Monday, June 15, 2009

TUNAWEZA KUBADILI/KUACHA KUPIGA WATOTO

Katika maongezi na Mzee wa changamoto tukaingia kwenye mada hii, yaani kuchapa watoto viboko. Yeye alisema haoni kosa kuchapa watoto viboko. Ndo nikapata wazo la kuandika mawili machache. Haya wasomaji tusaidiane.

Mnajua katika nchi nyingi dunianai wanaona si kitu cha ajabu kuchapi/kupiga watoto. Wanaona ni moja ya malezi. Kama Mzee wa C TUNAWEZA KUBADILI/KUACHA KUPIGA WATOTO
Jana nilikuwa naongea na Mzee wa Changamoto na baadaye katika maongezi tukaingia katika mada hii ya kuchapa watoto viboko. Yeye alisema haoni kosa kuchapa watoto viboko. Ndo nikapata wazo la kuandika mawili machache. Haya wasomaji tusaidiane.

Mnajua katika nchi nyingi dunianai wanaona si kitu cha ajabu kuchapi/kupiga watoto. Wanaona ni moja ya malezi. Kama Mzee wa changamoto anavyosema. Ila mimi ni kinyume na Mzee Changamoto pia watu wote wanaoona ni haki watoto wapigwe viboko.

Lakini tukumbuke kila mtoto ana haki ya malezi yenye usalama. Inabidi tukazane kwani mpaka sasa, yaani leo hii kuna nchi 24 tu ambazo ni marufuku kupiga watoto.

Nadhani karibu kila mtu anakumbuka jinsi tulivyopata viboko, yaani nyumbani pia shuleni. Ndugu zanguni wasomaji tujaribu kusaidiana kuzuia kuchapa/kupiga watoto kwani viboko sio dawa ya malezi. Jinsi mimi ninavyoona/fikiri mtoto akishazoea kupigwa viboko kila siku anakuwa sugu(hasikii) anaona kawaida tu na pia akili yake inadumaa. Najua ni jambo (somo) ambalo wengi hawatakubaliana nalo lakini ni LAZIMA tuanze. Tuache kupiga watoto nyumbani na pia shuleni. Wazazi wawe huru kwa malezi ya watoto wao wakati wote na pia wawe na haki sio kuwapiga piga.
Sio kufuata sheria tu pia wazazi na walimu wanaweza kusema /kuona ni nini na aina gani ya malezi yanatakiwa.
hangamoto anavyosema. Ila mimi ni kinyume na Mzee Changamoto pia watu wote wanaoona ni haki watoto wapigwe viboko.

6 comments:

  1. Dada yangu, ulipigwa sana viboko nini?
    Kwanini?

    Je, Ulinyanyaswa ama ulikuwa mtundu? Au mvivu ama mkorofi?
    Je ni lipi haswa?

    Leo hii, sifa yako kitabia ni ipi haswa? Kama zile za wakati unachapwa? Au viboko vimekuathiri vipi?

    Mimi nakumbuka kwamba wazazi walichuma fimbo pale ambapo ilibidi waninyuke kweli nisisahau na nisirudie kosa langu!
    Sikuwa mtundu lakini utoto na ujana unakuja na vijijaribio fulani ambavyo vinaweza visieleweke kwa wazazi ama watu wazima wanaokuzunguka.

    Hebu nikumbuke kwanini nilichapwa.

    Nilipigwa marufuku kupanda miti. Au ni kukwea? Sijui vipi siku hiyo nikajikuta nakwea mnazi uliopo uwani. Shangazi akaanza kunikanya, SIKUMSIKILIZA. Yeye alikuwa hana haki ya kunipiga (ingegeuka kuwa vita kubwa!), hivyo akawa ananiambia ATANISHTAKI.
    Nilikaidi.

    Ilikuwa jioni hivi, nimeshafika juu kidogo, ghafla nikasikia gari la dingi likisimama getini. Duh! Noma! Wamewahi kurudi!
    Sikuruka, niliteleza fasta kurudi chini! Matokeo yake nilijichubua vibaya sana ubavuni mwa tumbo. Nikapata kidonda kikubwa cha wazi!

