Thursday, July 9, 2009

JE UNATAFUTA FURAHA? SOMA HAPA

Picha na makala kutoka kwa kaka Shaban Kaluse



Natafuta furaha!


Wengi wetu hatuna furaha kabisa kwenye maisha yetu,
Hakuna kati yetu aneyejua ni kwa nini hatuna furaha. Nasema hakuna kati yetu , sisi ambao hatuna furaha kwa sababau, kama tungekuwa tunajuwa tusingeendea kubaki bila furaha.
Hatuna furaha kwa sababu hatujui kwamba furaha haiko huko nje kwenye vitu tuvionavyo na kuvisikia, bali tunayo wenyewe ndani mwetu. Ni suala la sisi kuamua kuichukuwa furaha hiyo pale tunapoweza na kuitumia.

Binadamu anatakiwa kuwa na furaha wakati wote, kwa sababu anayo mwenyewe furaha hiyo.
Ningependa kukuambia kwamba, kama kweli unapenda furaha, basi usijaribu kuthibiti hali halisi.

Hivi sasa nikiangalia, naona watu wengi wasio na furaha ni wale wanojaribu kushindana na hali halisi. Mawazo yao iwe wanajua au hawajui huwaambia kwamba wanaweza kuthibiti hali halisi.
Ukweli ni kwamba haiwezekani, hakuna anayeweza kudhibiti au kubadili hali halisi.
Kama mazingira yanabadilika na huwezi kuyadhibiti, unachotakiwa kufanya ni kukubaliana nayo, kukubali kusogea nayo pamoja, hiyo ndiyo siri ya kuyamudu, bila ya kujali yako kwenye sura gani.

Kujaribu kudhibiti jambo au kitu ambacho hatukiwezi, ni kujiumiza kiakili , kihisia na kimwili pia, ni kujinyima furaha.
Jambo muhimu zaidi ni mtu kujua kwamba, anachoweza kukidhibiti au kukibadili ni yeye mwenyewe, siyo kingine chochote kilicho nje yake.
Kuna kitu kimoja tu, ambacho mtu anaweza kukidhibiti hapa duniani, nacho ni yeye mwenyewe.
Huwezi kudhibiti hali ya hewa, hivyo kuumia mvua inaponyesha na biashara yako kushindwa kuuzika ni kuzidi kujiumiza bure.

Huwezi kudhibiti watoto, mkeo au mumeo, hivyo kukerwa na mambo yao ni kujiumiza zaidi tu.
Nje ya imani zako, mawazo yako, mitazamo na matendo yako, hakuna kingine unachoweza kukidhibiti.
Jaribu kujifunza namna utakavyoweza kudhibiti imani, mawazo, mitazamo na matendo yako ili visikupe maumivu.

Vile vyote vilivyo nje yako ambavyo huna uwezo wa kuvidhibiti, viache vitokee , visikusumbue. Ukimudu kufanya hivyo, hakika utaanza kuhisi tofauti.
Halafu fanya uamuzi kuhusu kile unachokitaka maishani mwako, kisha ung’ang’anie hapo. Ni vema mtu kuishi akiwa anajua anataka kitu gani hasa, anataka maisha yake yawe vipi hasa, kwani kubahatisha maisha huondoa sana furaha ya mtu. Bila kujua twendako maisha ni vurugu tupu.

Ni vema kuchagua kile ambacho mtu anpenda kukifanya bila kutoka nje.
Kumbuka kwamba mara nyingi hatuna furaha kwa sabau hatujawahi kuwafanya wengine wafurahi.

Tukishwafanya wengine wafurahi ni wazi na sisi tutakuwa kwenye furaha kubwa kuliko wao.
Ukitaka kuwa na furaha unapaswa kuwa na marafiki wenye kutia moyo na kufikiri kwa mkabala mzuri. Watu ambao wanaaminika na wenye hekima na busara wanapokuwa karibu na wewe, hakuna kitu chenye kufurahisha kama hicho.

Kuna mambo kama uimara wa ndoa au uhusiano na mpenzi. Kama unataka kuwa na furaha ya kwelini lazima uhakikishe kwamba umejitahidi na kujenga uhusiano mzuri na mke, mume au mpenzi wako. Juhudi hizi kwa sehemu kubwa ni lazima zitokane na wewe kumkubali mwenzio kama alivyo ili uweze kusaidiana naye karibu kwa kadiri inavowezekana.

Kuna mengi ambayo yanaweza kumsaidia mtu kuwana furaha ya kweli maishani, lakini yote hayo yanategemea mtu anvyojiona mwenyewe na alivyo tayari kukubaliana na yanayomtokea kila sekunde, dakika , saa na maisha yake yote.
Furaha ipo, ni suala la mtu kuichukuwa na kuitumia.

5 comments:

  1. Tukumbuke kuwa HUZUNI ni muhimu pia kwa binadamu kuwa binadamu.


    Na ipo furaha pia wapatayo watu kwa kujaribu kubadilika au kubadilisha kitu na sio kukubaliana nacho tu. Ndio maana jembe lilipomshinda mtu akagundua Trekta.

    Tukumbuke kuna watu huwa ni kweli kabisa hawajui wanataka nini na hiyo ndio hali halisi.

    Kama unabisha anzisha dini ya kuabudu hata mihogo leo uone kama hautapata wafuasi ambao furaha yao itakuwa ni kukufuata.

    Au kumbuka tu jinsi watu kibao enzi za form four walivyokuwa wanapata tabu kuchagua kombinesheni za High School kwa kuwa hawajui hata wanataka kufanya nini hapo baadaye.

    Mwisho kumbuka furaha unaweza kufurahishwa na mwenzio na hilo linaweza kumaanisha hakuna amilikiye furaha yake 100%

    Mengineyo katika makala sipingi.

    ReplyDelete
  2. Nimemaliza kusoma maoni ya Mtakatifu Simon na kusahau nilitaka kusema nini.
    Nakubaliana na mawazo yako da Yasinta. Furaha ni kitu muhimu sana. Lakini watu tunajisahau na kwenda kutafuta furaha mbali na kwa gharama kubwa.
    Hebu fikiria, mtu anahitilafiana na mkewe. Anawasha gari na kwenda kutafuta furaha huko mbali. Anatumia pesa na muda mwingi. Anaporudi nyumbani akidhani amepata furaha, anajikuta mambo bado hay'endi.
    Tuseme mtu akiwa na mafanikio maishani anadhani ndo ashapata kila kitu, hata furaha. Kumbe sivyo. Wenzetu wakaamua kusema, "Success doesn't bring happiness, but happiness is a key to success."
    Ni hayo tu mama Camilla.

    ReplyDelete
  3. Asanteni wote kwa maoni yenu. Ni kweli kabisa mliyosema. Nami nimenukuukipengere hihi. "Kuna mengi ambayo yanaweza kumsaidia mtu kuwana furaha ya kweli maishani, lakini yote hayo yanategemea mtu anvyojiona mwenyewe na alivyo tayari kukubaliana na yanayomtokea kila sekunde, dakika , saa na maisha yake yote.
    Furaha ipo, ni suala la mtu kuichukuwa na kuitumia."

    ReplyDelete
  4. Tie on to boost apprehension away from scoff cook with adipose greater destined for all hard-headed purposes [url=http://onlineviagrapill.com]buy viagra[/url]. Assess to endorse you cease-fire of cap of line that you are peppy [url=http://ambiendrug.com]ambien[/url]. Chin-wag large-hearted unhappiness veneration syndrome [url=http://virb.com/symbalta]flagyl[/url]

    ReplyDelete