Thursday, August 27, 2009

JE, UPWEKE NI UGONJWA?

Kabla na baada ya kuja huku niliko nilikuwa na marafiki wengi kifani. Lakini baada ya kuishi mwaka mmoja hap nililetewa barua toka kwa marafiki zangu na kuniomba niwatafutie wachumba au kazi. Na nilipowajibu kuwa mimi nilikuwa mgeni, pia binafsi sikuwa na kazi wala sikujua lugha walikata mawasiliano nami.
Nikawa nashangaa kwa nini? je? hawa kweli walikuwa marafiki wa kweli yani wale ambao wanasema hufaana kwa penye furaha na taabu. Kwa hiyo nikabaki mpweke bila rafiki wa karibu isipokuwa nilikuwa na rafiki yangu wa karibu sana ambaye ni mume wangu na baadaye wanangu. Na baadaye yaani kama mwaka mmoja uliopita nilianza kublog na hapo nikapata marafiki wengi tena. Na natumaini ninyi rafiki nilowapata hamtanikimbia. Hii ndio sababu nimeuliza je? upweke ni ugonjwa? kwasababu mimi nilikosa sana raha nilipokuwa mpweke.

11 comments:

  1. Ni ugonjwa tena mbaya sana.Tiba yake nini? Labda "Socialization, partner,children,work,company"

    ReplyDelete
  2. Yabidi ufanye utafiti kujua ya kuwa wanablog wote waliopo hasa ya nyumbani, wameanzisha ili kuondokana na upweke au ni ....

    Ila watu wanafikiri wachumba wanapatikana kwa urahisi hivyo!! Touch ya kwako ni tofauti na ya kwao, pia watu wanatofautiana, huwezi kumtafutia mtu perfect kwake. Pole kwa maombi ya kila namna! Angalia tu wasijekukuomba uwaazime japo nyumba yenu!! :-(

    ReplyDelete
  3. Mlongo, Upweke ni ugonjwa mmbaya sana, kwakweli watu wengi wanaoishi Ulaya wanaugonjwa huu zaidi wazaliwa wa uko. wengine wanaweza uchanganyikiwa kabisa na kuishia kwenye hodi za vichaa, ndio mala kwa mala uku mtu anaweza kufa ndani peke yake na watu wakagundua baada ya miezi au miaka kuwa amekufa. umebarikiwa kwa kuwa na mume na watoto kwani hao ni marafiki wa milele. hayo ya nitafutie, nisaidie, bla bla bla ata mimi yalinipata ili ni tatizo la watu nyumbani kutokuelewa juu ya maisha ya uku, ata mimi mwenyewe sikuyajua mmpaka nilipofika uku na kujionea mwenyewe. Kazi njema mlongo.

    ReplyDelete
  4. Uku tuliko ni lahisi mtu kuwa mpweke ingawa unaweza kukutana na watu wa nyumbani mkajalibu kuwa marafiki lakini mala nyingi uleta matatizo na baadae wengi uamua kuwakimbia wenzao kwa kuogopa matatizo. na wengi wao uwa wanatembea na mambo mengi makubwa moyoni na wanaogopa kumwambia mtu mungine kwa kuogopa kusemwa vibaya, hii pia uleta upweke na ndio maana utakuta watu wengi wa kuja zaidi kutoka afrika wanaishia kwenye hodi za vichaa.kwasababu sio mila na desturi yetu kuwa wapweke uko nyumbani kuna wengi wa kuongea nao au wa kukushauri ki mila zetu.

    ReplyDelete
  5. wewe yasinta, hata mimi ni rafikiyo?

    usihofu, hata tukikukimbia, si utapata wengine tu? ulimwenguuna watu karibu bilioni saba sasa hofu ya nini?

    ReplyDelete
  6. hata mimi nilikuwa mpweke pia.....

    ReplyDelete
  7. UPWEKE wa marafiki ama upweke wa watu waliopo duniani? au uwe mpweke kwakuwa KAMALA kakukmbia katika urafiki??? Lol ha ha ha ha ipo kazi....lakini upweke ni tatizo la kisaikolojia na mara nyingi waliopo katika hali hiyo hawawezi kujisadia mpaka waambiwe UTAMBUZI NA KUJITAMBUA kuwa WEWE NI NANI?

    NANGOJEA WAGUEKE halafu na unacheka nao wala usijali kama huwajui

    ReplyDelete
  8. Ahsantena wote kwa kuongana nami katika mjadala huu wa upweke na kwa kufanya hivyo kwa kweli upweke huwa unapungua. unajisikia raha kuona jinsi mlivyo na ushirikiano mzuri. Ni hayo tu Ahsante tena.

    ReplyDelete
  9. Sijui kwa nini baada ya kusoma hiki KITITA naanza kujisikia mpweke na WAKATI nimezungukwa na kama MTU ishirini HIVI sasa hivi!:-(

    Unafikiri ni kweli bado kuna watu HUFIKIRI kuwa dawa ya upweke ni kuwa na watu?

    ReplyDelete
  10. Hey Yasinta wala si peke yako yanakukuta, mie mdau wako nipo hapa US! Nami nilikuwa na marafiki wengi back home nilipofika huku walikuwa wakitaka niwatafutie sponsors waingie vyuoni. Nilipowaambia kuwa si rahisi wote wananichunia hakuna anayetaka kuongea nami tena!!!!Jamani hata waliozaliwa huku kama hawana pesa hawaendi shule huku hakuna kujuana kama nyumbani.
    Mdau US

    ReplyDelete
  11. upweke in ugonjwa dadangu na wala hauko peke yako, inatokea mara nyingi sana, mshukuru Mungu weye una mume na watoto sasa wale waliokatika hali hii wasio na watu wakaribu ndio noma zaidi.
    lycka till!

    ReplyDelete