    Dah! Nitajieleza vipi? Shangazi alishaenda kuwapokea, hakuona taharuki yangu na hakujua nimejiumiza.
    Siku hiyo na kwa wiki nzima ilinibidi niwe msanii mwenye maumivu makali sana! Ilibidi niwasalimie wazazi huku nimeficha kidonda. Nioge kwa maumivu, nijitibu mwenyewe kisiri! Kidonda kilianza kuota usaaa na kuwa kikubwa zaidi!

    Sikuweza vumilia, ikabidi nimwonyeshe Maza bonge moja la donda weekend moja baadaye!
    Utadhani aliona utumbo wangu kwa jinsi alivyoshangaa kukiona kidonda! Maelezo yangu nayo yalizidi kumshangaza na kumkera, haswa ilipobidi nikiri kukwea mnazi kinyume na maagizo ya wazazi wangu!

    Kumkaidi shangazi, kuficha kidonda! Dah, nilikuwa na jalada kubwa sana.
    NILICHAPWA na kidonda changu!!!!!

    Unajua, sikulaumu double maumivu! Nilistahili! Tena adhabu zangu zilikuwa zimejipanga saaaafi! Ukaidi ni wangu na ujinga ulikuwa wangu! Droo!

    Nikikumbuka enzi zile, silaumu sana nidhamu kwa bakora. Kuna wakati ilibidi. Nyumbani na pia shuleni.(Nikiwa chekechea, niliwanyanyasa watoto wenzangu kwa kuwavuta masikio hadi wanasimama kwenye vidole. Nikashtakiwa. Mwalimu mbele ya darasa akaniadhibu hivyohivyo! Nikiwa nimesimamia vidole, masikio yanauma ile mbaya, nikamnasa kibao! Khee! Nikakimbia! Ikawa mwisho wa chekechea!).

    Utotoni kuna hatari sana. Udadisi wetu mara nyingi unahitaji kuthibitiwa.
    Utamuonya vipi mtoto asicheze na wembe? Au moto? Bila karipio? Lakini ni mara ngapi mtoto atawasha moto kinyume na maagizo? Usemi ule unasemaje?

    Mzazi anayeshusha mjeledi kama vile mwanae ni mfungwa atakuwa naye ni mwathirika wa viboko au mbaya zaidi. Mzazi anatakiwa kumchapa mtoto akifoka, akiuliza, akitaka jibu la adabu! Hamkumbuki jamani?

    Eti kuna raha fulani fimbo inapochumwa(unapoichuma mwenyewe!), unasubiri, machozi yanakulenga, ndugu yako anakukejeli!

    Ni sawa na kukabiliana na Boss ofisini, memo umepata, umeitwa, sasa ni nidhamu yako dhidi ya zero zake ama ni wewe uache kazi ama yeye?

    Maisha ni NIDHAMU ama ADHABU. Ukimchapa mtoto, hauna nia ya kumuumiza. Nia ni kuweka alama ya kudumu kwamba kitu fulani ni punishable! Kina adhabu.

    Tangu unapong'ata titi la mama naye anakufinya uache, ni namna ya mawasiliano. Wengine tumezaliwa watu wa kuuma tu! Hatujua kupuliza!

    ReplyDelete
  2. Nilichezea sana viboko kuanzia nyumbani hadi shuleni, na hii ilikuwa kwa sababu ya utundu wangu kuanzia home mpaka shule
    Dingi alikuwa na tabia ya kukukanya kila mara lakini siku akishika kiboko anaanza na kosa hata la miezi kadhaa iliyopita na wewe usha sahau, basi hapo utasomewa mashtaka yako yote hata kama yako kumi halafu ndio anakutandika kisawasawa
    Shule nilisoma ya kijeshi (jitegemee) kwa hiyo viboko vilikuwa kama chai tu na ilifika mahala tukawa tumezoea na hatuogopi ila tulikuwa tunaogopa adhabu za kijeshi tu
    Kuhusu watoto mimi mwanangu huwa simchapi bali nampa adhabu kama vile kwenda kulala hata kama katoka kulala, au kumuacha kama mnatoka out kidogo au mnaenda shamba si unajua watoto wa kibongo wanavyopenda gari hawachoki ingawa wanapanda kila siku kwenda na kurudi shuleni. Siku moja nilimchapa ingawa iliniuma, alitia maji kwenya tanki la gari nikamkanya kesho yake akatia tena maji ya sabuni, nilimtandika maana nilikasirika sana na alinitia hasara mara mbili

