOTO!
ReplyDeleteNashauri suala hilo lifikishwe kwa vyombo vya sheria
oooh jamani, ndio maana laana zinazidi kutuandama maana hata Yesu kwenye biblia alisema "Waacheni watoto wadogo waje kwangu...." Sasa watu wengine sijui wana roho gani,kwama vile wao si watoto waliozaliwa kama huyo?
ReplyDelete"Do not take advantage of a widow or an orphan.If you do and they cry out to me, I will certainly hear their cry. My anger will be aroused, and I will kill you with the sword; your wives will become widows and your children fatherless.
ReplyDelete(OXODUS 22-22:24)
kwa jinsi hii,tunaokelekea ni kubaya..
ReplyDeletewanadamu hawana imani tena.
Nakubaliana nanyi wote kuwa kuna watu katika dunia hii hawajui HURUMA ni nini. Nimeudhika sana na kitendo akifanyacho huyo mama afadhali hata angekuwa baba ambaye hajabeba mimba miezi tisa na kuzaa watoto. Huyu mama dawa yake iko jikoni. Na naamini kesha laaniwa na kama bado basi alaaniwe kabisa. natumanini kuna mtu/watu watamwokoa mtoto Filimina kwani hastahili kuishi maisha yenye mateso kiasi hiki. Ni kweli inabidi tulipeleke hili jambo kwenye vyombo vya shereia na lichukuliwa hatua tena hatua kali tu.
ReplyDeleteRoho inaniuma sana kwa kutofanya kitu wakati nataka kufanya kitu. Kumchoma mtoto mdogo moto na kumpiga kama unapigana na mtu mzima mwenzako. Kama huyo mama ana nguvu za kutosha achukue jembe na aende kulima madimba...Nikiwaangalia wanangu na nikisoma habari hii machozi yananitoka. Kama hampendi kwa nini asiseme kuliko kumtesa hivyo. Yaani huyu mama ....basi tu.