VIPIMO
(Manda ya sambusa ya tayari Kiasi zinavyouzwa
Kiasi cha sambusa 40-50)
Mafuta ya kukaangia Kiasi
Nyama ya Kusaga kilo moja na nusu 3LB (Pounds)
Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 Vijiko vha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Pilipili manga 1 kijiko cha supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Chumvi Kiasi
Vitunguu maji vilivyokatwa
(chopped) 3 Vidogo au 2 Vikubwa
Kotmiri iliyokatwa (chopped) Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Pika nyama ya kusagwa kwa kutia chumvi, thomu na tangawizi, pilipili na ndimu.
2. Kabla haija kauka tia Garam masala.
3. Zima moto acha kidogo ipoe tia vitunguu na kotimiri.
4. Funga sambusa katika manda kama kawaida.
5. Pika sambusa katika mafuta ya moto hadi ziwe nyekundu na zikiwa tayari kuliwa.
Duh!! Matamanisho hayo. Ntatengeneza zisizo na nyama week end.
ReplyDeletenina penda sambusa kwasababu zina noga sana na fanta nanasi baridi!!
ReplyDeleteErik baraka.wa ruhuwiko songea!!
Bora maana tulikuwa hatujala tunaongea tu, mara ya mwisho tulikula maandazi mpaka leo, ngoja nikaandae fresh juice ya parachichi, embe na chungwa
ReplyDeleteHapa unanitoa udenda!
ReplyDeleteSambusa na vitumbua ndio vyangu. Maandazi , Mikate na keki naweza kuwaachieni!
Na bado kiporo cha wali wanazi na maharage ya nazi unapanda kishenzi tokea enzi za bodingi skuli!
mimi simo!
ReplyDeleteSambusa.! We acha tu.
ReplyDeleteWote mnakaribishwa hapa Ruhuwiko kwani kila siku hazikosekani. Karibuni sana. Na msiwe na wasiwasi zipo za mboga na nyama. Ila nikweli sambusa tamu sana.
ReplyDeleteMhh! patamu hapo dadangu, kotmiri ndio nini?
ReplyDeleteMmm huwo msosi ni noma lazima nitajifunza jinsi ya kupika sambusa za nyama
ReplyDeleteLakini Dada yangu hiyo Garam masala na Kotrimil ni nini
Kazi nzuri
Off course katika vitafunio vitamu hasa kwa soda na chai sambusa au samosa ni namba moja, napenda kuliko chapati, maandazi na mikate. mafunza mazuri
ReplyDelete