    ReplyDelete
  3. Dada! Mimi nasema kuwa fimbo zaweza kuwa USED na sio ABUSED. Ni adhabu kama adhabu nyingine yoyote ile. Kama time out, kama kumnyima mtoto trip ya mall, kama kumfinya, kama adhabu yoyote ile.
    Suala hapa ni kwanini itumiwe, wapi itumiwe, vipi itumiwe na kwa nani itumiwe ili nini kifanyike.
    Naeleweka lakini?

    ReplyDelete
  4. Kamala nimekuelewa.

    Kaka Master kwanza nasema karibu sana na asante kwa maoni yako. Nasema tu hapana SIKUPINGWA sana viboko. Ila tu sipendi vibiko na sipendi kumpiga mtu.

    Bennet nakuelewa mara nyingine ni kweli mtu unakasirika na kufanya kitu usichotarajia.

    Mzee wa Changamoto Kama ni adhabu kama adhabu nyingine kwa nini usitumie hizo nyingine na kuacha kiboko?

    ReplyDelete
  5. Watu wengi hususani walezi wanafikiri kulea ni kuhakikisha mtoto kala, kavaa na kalala.

    Kwa malezi yetu kulingana na hatua za ukuaji wa binadamu, kila hatua ina mambo yake ambayo kama yatatimizwa, ni dhahiri kuwa binadamu huyo atakuwa ktk mstari ulionyooka.
    Hapa namaanisha kuwa malezi yanatakiwa wawe ni ya kisaikologia(psychology of human development)
    Mtoto aliyekuzwa kwa kuzingatia kanuni hizi za kisaikologia atakuwa na uwezo mkubwa kabisa kuweza kukabiliana ipasavyo na mazingira, kwani atakuwa na uwezo wa kutambua baya na zuri.

    "umewahi kujiuliza ni kwa nini kuna watu wanaoweza kuvumilia kutofanya ngono mpaka watakapooa au kuolewa na kuna wengine wameshindwa kabisa!


    Ikumbukwe kuwa fimbo ni adhabu ambayo ilitumiwa na wakoloni kuwachapa mababu zetu.Wazazi wengi huwa wanakosea kwani huwa wanatoa adhabu hususani hii ya kuchapa bila kuuliza au kuchunguza kwanza kwa nini mtoto akafanya kosa fulani. Kukosea kwa mtoto kusichukuliwe kuwa ni kitu ambacho ni negative.Kumchapa mtoto kunaweka tu vitisho lakini si lazima kumfanye mtoto kutokurudia kosa.Anayefaa kuelewesha,aeleweshwe, ambaye bado inamaana kuwa bado una nafasi nzuri ya kumjenga vizuri ili baadae asifanye mambo ambayo utapelekea kumchapa viboko huku ukisahau kuwa umechangia sana mtoto kutokuwa na maadili.

    "mtu mzima akikosea huwa anachapwa viboko? Ni kwa namna gani huwa wanaelimishana? Huwa wanatishana?
    Kwa nini watoto wasielezwe waliyokosea, hata mtoto akirudia kosa lile lile, si kosa lake, bali kuna tatizo ktk malezi na si vizuri kumwadhibu kwa fimbo na hata adhabu ambazo zitamharibu kisaikologia bali ziwe za kumjenga kisaikologia.


    " parents/guardians are the main composers of any melody from a child"


    Binafsi sikubaliani na adhabu hii ya kuwachapa watoto viboko kwani ni adhabu ambayo kwanza tuliipata baada ya kutumiwa na wakoloni ktk kudhalilisha mababu zetu na pili adhabu hii haijengi bali inaweka vitisho ni kwa kosa moja moja. Mtoto akifanya kosa na akichapwa ataogopa kurudia kosa lile lakini atakuwa huru kufanya kosa jingine, na atajua kuwa ni kosa baada ya kuchapwa na utaratibu huu utaendelea.

    ReplyDelete