Tuesday, May 12, 2009

TUDUMISHE UTAMADUNI WETU WA ASILI


Hapa ni barabara ya Morogoro-Iringa niendapo Songea lazima nisimame na kununua kitu.


Watu tunatoka mbali, watoto wanacheza kuwa wao ni akina mama. Nimekumbuka mbali sana!!

9 comments:

  1. Vikapu na mapambo ya asili hapo hunivutia sana. Mara kadhaa huwa nanunua hapo.

    ReplyDelete
  2. Kumbe! Yah, hakuna kitu kizuri kama mambapo ya asili au niseme vitu vya asili kwa ujumla.

    ReplyDelete
  3. mwenzangu, hapo umenitonesha yaani nengepita hapo nigebeba vyote, yaani wadau wangu wangefurahi sana, dah sijui nitavipataje, yaani huu ndio msimu wake, yaani summer ikiisha na festival hakuna tena.

    ReplyDelete
  4. Hata sijui dadangu, ningejua ningekusaidia. Nasikitika siwezi kukupa hata ushauri kuwa ufanyeje?

    ReplyDelete
  5. du, sijaona vijomela hapo, nami siwezi kunywa ugimbi bila kutumia chimojela

    ReplyDelete
  6. Ukitaka chijomela basi nenda sehemu za Mgazini au Peramiho huko ndo utavipata

    ReplyDelete
  7. habari za hapa..nimependa sana kwa kasi unayoendelea nayo kublog


    tupo pamoja dada yangu nimepata ujumbe wako..

    napita hapa kila siku sema siku nyingine napita kwa kasi ya ajabu.

    nimependa sana ulivyoandika kuhusu Likuyu Fusi.

    Nilibahatika kuwepo huko kwa miezi 2 mwaka 2005.Moja ya kituo changu cha kazi ilikuwa pia Likuyufusi..

    Nilikuwa nafanya shughuli za jamii kuwaelimisha wakungu na wanajamii jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.Nilikuwa na shirika linajulika ORES (Orphans Relief Service -TANZANIA )

    nimeacha marafiki wengi sana likuyu fusi na songea kwa ujumla na wilaya nyingine kama namtumbo,mbinga..

    nilijifunza pia kutengeneza pombe ya kienyeji inayoitwa myakaya...aaa..aahaaa ilikuwa uzoefu mzuri sana.

    TUPO PAMOJA

    ReplyDelete
  8. Kaka Edo! Ni kweli ulipotea nashukuru umerudi tena. Likuyu Fusi, ulikuwa unatengeneza myakaya je ulikunywa pia LOL! kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  9. Yasinta hapo umenikumbusha nyumbani,nakumbuka safari za Dar Iringa,hivi vitu vya asili ni vizuri sana na madukani ukivipata huku bei yake ni tofauti sana,tatizo watu kama hawa hawana msaada wa kutafutiwa masoko ya nje,lakini nauhakika kama wakipatiwa soko la kuuza bidhaa zao nje zitauzika sana.Nani alaumiwe?

    ReplyDelete