Ni kweli. Jumatatu ya wiki hii nilitazama kipindi kimoja kinaitwa "Music and Your Brain" na kilikuwa kipindi chenye kuhabarisha kweli kuhusu faida za muziki. Mbali na faida zake nyingine wanasayansi sasa wameshathibitisha kwamba muziki unasaidia ubongo kukua na kuimarika zaidi hasa katika maeneo muhimu yanayoshughulikia utambuzi, uundaji wa dhana dhahnia n.k. Ndiyo maana vingunge wengi wa sayansi (mf. Albert Einstein) na wengineo walikuwa ni wanafunzi wa muziki na walikuwa wanacheza angalau ala moja ya muziki. Hitimisho: muziki una faida kubwa katika kukua na kupevuka kwa ubongo. Hapa nakubaliana nawe moja kwa moja!
Mmhhhhhh! Swadakta. Nimeburudika na (naamini) nimenufaisha ubongo kama alivyosema Profesa Matondo. Asante kwako Da Yasinta kwa burudani na Profesa kwa kututanabaisha kuhusu faida za muziki ambao wengine tunausikiliza kila uchao lakini hatujui faida zake za ndani na uhusiano wake na "chaji" za ubongo. Baraka kwenu
Ni kweli. Jumatatu ya wiki hii nilitazama kipindi kimoja kinaitwa "Music and Your Brain" na kilikuwa kipindi chenye kuhabarisha kweli kuhusu faida za muziki. Mbali na faida zake nyingine wanasayansi sasa wameshathibitisha kwamba muziki unasaidia ubongo kukua na kuimarika zaidi hasa katika maeneo muhimu yanayoshughulikia utambuzi, uundaji wa dhana dhahnia n.k. Ndiyo maana vingunge wengi wa sayansi (mf. Albert Einstein) na wengineo walikuwa ni wanafunzi wa muziki na walikuwa wanacheza angalau ala moja ya muziki. Hitimisho: muziki una faida kubwa katika kukua na kupevuka kwa ubongo. Hapa nakubaliana nawe moja kwa moja!
ReplyDeleteMmhhhhhh! Swadakta. Nimeburudika na (naamini) nimenufaisha ubongo kama alivyosema Profesa Matondo. Asante kwako Da Yasinta kwa burudani na Profesa kwa kututanabaisha kuhusu faida za muziki ambao wengine tunausikiliza kila uchao lakini hatujui faida zake za ndani na uhusiano wake na "chaji" za ubongo.
ReplyDeleteBaraka kwenu
Huyu kaka yupo makini, sauti imetulia sana, yaani unapata mantiki ya wimbo kwa sababu ya utulivu wake. Big up Marlow na Asante Da'Yasinta
ReplyDelete