Wednesday, June 17, 2009

SAFARI YA SONGEA MWAKA 2009

Najua wengi mnakumbuka mwaka huu mwanzoni kabisa nilikuwa nyumbani Tanzania. Ni kwamba baada ya wiki moja, nilikwenda madukani kununua vyombo ilikuwa siku ya Ijumaa. Si mnajua Ijumaa ni siku ya watu kupita madukani kuomba. Songea ni hivyo sijui sehemu nyingine Tanzania pia. Basi nikiwa katika harakati za kulipa akaja mtu mmoja au niseme alikuwa (kijana)au pia naweza kusema alikuwa na "changamoto za kifikra" (mentaly challenged)?
Alivyoonekana alikuwa kichaa. Akamwambia mwenye duka naomba hela akamjibu leo hakuna.

Akageuka kwangu we dada je? naomba hela nami nikamwambia sina. Akanipiga kofi na akaondoka zake. Kwa kweli nilishikwa na mshangao sana. Nimeandika hii kufananisha na mambo anayofanya dada Koero ninavyoamini mimi angekuwa pale angeacha kununua vyombo na angempa yule mwombaji. Nimejifunza mengi sana katika mada zake dada Koero asiyesoma basi chukuni muda na someni. Koero Mkundi hasa hii mada ya ANITA NA MIKASA YA DUNIA .Nashukuru Mungu ametuumba tofauti. Ni hayo tu kwa leo ni mada fupi lakini ina ujumbe wake.

6 comments:

  1. Ukikosa wamlamba mtu kofi!!! Ama kweli maajabu hayo. Pole ingawa maumivu umeyasha yasahau.
    Omba omba niliokutana nao Ujerumani ni wazungu, na kama nilikuwa na mtu mweupe, walikuwa hawamwombi wanakuja kwangu, mara nyingi walikuwa wazee wachafuuu, au vijana wengi wenye ulemavu wa viungo kama mguu, ingawa walikuwa smart kidogo. Sikuona vibao huko, ila wengi wao ukiwapa, wanaenda kujichana kabia angalau kamoja ka kulalia.

    ReplyDelete
  2. Pole kwa kibao... maisha hayo.

    ReplyDelete
  3. Pole sana,lakini usimlaumu sana,umesema huyo kijana ni kichaa lakini alijua anachokifanya mbona mwenye duka hakumpiga?alijua akimpiga hataruhusiwa tena kuingia hapo dukani.

    ReplyDelete
  4. Duh! Alikupiga kofi?? Pole dada.

    Ila sijui wanakuwa depressed mpaka hawajui wanachofanya coz my friend alionana na mtu pia akamuomba hela then rafiki yangu akasema hana. When she was walking away yule mtu akamuita the N word.

    They will just say anything but it's not to take it serious

    ReplyDelete
  5. DUH!!!!!!!!!!
    Lakini dada Yasinta inawezekana hata mimi kama ningempa angenipiga kofi labda angeona ni ndogo.
    Hata hivyo nakupa pole dada yangu.

    ReplyDelete